Jinsi Muungano unavyoathiri Waislamu wa Tanganyika wakati wale wa Zanzibar wakineemeka

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,487
51,064
Katika nchi hii, Muhimili wa Power upo katika makundi makubwa mawili. (a) Wakiristo wa Tanganyika (b) Waislamu wa Zanzibar.

Haya Makundi ndiyo makundi makuu yenye mamlaka za kisiasa hapa nchini. Hali hii inawaathiri sana Waislamu wa Tanganyika, nitaeleza.

a) Kutokana na kwamba kule Zanzibar Waislamu ni Majority, basi nafasi yoyote ya Uteuzi ktk serikali ya Muungano, kama mzanzibari ndiye atateteuliwa, basi kuna probability kubwa kuwa mtu huyo akawa Muislamu. Na hivyo basi wakishateuliwa kushika hizo nyadhifa Inakuwa ni vigumu sana kwa nafasi nyingine zilizobaki kuteua waislamu wengine wa Tanganyika kujaza au kuchukua nafasi hizo zilizobaki, Ili isije kuonekana teuzi zimelalia watu wa dini moja. Kwa hivyo basi, nafasi zilizobaki watateuliwa Wakiristo wa Tanganyika.

Chunguza teuzi nyingi za Serikali, hata serikali hii ya awamu ya Sita. Utaona wazi kuwa kama aliyeteuliwa ni muislamu, basi kunakuwa na uwezekano mkubwa wa mteuliwa huyo ni Muislamu wa Zanzibar badala ya Muislamu wa Tanganyika.

b) Tatizo hilohilo pia linajitokeza katika Ajira na Utumishi. Wazanzibari kwa mujibu wa Makubaliano ya kimuungano, wameshatengewa asilimia 25 za ajira zote za Muungano. Halafu asilimia 75 zimebaki kwa Watanganyika. Sasa huku Tanganyika maana yake ni kwamba Wakiristo wa huku na Waislamu wa huku na watu wachache wa dini nyingine ndo wanagombea asilimia 75 zilizobaki.

Hii pia inawaathiri Waislamu wa Tanganyika kwa maana, HR Manager au mamlaka za ajira zinapoletewa requirement ambayo tayari 25% ni watu wa dini moja, Ni vigumu kudhani watakuwa malaika kuongeza namba ya watu wanaofanana na hao ambao tayari wameshalamba shavu. Watataka watu wa Imani nyingine ili kuoffset imbalance ya kiimani. Hapa ndipo Waislamu wa Tanganyika inapokula kwao!

KWA HIYO
1. Huu muungano, kwa namna Ulivyo Waislamu wa Tanganyika ni kama Pawns, ila Wakiristo wa Tanganyika na Waislamu wa Zanzibar ndiyo King Makers

2. Ipo haja ya kukaa mezani seriously na kuangalia aina gani ya Muungano tunayoitaka (Kama muungano wenyewe unamake sense anyway), Na tukikaa Mezani tuzungumze Masilahi serious ya kila kundi, siyo habari za tumeoleana kwa muda mrefu. Mambo ya kuoa na kuolewa ni personal hayana maslahi mapana kwa Taifa.

3) Waislamu wa Tanganyika sasa nao waamke, waanze kudai uwakilishi zaidi serikalini, katika teuzi mbalimbali za kuhudumu serikalini n.k

Inabidi wadai kunufaika ipasavyo na matunda ya uhuru (walioupigania sana wakati ule wa kudai uhuru) ikiwemo ajira, na utumishi wa ndani ya serikali
 
Nakubaliama na wewe 100%. Hali ni mbaya zaidi CCM. Ukiangali structure ya uongozi ya CCM utaona nafasi walizonazo Waislam wa Zanzibar ni nyingi kuliko wale wa Bara. Na hii inatokana na kwamba CCM wenyewe wanataka Wazanzibar wawepo kwenye uongozi ambao automatic ni Waislam so inapokuja nafasi wapewe watu wa Bara, nafasi wanachukua Wakristu kwa zaidi ya 80%
 
Vipi kuhusu Wakristo wa Zanzibar? Japo ni "minority" lakini kupitia hoja yako una maoni gani kuhusu kundi hili? Jielekeze katika haki zao, uhuru wao, na amani yao kupitia katiba ya JMT.

Vipi kuhusu makundi mengine, mathalani dini za kijadi, Kihindu n.k. Nafikiri ni vyema tukajitazama kama taifa, zaidi ya kujiangalia kupitia itikadi zetu za kidini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwaanzishia uzi ili kujua nao wanaathirika vipi itapendeza sana. Itatusaidia kuutazama upya muungano wetu.
 
Ingekuwa busara tukapata baraza la mawaziri la Tanganyika 1961 - 1963 na baadae ajira serikalini katika kipindi hiko ili tupate kulinganisha. Huenda tunazungumza kwa kuhisi tu lkn mambo sio kama tunavyofikiria.
 
Naona kisa kupewa huyo Mzanzibari Uenyekiti wa bodi ndio umekosa raha.

Nyie viumbe mna matatizo sana, wakati wa Magufuli mlikuwa mnalalamika anapendelea wakristo wenzake, leo amekuja mwenzenu bado mnaendelea kulalamika anapendelea kule atokako hata kama anawateua waislamu wenzenu..

Sikutegemea kwa namna mnavyobebwa huku bara kwenye teuzi siku hizi, bado mtazitolea macho nafasi za Zanzibar ikiwa bado wanapewa waislamu wenzenu, huu ubinafsi sijawahi kuuona hapa duniani, nyie iko siku mtatafunana..
 
Vipi kuhusu Wakristo wa Zanzibar? Japo ni "minority" lakini kupitia hoja yako una maoni gani kuhusu kundi hili? Jielekeze katika haki zao, uhuru wao, na amani yao kupitia katiba ya JMT.

Vipi kuhusu makundi mengine, mathalani dini za kijadi, Kihindu n.k. Nafikiri ni vyema tukajitazama kama taifa, zaidi ya kujiangalia kupitia itikadi zetu za kidini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa hawezi gusa, hao viumbe ni selfish sana, na kulalamika ndio jadi yao.
 
Angalia uteuzi ufuatao wa mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri ardhini( LATRA).

Walioteuliwa majority ni Waislamu wa Zanzibar na Wakiristo wa Tanganyika.

IMG-20230117-WA0018.jpg

IMG-20230117-WA0019.jpg

Sijui kama mambo ya Usafiri wa ardhini ni jambo la Muungano anyway, Lakini unaona mamlaka za Uteuzi zinajaza Waislamu wa Zanzibar tupu. Huku wale wa Tanganyika wakiwa kama Yatima.

Huu muungano ni pasua kichwa!
 
Naona kisa kupewa huyo Mzanzibari ujumbe wa bodi ndio umekosa raha...

Nyie viumbe mna matatizo sana, wakati wa Magufuli mlikuwa mnalalamika anapendelea wakristo wenzake, leo amekuja mwenzenu bado mnaendelea kulalamika anapendelea kule atokako hata kama anawateua waislamu wenzenu..

Sikutegemea kwa namna mnavyobebwa huku bara kwenye teuzi siku hizi, bado mtazitolea macho nafasi za Zanzibar ikiwa bado wanapewa waislamu wenzenu, huu ubinafsi sijawahi kuuona hapa duniani, nyie iko siku mtatafunana..

Hii mada iko objective. Utapotea sana ukiijadili kwa hisia, udini au ushabiki.

Hii mada siyo ya kidini ndiyo maana Inahoji namna gani waislamu wa upande mmoja wanufaike zaidi kuliko wa upande mwingine licha ya wote kuwa dini moja.

Kwa hiyo weka hisia pembeni, njoo tujadili hili suala la kijamii tukiwa open minded!
 
Katika nchi hii, Muhimili wa Power upo katika makundi makubwa mawili. (a) Wakiristo wa Tanganyika (b) Waislamu wa Zanzibar.

Haya Makundi ndiyo makundi makuu yenye mamlaka za kisiasa hapa nchini.
Hali hii inawaathiri sana Waislamu wa Tanganyika , nitaeleza

a) Kutokana na kwamba kule Zanzibar Waislamu ni Majority, basi nafasi yoyote ya Uteuzi ktk serikali ya Muungano, kama mzanzibari ndiye atateteuliwa, basi kuna probability kubwa kuwa mtu huyo akawa Muislamu. Na hivyo basi wakishateuliwa kushika hizo nyadhifa Inakuwa ni vigumu sana kwa nafasi nyingine zilizobaki kuteua waislamu wengine wa Tanganyika kujaza au kuchukua nafasi hizo zilizobaki, Ili isije kuonekana teuzi zimelalia watu wa dini moja. Kwa hivyo basi, nafasi zilizobaki watateuliwa Wakiristo wa Tanganyika.
Chunguza teuzi nyingi za Serikali, hata serikali hii ya awamu ya Sita. Utaona wazi kuwa kama aliyeteuliwa ni muislamu, basi kunakuwa na uwezekano mkubwa wa mteuliwa huyo ni Muislamu wa Zanzibar badala ya Muislamu wa Tanganyika.

b) Tatizo hilohilo pia linajitokeza katika Ajira na Utumishi. Wazanzibari kwa mujibu wa Makubaliano ya kimuungano, wameshatengewa asilimia 25 za ajira zote za Muungano. Halafu asilimia 75 zimebaki kwa Watanganyika. Sasa huku Tanganyika maana yake ni kwamba Wakiristo wa huku na Waislamu wa huku na watu wachache wa dini nyingine ndo wanagombea asilimia 75 zilizobaki. Hii pia inawaathiri Waislamu wa Tanganyika kwa maana, HR Manager au mamlaka za ajira zinapoletewa requirement ambayo tayari 25% ni watu wa dini moja, Ni vigumu kudhani watakuwa malaika kuongeza namba ya watu wanaofanana na hao ambao tayari wameshalamba shavu. Watataka watu wa Imani nyingine ili kuoffset imbalance ya kiimani. Hapa ndipo Waislamu wa Tanganyika inapokula kwao!

KWA HIYO
1. Huu muungano, kwa namna Ulivyo Waislamu wa Tanganyika ni kama Pawns, ila Wakiristo wa Tanganyika na Waislamu wa Zanzibar ndiyo King Makers

2. Ipo haja ya kukaa mezani seriously na kuangalia aina gani ya Muungano tunayoitaka ( Kama muungano wenyewe unamake sense anyway), Na tukikaa Mezani tuzungumze Masilahi serious ya kila kundi, siyo habari za tumeoleana kwa muda mrefu. Mambo ya kuoa na kuolewa ni personal hayana maslahi mapana kwa Taifa.

3) Waislamu wa Tanganyika sasa nao waamke, waanze kudai uwakilishi zaidi serikalini, katika teuzi mbalimbali za kuhudumu serikalini n.k.
Inabidi wadai kunufaika ipasavyo na matunda ya uhuru (walioupigania sana wakati ule wa kudai uhuru) ikiwemo ajira, na utumishi wa ndani ya serikali
Vipi kuhusu wakristo wa zanzbar na dini nyingine kaka???
 
Naona kisa kupewa huyo Mzanzibari Uenyekiti wa bodi ndio umekosa raha...

Nyie viumbe mna matatizo sana, wakati wa Magufuli mlikuwa mnalalamika anapendelea wakristo wenzake, leo amekuja mwenzenu bado mnaendelea kulalamika anapendelea kule atokako hata kama anawateua waislamu wenzenu..

Sikutegemea kwa namna mnavyobebwa huku bara kwenye teuzi siku hizi, bado mtazitolea macho nafasi za Zanzibar ikiwa bado wanapewa waislamu wenzenu, huu ubinafsi sijawahi kuuona hapa duniani, nyie iko siku mtatafunana..
Hawa watu sampuli ya mleta uzi huu ni hatari sana na mawazo kama haya yakikomaa yanazaa element ya ugaidi. Kila wakati mtu anawaza udini tu utafikiri hiyo dini ndiyo inampatia mkate wake wa siku.
 
Hii mada iko objective. Utapotea sana ukiijadili kwa hisia, udini au ushabiki.

Hii mada siyo ya kidini ndiyo maana Inahoji namna gani waislamu wa upande mmoja wanufaike zaidi kuliko wa upande mwingine licha ya wote kuwa dini moja.

Kwa hiyo weka hisia pembeni, njoo tujadili hili suala la kijamii tukiwa open minded!
!!!Zungumzia na wakristo wa zanzbar pia kama mada yako ipo objective
 
Hii mada iko objective. Utapotea sana ukiijadili kwa hisia, udini au ushabiki.

Hii mada siyo ya kidini ndiyo maana Inahoji namna gani waislamu wa upande mmoja wanufaike zaidi kuliko wa upande mwingine licha ya wote kuwa dini moja.

Kwa hiyo weka hisia pembeni, njoo tujadili hili suala la kijamii tukiwa open minded!
Listen, kama ungekuwa na nia njema ungelizungumzia hili suala kwa ujumla wake, kwasababu kiuhalisia, sio waislamu wa Bara pekee wanaokosa teuzi Zanzibar.

Hata wakristo na makundi mengine nao wana tatizo hilo, tena kwangu ni kubwa zaidi na limekuwepo kwa muda mrefu zaidi ya hili tatizo lako uliloleta hapa.

Lakini kuamua kwako kutowazungumzia hawa kwa ujumla wao, badala yake ukajikita kulizungumzia kundi specific ulilo na interest nalo, kumeonesha nia yako na dhamira yako ya upendeleo, hii ni dalili kwamba...

Kwako kama hao waislamu wa Bara wangepata teuzi unazotaka Zanzibar, ungefunga mdomo wako usiyazungumzie makundi mengine, kwasababu unaamini shida yako ingekuwa imemalizwa...

Ndio maana umemjibu mdau aliyekuuliza kuhusu makundi mengine pale juu kwamba aanzishe uzi wake kuzungumzia tatizo lake, wakati kimsingi tatizo lake ndio tatizo lako pia, ila ubinafsi umekufunga akili hulioni hilo.
 
Listen, kama ungekuwa na nia njema ungelizungumzia hili suala kwa ujumla wake, kwasababu kiuhalisia, sio waislamu wa Bara pekee wanaokosa teuzi Zanzibar.

Hata wakristo na makundi mengine nao wana tatizo hilo, tena kwangu ni kubwa zaidi na limekuwepo kwa muda mrefu zaidi ya hili tatizo lako uliloleta hapa.

Lakini kuamua kwako kutowazungumzia hawa kwa ujumla wao, badala yake ukajikita kulizungumzia kundi specific ulilo na interest nalo, kumeonesha nia yako na dhamira yako ya upendeleo, hii ni dalili kwamba.

Kwako kama hao waislamu wa Bara wangepata teuzi unazotaka Zanzibar, ungefunga mdomo wako usiyazungumzie makundi mengine, ndio maana umemjibu mdau hapo juu aanzishe uzi wake kuzungumzia tatizo lake, wakati kimsingi tatizo lake ndio lako pia, ila ubinafsi umekufunga akili huoni hilo.
Mada inajitosheleza. Kama unadhani una mawazo bora zaidi na wewe fungua ya kwako.
 
Naona kisa kupewa huyo Mzanzibari Uenyekiti wa bodi ndio umekosa raha...

Nyie viumbe mna matatizo sana, wakati wa Magufuli mlikuwa mnalalamika anapendelea wakristo wenzake, leo amekuja mwenzenu bado mnaendelea kulalamika anapendelea kule atokako hata kama anawateua waislamu wenzenu..

Sikutegemea kwa namna mnavyobebwa huku bara kwenye teuzi siku hizi, bado mtazitolea macho nafasi za Zanzibar ikiwa bado wanapewa waislamu wenzenu, huu ubinafsi sijawahi kuuona hapa duniani, nyie iko siku mtatafunana..
Naona chawa wa Mbowe linapokuja swala la dini huwa mnatofautiana sana aisee. Yani kila mtu anaangalia dini yake badala ya taifa lake 😂😂😂
 
Back
Top Bottom