menikumbusha Miaka ya mwanzo ya themanini nikiishi Sumbawanga, kuna mzee mmoja alikuwa akilinda nyumba ya mkuu wa mkoa wakati huo ikijengwa, basi katika cheza cheza yetu na sababu tulikuwa tunaishi jirani pale Regional Block tulikuwa tunaingia mle ndani tunamkuta babu wa kinyaki ndo mlinzi pale, jioni hiyo babu kishajikoki na SUTE (pombe ya kienyeji) anatupa story za Tukuyu yeye alikuwa hana meno ya mbele so Tukuyu yeye anatamka TUKUJU, alipenda sana kusema wanangu Tujuku Bulaya wanangu bulaya kabsaaa yaani Tukuyu ulaya wanangu uklaya kabsaaa!