Karibu Tanganyika

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Yaaani kurudi kwa Tanganyika nafananisha kabisa na siku tuliopata Uhuru, ni furaha kubwa ilioje kuiona Nchi yangu Tanganyika inarudi ,naiona siku hii ni siku ambayo wale wasiowahi siku ile ya kupata Uhuru hii itakuwa kama second Chance.

Vipi Serikali yaTanganyika itarudi huu ndio mtihani kwa waTanganyika la si hivyo watazidi kuuwana na kuchinjana kama tuonavyo kwenye visa vya wakulima na wafugaji.

Inahitaji kuanza mchakato wa kuipanga ni jinsi gani serikali itarudi ,je itakuwa ni hii ya muungano ndio iwe ya Tanganyika ,hapa naiona hali ya viongozi wengi waliomo Serikalini au wote kutopenda kuona serikali ya Tanganyika inarudi.



Akielezea mchanganuo wa takwimu hizo, alisema kwa upande wa Tanzania Bara, asilimia 13 walitaka serikali moja, wakati asilimia 24 serikali mbili na asilimia 61 serikali tatu.

Alisema kwa upande wa Zanzibar, asilimia 34 walipendekeza serikali mbili, asilimia
60 Muungano wa Mkataba na asilimia 0.1 (watu 25) serikali moja.
 
CCM wamewachwa kwenye mataa kwa kung'ang'ania takwimu ,yaani hata sijui sasa watakamata wapi kila wanapokamata hupewa muda kisha hupigwa na chini ! Leo wameadhirishwa vibaya sana sana !
 
Back
Top Bottom