Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 780
- 1,831
Jarida hili litakuelimisha na kukupatia taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya uchumi na sekta ya fedha nchini, hususani yale yanayoratibiwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania kwa mujibu wa sheria. Katika toleo hili, utapata taarifa kwa kina kuhusu shughuli na majukumu ya Benki Kuu Ya Tanzania (BOT) katika kuratibu na kusimamia sekta ya fedha na uchumi wa nchi kiujumla.
Miongoni mwa habari tulizokuandalia katika jarida hili ni pamoja na Gavana wa Benki Kuu awataka wafanyakazi wa sekta ya fedha nchini kuwa wazalendo na kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu. Vilevile utaelimishwa kwa kina namna mifumo ya malipo ya Taifa inavyowezesha ulipaji malipo mbalimbali kwa ufanisi mkubwa.
Kwa kushirikiana na wadau wetu mbalimbali, utapata fursa ya kupata habari na taarifa kutoka kwa taasisi za fedha nchini ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Mitaji na Dhamana nchini (CMSA), Bodi ya Bima ya Amana nchini (DIB), Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Katika kujenga ushirikiano na jamii inayotuzunguka, Benki Kuu hutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza kutoa elimu kwa Umma kuhusu majukumu inayotekeleza, kupokea maoni na ushauri mbalimbali toka kwa wadau wetu kwa minajili ya kuzidi kuboresha zaidi huduma zetu.
Ni matumani yangu kuwa, kupitia jarida hili utapata fursa ya kuielewa sekta ya Uchumi na Fedha kupitia makala, vibonzo, habari picha na mashairi yaliyomo katika Jarida letu Uchumi wetu Toleo la 3.
Endapo una maoni, ushauri au mapendekezo yoyote, tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe: botcommunications@bot.go.tz
Nakutakia usomaji mwema.
Victoria Msina Meneja, Idara ya Mawasiliano