Karibu ktk sherehe za kuzaliwa CCM-Mwanza

Karibu ktk sherehe za kuzaliwa CCM-Mwanza

Kweli nimeamini hawa ccm ni vipofu, viziwi, na akili imechanganyika na ulevi tena wa pombe ya kienyeji. Chama kinaelekea kufa badala wakae chini watafakari namna ya kujipanga upya, wao wanafanya sherehe! Wanazidi kukimaliza chama! Au ndio wameamua kukimalizia kife kabisa!?
Juzi wamefanya sherehe za uhuru wa Tanganyika kwa karibu 50bil, kesho watatuambia sherehe za ccm zimegharimu sijui bilion ngapi! Wao ni kutumia hela kwa anasa tu, hakuna kufanya maendeleo!

Wakazi wa Mwz neema inakuja! Mtapewa tshirt, kofia,kanga, ubwabwa,usafiri na hela ili muende mkutanoni. Msiviache. Chukueni vyote. Tshirt mwende nazo shambani, kanga mwende nazo ngomani, hela mkajazie ada, pombe na pilau mle na kunya msahau kidogo shida zetu. Wakimaliza sherehe muwaage halafu maisha yanaendelea!
 
Miji na majiji yote yamechukuliwa labda waende mji wa Igunga.

Acha kukurupuka toka usingizi wa pono!

Miji ya Songea, Mtwara, Morogoro,Tanga, Babati,Singida, Shinyanga, Tabora, Bukoba, Dodoma, Sumbawanga, Njombe, Ifakara, kote CCM inatamba
 
WanaJF,tuna furaha ya kukualikeni kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi kitaifa jijini Mwanza,tuna sababu nyingi za kuifanya sherehe hii hapa:
1.Kuwashukuru wananchi wa kanda ya Ziwa kwa kura walizotupigia ingawa hazikutosha.
2.Kuimarisha chama upya,kuleta mvuto mpya kwa wananchi na wanachama wa CCM kwa kanda ya Ziwa.
3.Kuwaeleza Watanzania namna tunavyoongozwa na mtu makini kabisa.
4.Kushirikiana na wanachama kuhakikisha 2015 majimbo yote 3(ILEMELA,NYAMAGANA,UKEREWE)yaliyotwaliwa na CHADEMA yanarudi CCM.
5.Kufufua na kuimarisha upya ngome yetu ya CCM ya kanda ya Ziwa.Ni mengi mno,kwa ufupi nawasilisha.
Kidumu CHAMA CHA MAPINDUZI
Unatuona feki ee...! Hatudanganyiki ng'o!... Kawadanganye waliolala huko Igunga!
 
If i recall properly! mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa mwanza alikuwa ni mfanyabiashara za magendo ya bia kutoka kenya in 80s via lake victoria shores. kweli CCM ni Chama Cha Majambazi!
 
ungechukua hizo pesa za sherehe na kuzitumia kujazia madawa mahosptalini na madawati mashuleni watanzania wangewashukuru kuliko kupoteza pesa kufanya sherehe wakati wanakufa mahospitalini kwa kukosa madawa.
 
Acha kukurupuka toka usingizi wa pono!

Miji ya Songea, Mtwara, Morogoro,Tanga, Babati,Singida, Shinyanga, Tabora, Bukoba, Dodoma, Sumbawanga, Njombe, Ifakara, kote CCM inatamba
tatizo wizi tu nao wangefanya kama walivyo fanya Mbeya, Arusha, Mwanza etc leo usingekua na kauli hii
 
WanaJF,tuna furaha ya kukualikeni kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi kitaifa jijini Mwanza,tuna sababu nyingi za kuifanya sherehe hii hapa:
1.Kuwashukuru wananchi wa kanda ya Ziwa kwa kura walizotupigia ingawa hazikutosha.
2.Kuimarisha chama upya,kuleta mvuto mpya kwa wananchi na wanachama wa CCM kwa kanda ya Ziwa.
3.Kuwaeleza Watanzania namna tunavyoongozwa na mtu makini kabisa.
4.Kushirikiana na wanachama kuhakikisha 2015 majimbo yote 3(ILEMELA,NYAMAGANA,UKEREWE)yaliyotwaliwa na CHADEMA yanarudi CCM.
5.Kufufua na kuimarisha upya ngome yetu ya CCM ya kanda ya Ziwa.Ni mengi mno,kwa ufupi nawasilisha.
Kidumu CHAMA CHA MAPINDUZI

Nimetembelea Mwanza juzi , yaani mpaka hivi sasa wabunge wa CDM hawajafanya lolote aisee porojo kibao na fedha za kutekeleza ahadi hawana. Wana Mwanza wameingia choo cha kike safari hii aiseeeee

 
Nawasalimuni wanajf.

Nimesikia redioni, magazeti na baadhi ya TV juu ya maandalizi ya kusherehekea miaka 35 ya uwepo wa CCM yatakayoadhimishwa mjini Mwanza.

Miaka 35 ni kipindi kirefu na cha kutosha kuweza kufanya kitu kikasimama na kuonekana na nadhani wengi mtakubaliana nami katika wazo na mtazamo huo.

Hoja yangu hapa ni kutaka kushirikiana nanyi ili kujua ni kitu gani katika miaka hii 35, CCM kama chama wamekifanya na kukifanikisha na hivyo tunaweza tukajivunia kama wanachama wake na wale wasio wanachama ukichukulia kuwa sote ni Watanzania.

Binafsi nimeangalia maeneo kama 50 nchi nzima na inaelekea wameshindwa kwa zaidi ya 80% kufanya walichokusudia aidha bila kujua au kwa makusudi. Hii inadhiirisha mipango mingi waliyonayo huwa ni ya 'zima moto' na likishapita la kupita wanaachana nayo.

Hii ni baadhi ya miradi ya CCM isiyoeleweka na wewe unaweza ukaongezea kadiri unavyoelewa kulingana na eneo ulilopo:
1. Mradi wa SUKITA. Huwezi amini majengo yaliyogharimu pesa nyingi yapo kama magofu na hayakuwa hata kutumika.
2. Uwanja wa Alhaji Ali Hassani Mwinyi, Tabora. Hapa wananchi wote walichangia lakini ukiuangalia leo kama utatoa machozi.
3. .....
4. .....
Na endapo kuna mradi waliofanikiwa (mfano kama ujenzi wa Jengo la Vijana - Makao Makuu) unaweza kuuweka hapa tukaujua.

Nawasilisha
 
Popote mlipo wanaJF,Salaam kwenu,Niko hapa jijini MZA kwa siku kadhaa sasa.Maandalizi ya sherehe za kuzaliwa CCM yanaendelea,bendi za kutumbuiza siku hiyo zinafanya mazoezi ya nguvu,tayari mabasi kadhaa yameanza kuandaliwa kwa kusomba watu kutoka Magu,Sengerema,Usagara,Nyanguge,Kabangaja,Misasi,Hungumalwa,Fukaro,Nyanshimo,Sumve na kwingineko.Gari zinapita usiku kuhamasisha wananchi,kwamba wao ni chama cha zamani,wasapoti yote wanayoyafanya,picha mbioni kuweka.Nawasilisha.
 
Wapeleke bendi ambazo hazina market hapa mujini, Ngwasuma letu na Twanga watuachie kwa raha zetu, unadhani hapa mujini TOT plus ni nani atatoa pesa yake kwenda kuona show yao!!??
 
aiseeeeeeeeeee, endeleeni kusomba watu..........
 
Wananchi wanakufa mahospitalini watu wengine wanaendekeza ujinga,wamekataa kuwasikiliza madaktari,wazuieni hao,wekeni magogo,mawe makubwa hayo njiani wakipita wamwagieni michanga wapuuzi kweli CCM hali ya nchi ilivyotete kunasikukuu kweli
 
Wananchi wanakufa mahospitalini watu wengine wanaendekeza ujinga,wamekataa kuwasikiliza

madaktari,wazuieni hao,wekeni magogo,mawe makubwa hayo njiani wakipita wamwagieni michanga wapuuzi kweli CCM hali ya nchi

ilivyotete kunasikukuu kweli

Kabisa,ngoja tujipange.
 
Popote mlipo wanaJF,Salaam kwenu,Niko hapa jijini MZA kwa siku kadhaa sasa.Maandalizi ya sherehe za kuzaliwa CCM yanaendelea,bendi za kutumbuiza siku hiyo zinafanya mazoezi ya nguvu,tayari mabasi kadhaa yameanza kuandaliwa kwa kusomba watu kutoka Magu,Sengerema,Usagara,Nyanguge,Kabangaja,Misasi,Hungumalwa,Fukaro,Nyanshimo,Sumve na kwingineko.Gari zinapita usiku kuhamasisha wananchi,kwamba wao ni chama cha zamani,wasapoti yote wanayoyafanya,picha mbioni kuweka.Nawasilisha.
...mkuu uko Mwanza ya wapi?,Tanzania au Zambiya?,mimi niko hapa Mwanza Tanzania maeneo ya kirumba hakuna chote cha maana zaidi ya uchulo...
 
Waambie wachonge na majeneza yao kabisa na pia waandae sanda.
 
...mkuu uko Mwanza ya wapi?,Tanzania au Zambiya?,mimi niko hapa Mwanza Tanzania maeneo ya kirumba hakuna chote cha maana zaidi ya uchulo...

Endelea kula dagaa Mwaloni,ziko bendi hapa zinapiga nyimbo za kejeli.Ratiba ipo,inawezekana una habari za mlangoni,sibahatishi,magari yapo,na amin nakuambia,basi zipo,wale wa kubebwa bado wapo.Unaumia nini?Si chama chetu bwana,si mchungaji hula kondoo wake?B'dae
 
CCM navyokupenda nitakunywa sumu juu yako.Naapa naahidi mbele ya Chama Mapinduzi nitakulinda mpaka kufa,enzi zile za shule ya msingi
 
wakati utaamua, leo wanasomba watu kwa mabasi kesho watafanya nini? wakati utaamua
 
Back
Top Bottom