karibu watanzania wote ni wezi (WAWEKEZAJI KUWENI MAKINI)

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,035
326
inasemekana zaidi ya 100% maisha yao yaantegemea deal. Deal ni nini? Deal ni (WIZI). Kuanzia watanzania wa ngazi za juu, waajiriwa na waliojiajiri wanaishi kwa kutafuta deal ambazo kwa asilimia mia ni wizi . Na hata ambao hawapigi deal ni kwamba wanatamani ila tu waoga au wamekosa hiyo nafasi ya kupiga deal au kuiba
 
Tusipende kujiponda watanzania kwenye kila kitu, dili ziko kila mahali duniani
 
Inaonekana wewe ni mwizi pia ndio maana unaamini kuwa watanzania ni wezi,asilimia kubwa ya watanzania wapo vijijini,wanaiba nini?Maisha yao yanategemea deal gani kama si kilimo na ufugaji?
 
inasemekana zaidi ya 100% maisha yao yaantegemea deal. Deal ni nini? Deal ni (WIZI). Kuanzia watanzania wa ngazi za juu, waajiriwa na waliojiajiri wanaishi kwa kutafuta deal ambazo kwa asilimia mia ni wizi . Na hata ambao hawapigi deal ni kwamba wanatamani ila tu waoga au wamekosa hiyo nafasi ya kupiga deal au kuiba
ukitafakari sana ni kuwa tuna percentage ndogo iliyo juu na kutokana na mfumo wa maisha na katiba ya nchi ndio wana haki ya kujigawia kinachopatikana na hao ndio wezi. Nakiri kuwa bibi yangu hapa kijijini na baba yangu wanafanya kazi kutwa nzima ili waweze kuishi!
Nimemuona Rais M7 jana kwenye TV akiwaelezea wakulima na wafugaji wa Uganda kama "wealth maker". Kwamba wale watu ndio muhimili ya nchi na ndio watengenezaji wa utajiri wote badala ya hawa wezi wa maofisini na wachuuzi.

Nakuhakikishi ndugu yangu ikija KATIBA MPYA hapa iliyoundwa bila fitina na unafiki wa watawala wetu hawa, miaka 7 ni mingi kushuhudia Tanzania ikiwa kwenye level ya Ghana, Botswana na hata Malaysia!

Umefikirria tabaka dogo sana la watanzania, ambalo pengine ndilo wewe upo ukadhani kuwa wote wamo humo, sikweli!
 
na yule mjerumanai aliyekamatwa juzi akifanya lile deal la gustavic acid /chanjo ya wanyama naye ni mtz?deal ni whole world tutake radhi wewe mtoa mada tanganyikajeki
 
Last edited by a moderator:
inasemekana zaidi ya 100% maisha yao yaantegemea deal. Deal ni nini? Deal ni (WIZI). Kuanzia watanzania wa ngazi za juu, waajiriwa na waliojiajiri wanaishi kwa kutafuta deal ambazo kwa asilimia mia ni wizi . Na hata ambao hawapigi deal ni kwamba wanatamani ila tu waoga au wamekosa hiyo nafasi ya kupiga deal au kuiba

Hata Kardinali Pengo alisema kuwa mnaopiga kelele za ufisadi ni kweli yanatoka rohoni, mnauchukiakwa dhati au ni kwa vile hamna nafasi ya kufanya ufisadi
 
Tusijitetee sana kwenye hili. Watanzania wengi wanakera sana. Maadili yamepotea kabisa. Hili swala lipo kila mahali. Ni kansa ambayo inatakiwa kuondolewa la sivyo nchi haitafika popote. Nitakupa mifano michache:

Maofisini watu wengi dili zao ni namna ya kumwibia mwajiri, hata wakilipwa ngapi. Kila siku tunasikia jinsi ambavyo mabilioni yanavyokwapuliwa. Walioiba EPA ni watu wanaolipwa vizuri sana kupita nchi nyingi za Afrika. Wafanyakazi wadogo ndiyo usiseme wanakula sahani moja na majambazi ambao wanawapa habari nyeti za ofisini kama vile pesa zitasafirishwa lini, n.k.

Huko vijijini nako kuna matatizo. Ukisafiri na gari na bahati mbaya upate ajali unavamiwa na wananchi wanakuja siyo kukusaidia bali kukuibia hata kukuua. Hili lipo Tanzania, na huenda ni Tanzania peke yake. Ni aibu kubwa. Inajulikana na tusijidanganye kuwa halipo.

Wakulima vijijini wanajaribu kudanganya kwa kuchanganya mazao yao na mazao fifi, mawe, mchanga, na hata kulowanisha na maji.

Wafanyabiashara wadogo kama wauza nyanya, vitunguu, mahindi, n.k. wanadanganya kwa kuweka takataka ndani, kukata madebe, kupanga pyramid ndani, kugonga debe libonyee kabisa, n.k. Watanzania wanaamini kufanya biashara ni kudanganya!
 
Huyo mjerumani hawezi kuiba bila kupata ramani kutoka kwa wa tanzania wenyewe. Ukienda vijijini na ukaonekana wewe ni mgeni katika ule mji au umetoka mjini ni lazima wakutengeneze. Na huko uswahili wanaotoa deal za wenzao kuibiwa si wa huko huko uswazi . I mean masikini kwa masikini wanaibiana . So sio watu wa level ya juu tu wanaopiga deal au kuiba hata wa chini ni wezi
 
Baba Riz 1, kala dili la suti kali kamwachia mwarabu hotel, Kale ka naibu waziri kalikula dili za kwenda kutalii nje, kakatoa dili pale bandarini, mama Rwakatare kala dili la umeme wa dezo, mama kilango kachangamkia la madini na la kiwanda fafa cha tangawizi, Magufuli alikula dili akapindisha makao makuu ya mkoa kuwa chato kijijini kwake pia baadhi ya vipande vya barabara vilivyosalia kwenye mikataba alivihamishia jimboni kwake
Baba Riz 1, kahamasisha bandari ya Bagamoyo kuwa ndo bandari kubwa, kuliko ya bongo daslamu, barabara kubwa na vitega uchumi vinamfuata Msoga sasa
Dili la Riz kubambwa na candy dingi kauza dili la gesi kwa wachina
 
inasemekana zaidi ya 100% maisha yao yaantegemea deal. Deal ni nini? Deal ni (WIZI). Kuanzia watanzania wa ngazi za juu, waajiriwa na waliojiajiri wanaishi kwa kutafuta deal ambazo kwa asilimia mia ni wizi . Na hata ambao hawapigi deal ni kwamba wanatamani ila tu waoga au wamekosa hiyo nafasi ya kupiga deal au kuiba
kwa hiyo na weye mwizi??
 
Ungetaka kuwa mkweli kabisa, basi ungeandika hivi:-...

Wawekezaji wote ni wezi, Watanzania kuweni makini !!
 
Nadhani mfumo wetu ndio unaoandaa tabaka la wezi. Mfano, kuna thread ngapi humu JF members wanauliza ni fani ipi ina ajira nyingi na maposho mengi? Hapo maana yake kipaji kinasubiri kwanza.
 
Back
Top Bottom