Karibu Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karibu Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mbilimbi Mbovu, Jun 22, 2011.

 1. Mbilimbi Mbovu

  Mbilimbi Mbovu Senior Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: May 25, 2015
  Messages: 185
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Historia ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine inaanza mwana 1965, ambapo kilianzishwa kikiwa Chuo cha Kilimo kilichokuwa kinatoa mafunzo ya kilimo kwa ngazi ya diploma.

  [​IMG]

  Kufuatia kuvunjika kwa kilichokuwa Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki na kuanzishwa rasmi kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1970, chuo hiki kilibadilishwa na kuwa Kitivo cha kilimo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuanza kutoa Shahada ya Sayansi katika Kilimo.

  Mwaka 1974, Kitengo cha Misitu kilianzishwa na hivyo taasisi nzima ikanbadilishwa jina na kuitwa Kitivo cha Kilimo na Misitu. Kufuatia kuanzishwa kwa Shahada ya Sayansi za Tiba ya Mifugo mwaka 1976 pamoja na kuanzishwa kwa kitengo cha Utabibu wa Migugo, jina la taasisi likabadilishwa tena na kuwa Kitivo cha Kilimo, Misitu na Sayansi za Tiba ya Mifugo.

  Julai 1 1984, kitivo kilibadilishwa kwa Sheria ya Bunge Na.6 ya mwaka 1984 na kuwa Chuo Kikuu Kamili na kupewa jina la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, kikiwa na vitivo vitatu; Kilimo, Misitu na SayansiTiba za Mifugo.

  Hadi sasa, chuo kina vitivo vinne; Kitivo cha Kilimo, Kitivo cha Misitu na Uhifadhi, Kitivo cha Sayansitiba za Mifugo na Kitivo cha Sayansi.

  [​IMG]


  Kwa sasa chuo kina kampasi nne; Kampasi Kuu iliyopo Manispaa ya Morogoro, Kampasi ya Solomon Mahlangu iliyopo Mazimbu, Morogoro, Msitu wa Mafunzo Omolonyi, uliopo Arusha na Pori la Akiba la Mazumbai lililopo Manispaa ya Tanga.

  Kwa sasa chuo kinatoa kozi 30 za shahada ya kwanza na kozi 45 za uzamivu.

  Kampasi kuu ipo Manispaa ya Morogoro, mwendo mfupi kutoka Stendi Kuu ya Msamvu.

  [​IMG]

  ========================================
  ========================================


  Soma: Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine
   

  Attached Files:

  • sua.png
   sua.png
   File size:
   1.3 MB
   Views:
   1,471
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kama kigezo cha umaarufu ingekuwa umri, kwa nini unataka SUA iwe maarufu kama UDSM wakati chuo hicho ni mama yake?

  Ukiacha umri, kuna vigezo kadhaa vinavyotumika kimataifa kulinganisha vyuo. Hujadokezo vigezo ulivyovitumia kuonyesha kwamba SUA iko chini ya vyuo ulivyovitaja.
   
 3. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Nafikiri hujafanya utafiti wowote kuhusu SUA ila umeamua tu kuandika bila ya kuwa na vigezo vyovyote, kwa muda wa miaka mingi sasa kila inapotolewa rank ya vyuo vikuu africa UDSM huwa inaongoza na SUA huwa inafuatia.

  Hivyo vyuo unavyovija wewe huwa havionekani kabisa kwenye rank ya vyuo vikuu africa.
   
 4. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,231
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Senetor sina hakika kama unaperuzi takwimu na rank mbali mbali ya academic institutions duniani...

  kwa kukusaidia tu Unapozungumzia kwenye jukwaa la kimataifa kuhusu vyuo na taasisi za elimu Tanzania utaanza na chuo kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Chuo cha kilimo cha Sokoine...

  na ukifunua zaidi utagundua kwamba kwa Afrika SUA imesimama sana linapokuja suala la vyou vya kilimo... Fanya utafiti kabla hujaconclude jambo!
   
 5. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,455
  Likes Received: 2,040
  Trophy Points: 280
  Nakifahamu vizuri chuo cha Sokoine na ninaweza kufafanua kwa nn mtoa hoja ana wasiwasi na popularity ya hiki chuo midomoni mwa watu.

  Kwa ufupi ni kwamba Sokoine ni chuo kikuu cha kilimo na masomo ya Kilimo yana nature ya science ambayo yanaogopwa na watu wengi sana nchini.

  Umaarufu wa chuo hiki ni mkubwa sana kitaaluma kwani kina idadi kubwa sana ya maprofesa na madokta ukifananisha na chuo kama Mzumbe na pia kuna researcher wazuri sana pale SUA waliobobea haswa kwenye tafiti za kisayansi Pia walimu wengi wa Mzumbe kwa sasa wanasoma PhD SUA na UDSM kwa hiyo ukiangalia vizuri utagundua kuwa SUA inategemewa sana hata kutoa elimu kwa taasisi nyingine.

  Vyuo kama Mzumbe, IFM n.k vinasikika sana kwa kuwa watu wengi ambao ni waoga wa masomo ya science wanakimbilia kule hasa wanawake hivyo utakuta kwa mtu mvivu wa kufikiri anaweza kuona ni vyuo maarufu kwa kuwa kuna watoto wengi wa wakubwa na watu wanaotaka uraisi kimasomo hasa waliopo makazini upendelea sn vyuo hivi Idadi ya PhD holders SUA ni 256 na Mzumbe ni 22 hapo nadhani unapata picha ya ubora wa chuo achilia mbali takwimu iliyotolewa hapo juu ambayo inaonyesha kuwa SUA ni chuo kikubwa tu Africa
   
 6. HOYANGA

  HOYANGA Senior Member

  #6
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  vyuo kama mzumbe, ifm na iaa sio vya kulinganisha na sua na wala sio maarufu kitaaluma kama sua, labda umaarufu katika mambo mengine yasiyokuwa na msingi ndio sua unaweza jaribu kuilinganisha na ikawa sio maarufu!!!!......ila ukitaka shule nenda sua.
   
 7. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  huwezi kuilinganisha sua na hapo red, linganisha sua na kcmc/bugando
   
 8. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Ni kweli sua na udsm ni vyuo vizuri sana kwa upande wa vyuo vikuu,vipi taasisi za elimu ya juu kama dar es salaam institute of technology (dit) zamani dar technical college? Mnakionaje chuo hiki?
   
 9. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #9
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  SUA inaheshimika mkuu..kutokuisikia kwako sio kigezo cha kutokuwa chuo bora.
  pale ni elimu zaidi mkuu
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Dark City
  Nakumbuka Mazimbu,sitaki hata kukiongelea SUA,kwani nilikuwa pale hususani ktk yale makozi ya engineering na BVM,kuna kipande kinaitwa fucult of science yaani dakika yeyote ile jamaa wanakula kichwa,

  anayesema kuwa kozi za SUA hazilipi anajidanya kwa sasa tupo manchi ya watu kwa ajili ya makozi tuliyo yasoma pale SUA,

  Ukitaka utamu wa SUA we peleka mtoto wako ama ndugu yako atakupa jibu,

  nakifananisha na hivi vyuo nipo sasa nao ni mchaka mchaka

  kwa mfano watu wanao soma degree ya kwanza na yapili kwa bongo wanafunzi hawapublish paper zao,lakini hapa ni tofauti sana

  sua
  ardhi ni hazina
   
 11. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Kivipi mkuu?, au unamaana gani? hapa tunazungumzia kwa nini SUA si maarufu wewe unaleta mambo yako ya DIT. any way umaarufu anaoutaka ni kama UDOM kila siku kwenye magazeti ooh jaamaa wamegoma, mara college fulani wamefukuzwa nk, IFM wao ni kwenye skendo mara fulani shoga mara miss katoka IFM pia idadi kubwa ya madenti pale IFM ni MASHALOBALO
   
 12. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  cjazungumzia ubora mkuu,nimezungumzia umaarufu,mfano..vijana weng wanaomalza kdato cha 6,hukimbilia mzumbe,ifm nk 7bu kubwa ikiwa ni kwamba vyuo hvo ni maarufu au lugha nyingne unaweza kusema vina majina huku mtaani,so swali langu ni kwamba kwa nini sua imezidiwa umaarufu na vyuo vichanga kama mzumbe,ifm na vingne?
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Huyo anatoka kulala usingizi wa siesta......sijui anatoka wapi.....sua si chuo maarufu??????koz haziuziki??????MIMI SIJASOMA SUA LAKINI NIMEISH CAMPUS ZA SUA KWA MIAKA MING AND MY PARENT WAZ A LECTURER THERE.......
   
 14. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Yeah wewe unaijua SUA....asante
   
 15. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  me nilijua na wewe umesoma sua,kumbe umeishi 2,wacha waliosoma hapo wa argue hii mada na co wewe ulie ishi sua.
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sasa wewe ambae hata kupajua hupajui.....unataka umaarufu wa kuvaa vimini.....??????si unakiona ni chuo cha 90 afrika????we unadhan wanabahatisha?????
   
 17. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  hiv unajua mwananch wa kawaida wa morogoro anaweza akawa anaijua mzumbe zaidi ya sua mkuu?na hapa siöngelei umaarufu wa kuvaa vimini au vipedo bali nazungumzia umaarufu wa kujulikana miongon mwa watanzania wengi kwa either products zao walzotoa ktk soko au umaarufu wa kozi za chuo husika.
   
 18. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mkuu labda nikusaidie, vijana wengi wanaomaliza A-level wanakuwa wamesoma michepuo ya Arts na Biashara.. Michepuo hiyo SUA kwa iaka mingi hakukuwa na kozi zake. Pale ni pure science yaani unakuta Veterinary Medicine, Agriculture Engineering, Forestry, Animal Science, Crop Science n.k. Vijana wa siku hizi ukiwaambia wasome hayo ni sawa kuwaambia wapande Mlima Kilimanjaro, hawawezi!! Kila mtu anakimbilia BA, Accounts, Tax etc kwenye hivyo vyuo vyenu uchwara!!

  So, kwa mtu asiyeyejua anaona SUA ni chuo cha kishamba!! Mimi nilimaliza UDSM lakini wakati nipo Japan Kagoshima University, ndipo nilipoona umuhimu wa SUA baada ya kukuta wanafunzi wengi wa SUA pale mpaka wa Undergraduate na jinsi jamaa wanavyoshirikiana na SUA katika masuala ya kuendeleza sayansi za kilimo, mifugo na chakula. Imenishawishi kufanya MSc yangu hapa SUA..

  SUA NI CHUO MUHIMU SANA KWA MAENDELEO YA TANZANIA NA UMAARAFU WAKE UPO ZAIDI NJE YA NCHI, SIDHANI KAMA HAPO IMF AU CBE UNAWEZA KUTA PROJECTS ZA KIMATAIFA KAMA ZILIZOPO UDSM NA SUA!!
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wana umaarufu sana tu na kuna coz pale ni hot cake tu mdaumfano B.A RURAL DEVELOPMENT,INATOKA SUA TU KWA TANZANIA HII,LAKINI KUNA VERTENARY,ENVIRONMENTAL ENGINEERING,AGRICULTURE EXTENSION NDIO INATOA MABWANA NA MABIB SHAMBA,BIO-TECHNOLOGY AND LABORATORY SAYANSI,AGRONOMY N AGRIBIZNESS......FOREST NA KADHALIKA,KUNA BAADH YA ORGANIZATION HATA ZIKITOA NAFAS ZA KAZI HUWA WAZ,WANASEMA WANATAKA MTU KUTOKA SUA.......SO U CAN SEE HOW FAMOUS THEY R......PIA KUNA KOZ MPYA YA TUARIZM MENEJMENT.....NADHAN NDO IMEANZA THIS YR
   
 20. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ninachojua mimi SUA ni chuo kizuri, nimeona wengi wanaomaliza chuo hicho wapo karibu kila mahala wanafanya kazi tena nyingi tofauti kabisa na kozi walizosomea , lakini nahisi wanaandaliwa vizuri mbona wanaperfom sana wanafunzi wa SUA, labda jina ndo linapotosha ukweli kuhusu SUA, sio chuo cha Kilimo tu kwani kwa sasa kozi zinazotolewa ni zaidi ya 20 na kozi za kilimo perse hazifiki 10, UDSM inabaki kuwa juu ukilinganisha na SUA hivi vingine vinafuatia
   
Loading...