Karibu Prof. Mama Anna Tibaijuka ndani ya JamiiForums!

Status
Not open for further replies.
Ila chonde chonde utawala wa JF, hatimae serikali isije ikanunua mtandao wetu, wengine ukombozi wetu upo huku.........huku tunalalamika, huku tunaponda, huku tunalia, huku tunapata hasira, huku tunapeana maisha, huku tunaelimishana, huku tunarubuniana, huku tunasengenyana, huku tunakasirika, huku tunafurahi, huku tunataniana, huku tunachukiana, huku tunapendana, huku tunaoneana, huku tunadhulumiana, huku tunatapeliana, huku tunaambiana ukweli, huku tunaambiana uongo, huku tunaisema serikali vibaya, huku tunaisema serikali vizuri, nk nk nk nk nk; huku JF sisi ni kila kitu kwenye maisha yetu ya kila siku......so plz serikali njoo kwa wingi lakini kuka kauli mbiu moja """where we dare to talk openly"""

Karibu sana mama Anna Tibaijuka, na hongereni utawala wa JF na members wake kwa kufanya JF iendelee kukubalika kila siku!!!!!

VUNJA BEI.
 
Last edited by a moderator:
Mama karibu lakini ukae ukijua umu tuna maswali magumu haswaaaaaa....kwa kuanzia hivi mbona upimaji wa viwanja umeishinda kabisa wizara yako.
 
Karibu mama, ila huku inabidi uwe na roho ya uvumilivu. Kuna comments nyingine zitakuumiza, nyingine zitakusifia, yote pokea kwa ajili ya kujiongezea ubora wa kazi, kubali kubadilika kupitia JF.

Karibu
 
Hongera mama Tibaijuka,
hivi inakuwaje kama angekuta jina lake linatumiwa na mtu mwengine?
CoPY: AshaDii
Swali lako ni la msingi. Mara zote watu wanapojisajiri kwa kutumia majina ambayo ni public figures, uongozi wa JF huyaweka kwenye zuio mpaka baada ya kuthibitisha kuwa anayefahamika zaidi kwa umma kwa kupitia jina husika ndiye kweli amefanya usajiri.

Hapo siku za nyuma alipata kujiandikisha mtu siku ya jumapili mida ya ibada kwa jina la E. Lowassa na kuanzisha uzi wenye malengo maalumu aliyotaka kukidhi. Baada ya Uongozi wa JF kufuatilia ikabainika kuwa Mh. E. Lowassa alikuwa kanisani muda ule.

Daima tunajitahidi kwa kila jinsi kuhakikisha majina ya watu hayatumiki kihalifu au vibaya ndani ya JF
 
Swali lako ni la msingi. Mara zote watu wanapojisajiri kwa kutumia majina ambayo ni public figures, uongozi wa JF huyaweka kwenye zuio mpaka baada ya kuthibitisha kuwa anayefahamika zaidi kwa umma kwa kupitia jina husika ndiye kweli amefanya usajiri.

Hapo siku za nyuma alipata kujiandikisha mtu siku ya jumapili mida ya ibada kwa jina la E. Lowassa na kuanzisha uzi wenye malengo maalumu aliyotaka kukidhi. Baada ya Uongozi wa JF kufuatilia ikabainika kuwa Mh. E. Lowassa alikuwa kanisani muda ule.

Daima tunajitahidi kwa kila jinsi kuhakikisha majina ya watu hayatumiki kihalifu au vibaya ndani ya JF

Ahsante kwa majibu yako mazuri yaliyojitosheleza.
 
Wana JF,

Nitumie fursa hii kumpongeza Prof. Anna Tibaijuka kwa maamuzi yake sahihi ya kujiunga na JF. Sote tunajua kuwa sio jambo rahisi kwa kiongozi katika nafasi yake. Anaongoza wizara nyeti yenye maswali mengi hivyo yataka moyo mtu kujitosa kwenye mtandao wenye maswali ya kila aina kama Jamii Forums.

Uongozi wa JF hongereni pia kwa kutuletea mwana mama huyu shupavu ambaye ameipaisha bendera ya nchi yetu katika mizania ya kimataifa.

Ombi langu kwa wanaJF and Mods, tutambue nia njema ya Prof. Anna Tibaijuka, na baadhi ya viongozi waandamizi waliokwisha jiunga na watakao jiunga baadae. Tujadiliane nao katika yale yanayohusu kazi zao bila kuingiza mambo ya kibinafsi au kuwavunjia heshima. Hivi ndivyo tutawapata wengi kujiunga kama Verified Users.

Pia tutambue majukumu ya Prof. Anna Tibaijuka hivyo mjadala wa moja kwa moja kwa njia ya maswali na majibu unaweza kumuwia mgumu kwa maana ya muda; na badala yake tunaweza tumia njia ya kukusanya maswali mbalimbali na kumtumia ili atafute muda wa kuyajibu kwa pamoja. Tuitumie hii fursa ya uwepo wake vizuri, naamini atatenda kwani ni mtu anayejiamini na ni mtendaji.

Kwa mara nyingine, karibu sana Prof. Anna Tibaijuka!
 
Wengi wamekukaribisha, lakini hawakusema furaha yao ni kitu gani?

Nakukaribisha na swali: Wizara yako inalalamikiwa sana kwa rushwa ambayo inasababisha wanyonge kudhulumiwa ardhi zao, Ukiwa kama Top, analionaje tatizo hili na unalishughulikia vipi?
 
Karibu sana Mama yetu kwenye jukwaa la wananchi wote.

Umeonyesha mfano wa kuigwa na Mawaziri wengine ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

Kwa lugha ya ki-Bariadi Bariadi tunapaita HAGAGIKOME!.

Obeja Mayu.
 
Baada ya kuiponda JF, naona jamaa wameanza kuziingiza 'silaha zao za Urais' JF.

Inabidi atueleze nini kilitokea 'Gigiri Complex' mpaka akanyang'anywa wadhifa wenye ushawishi mkubwa wa Mkurugenzi Mkuu wa 'UN Office at Nairobi (UNON)' na kubakia na wadhifa wa Mkurugenzi Mtendaji wa HABITAT.

Pia atueleze amewasaidia Watanzania wangapi kupata kazi nje ya nchi kwenye mashirika ya UN.
 
Karibu jamvini Mh. waziri. Washauri wenzio hasa Wassira, Lukuvi nao waje. Wajue kuwa hiki siyo kijiwe cha wahuni, ni ukumbi huru kwa watu wenye mawazo huru.

Tunategemea umshauri na mkuu pale magogoni naye aingie kwa jina lake halisi!
 
Karibu ukumbini Mhe Prof. Anna Tibaijuka. Kwa kuwa mimi huwa naingia mara moja moja JF, Kabla sijapotea naomba nikuulize swali, kwanini hadi leo hujamboa ghorofa la Mch. Mhe. Gertrude Rwakatale pamoja na kujenga sehemu ambayo imekatazwa na NEMC na mbaya zaidi ulivyo na double standard ukabomoe nyumba za walalahoi wengine huku ukiliachaa jumba Mch Rwakatale.

FYI, hizi double standards za CCM ndiyo zinafanya Watanzania wengi tuichukie CCM na kuipenda CDM. Mchawi wa CCM ni CCM yenyewe na wala sio CDM. Kupambana na CDM ili kuiidhoofisha ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. CCM inabidi ijiangalie yenyewe ni wapi ilipoangukia.
 
Na Wassira aje basi jamvini kuna watu wana majibu ya maswari yetu but all in all well come prof mama Tibaijuk.
ushauri uwe unatembelea mara kwa mara jamvini
 
Mama, Prof. Tiba, karibu sana!! Tungekuwa na viongozi wanaojiamni na kujua wanafanya nini kama huyu mama tungefika mbali Anakwmishwa tu na mfumo. Ningefurahi kama Mwakyembe, Magufuli, na wengineo wangejiunga humu maana nyakati nyingine hawa viongozi wetu hawaonekani kirahisi. Issues nyingi za msingi zaishia kwa wasaidizi wao na hivyo kuchelewesha maamuzi ya mambo ya msingi katika kuijenga nchi yetu.
 
Karibu jamvini Mh. waziri. Washauri wenzio hasa Wassira, Lukuvi nao waje. Wajue kuwa hiki siyo kijiwe cha wahuni, ni ukumbi huru kwa watu wenye mawazo huru. Cha muhimu, muwe mnakuja kutoa majibu hasa pale mnapohitajika maana ni jukwaa pekee mnalokaa na watu tofauti bila urasimu.
Tunategemea umshauri na mkuu pale magogoni naye aingie kwa jina lake halisi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom