Karibu mwezi mtukufu wa Ramadhani

Karibu mwezi mtukufu wa Ramadhani

Barubaru

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2009
Posts
7,161
Reaction score
2,329
Hakika zimesalia siku chache sana kabla waumin wa Kiislamu hawajaanza kufunga mwezi katika mwezi mtukufu wa ramadhwani. kama ilivyobainisha katika Qur'An

((Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa Swawm, kama waliyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah))(([Mfunge] siku maalumu za kuhisabika. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakayefanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua)) ((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini katika mwezi huu na afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Allaah Anakutakieni yaliyo mepesi wala Hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Allaah kwa kuwa Amekuongoeni ili mpate kushukuru)) [Al-Baqarah: 183-185]

Nawatakia waumini wote ramadhan mubarak
 
Point of correction: huku si kufunga ni kubadili ratiba ya kula (angalia kwa nini bei za vyakula hupanda mwezi huu, ni kwa kuwa ulaji umezidi)! Pia Qur'an haikushushwa yote (kama ilishushwa anyway) mwezi wa Ramadhan, otherwise Q2:185 inajipinga na Q17:106, 25:32. Hata hivyo, nawatakia waislamu wote mabadiliko mema ya ratiba za kula!
 
Na iwe Ramadhan yenye kufikia lengo ambalo ni uchamungu.

Tujihesabu je, ramadhan iliyopita ilitubadilisha nini ktk imani zetu na maisha yetu ya kila siku, jamii yetu tunayoishi nayo je ilifaidika nini na funga yetu??? Tukifikia hili lengo la uchamungu bila shaka tutakuwa na maisha yaliyojaa UPENDO, AMANI, USTAARABU/MAADILI NA KERO ZOTE TUNAZO ZIPIGIA KELELE KILA SIKU HAPA JF ZITAKWISHA (A.K.A RUSHWA/UFISADI)

Karibu as-shahar swiyaam
 
Kule nyumbani Afrika Mashariki, Ramadhani itakuwa Jumamosi tarehe 22 August 2009, na kwa wale wa Ansar Sunna, wajiandae kufunga kuanzia Ijumaa tarehe 21 August.

Moonsighting for Ramadan 1430

The Astronomical New Moon is on August 20, 2009 (Thursday) at 10:01 UT. This moon can not be seen in any continent. There is a small chance to see only in Polynesian Islands on August 20. On August 21, it is very difficult to see in Europe and Canada. It can be seen with difficulty in India, Pakistan, Middle East, and Northern Africa. On August 21, it can be easily seen in Australia, most Africa, and Americas.

SOURCE: Moonsighting.com
 
Point of correction: huku si kufunga ni kubadili ratiba ya kula (angalia kwa nini bei za vyakula hupanda mwezi huu, ni kwa kuwa ulaji umezidi)! Pia Qur'an haikushushwa yote (kama ilishushwa anyway) mwezi wa Ramadhan, otherwise Q2:185 inajipinga na Q17:106, 25:32. Hata hivyo, nawatakia waislamu wote mabadiliko mema ya ratiba za kula!

BUCHANAN,

Usikurupuke kuandika mambo bila kuyajua . Soma vizuri Aya hiyo nilioweka kwenye bandiko langu Qur'An 2:183 mpaka 185 ( Al-Baqarah: 183-185)
((Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa Swawm, kama waliyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah))(([Mfunge] siku maalumu za kuhisabika. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakayefanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua)) ((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini katika mwezi huu na afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Allaah Anakutakieni yaliyo mepesi wala Hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Allaah kwa kuwa Amekuongoeni ili mpate kushukuru)) [Al-Baqarah: 183-185]

Acha kudandia treni kwa mbele.

Mola akubariki, kwani ipo siku ukweli utadhihiri.

Ramadhani Kareem
 
BUCHANAN,
Sio bei ya vyakula hupanda bali ni bei ya futari inapanda. Hiyo yote ni kuonyesha utukufu wa mwezi huu na waislamu pamoja na fedha walizonazo, vyeo walivyonavyo, nafasi walizonazo wana acha yoooote hato na kukaa na njaa (kufunga) tokea jua linapochomoza mpaka linapozama. hii yote ni utukufu wa mwezi.

na wanapofungua basi wanatumia mali zao kuwalisha masikini ikiwa pamoja na kukaribishana.

Mimi mwenyewe nachukua nafasi hii kukukaribisha futari JAPO WEWE MKATOLIKI hustahiki kufunga.
 
Hakika zimesalia siku chache sana kabla waumin wa Kiislamu hawajaanza kufunga mwezi katika mwezi mtukufu wa ramadhwani. kama ilivyobainisha katika Qur'An

Nawatakia waumini wote ramadhan mubarak

Ninawatakia ndugu zetu waislamu wa Tanzania heri na baraka tele wanapoingia katika Mfungo mtukufu wa Ramadhani.!
 
ninawatakia ndugu zetu waislamu wa tanzania heri na baraka tele wanapoingia katika mfungo mtukufu wa ramadhani.!
__________________

mwanakijiji.
hakika mfungo huu ni kwa waislamu woooote wa madhehebu yote duniyani kote.

nawatakia waislamu wote ramadhani kareem
 
Mfungo mwema. Matendo mema ambayo mumeambiwa muyatende yaendelee hata baada ya mfungo wa Ramadhani.
 
Nawatakia kila jema ndugu zangu ambao mnajiandaa kwa mfungo.Pamoja sana!
 
Hakika zimesalia siku chache sana kabla waumin wa Kiislamu hawajaanza kufunga mwezi katika mwezi mtukufu wa ramadhwani. kama ilivyobainisha katika Qur'An

Nawatakia waumini wote ramadhan mubarak

Enyi mlioamini na waislamu wote, nakutakieni saumu yenye kukubaliwa!! Lakini mfungo ukiisha inshallah usisahau kutualika IDD EL FITR. Ramadhani Mubarak!
 
saumu njema waungwana, lakini mema yasiishie wakati wa mfungo tu
 
Wafuasi wa allah, nawatakia mfungo mwema.

Remember Jesus is coming soon
 
Ninawatakia ndugu zetu waislamu wa Tanzania heri na baraka tele wanapoingia katika Mfungo mtukufu wa Ramadhani.!

Ni bora mfungo uje mapema kabla hatujarudi Bungeni November maana hapo hatutacheka na Kima yoyote mpk Uchaguzi

Ramadhan Kareem
 
BUCHANAN,

Usikurupuke kuandika mambo bila kuyajua . Soma vizuri Aya hiyo nilioweka kwenye bandiko langu Qur'An 2:183 mpaka 185 ( Al-Baqarah: 183-185)

Acha kudandia treni kwa mbele.

Mola akubariki, kwani ipo siku ukweli utadhihiri.

Ramadhani Kareem

Ok, nakutakia ratiba njema!
 
Na iwe Ramadhan yenye kufikia lengo ambalo ni uchamungu.

Tujihesabu je, ramadhan iliyopita ilitubadilisha nini ktk imani zetu na maisha yetu ya kila siku, jamii yetu tunayoishi nayo je ilifaidika nini na funga yetu??? Tukifikia hili lengo la uchamungu bila shaka tutakuwa na maisha yaliyojaa UPENDO, AMANI, USTAARABU/MAADILI NA KERO ZOTE TUNAZO ZIPIGIA KELELE KILA SIKU HAPA JF ZITAKWISHA (A.K.A RUSHWA/UFISADI)

Karibu as-shahar swiyaam

Haya ni maneno ya hekima ambayo ningemshauri GT ayasome between the lines ili baada ya mfungo mwa mwezi mtukufu arudi hapa janvini akiwa na hoja zenye kujenga amani na mshikamano wa wadanganyika irrespective of their religious affiliation!!
 
Na iwe Ramadhan yenye kufikia lengo ambalo ni uchamungu.

Tujihesabu je, ramadhan iliyopita ilitubadilisha nini ktk imani zetu na maisha yetu ya kila siku, jamii yetu tunayoishi nayo je ilifaidika nini na funga yetu??? Tukifikia hili lengo la uchamungu bila shaka tutakuwa na maisha yaliyojaa UPENDO, AMANI, USTAARABU/MAADILI NA KERO ZOTE TUNAZO ZIPIGIA KELELE KILA SIKU HAPA JF ZITAKWISHA (A.K.A RUSHWA/UFISADI)

Karibu as-shahar swiyaam

Haya ni maneno ya hekima ambayo ningemshauri GT ayasome between the lines ili yamsaidie katika mfungo huu wa mwezi mtukufu; naamini akisha kuisoma na kuielewa nukuu hii atarudi janvini baada ya IDD na kuchangia hoja zitakazoendeleza upendo kati ya madhehebu mbalimbali. Nawatakieni wote mfungo uliojaa kheri na amani.
 
Back
Top Bottom