Kariakoo ni kero, machinga wamejaa kila kona

Kariakoo ni kero, machinga wamejaa kila kona

Yaani mtu ana diliki kusema this country is trash wakati kazaliwa hapa na atazikwa hapa na hana nchi nyingine ya kwenda ama kweli mchawi uliye iroga nchi hii naomba ufufuke there is no patriotism at all.
 
Ukianzia karume njia za waenda kwa miguu zimepangwa bidhaa na cc watembea kwa miguu inabidi tubanane na magari, barabarani kisa! Najua hata baadhi ya viongozi wa mkoa na wilaya hawapendi hiyo hali ila walishapewa maagizo hoa wasiguswe! Ndio mtaji.....
 
Nakumbuka miaka ya nyuma wamachinga na akina mama ntilie walikuwa wakifukuzwa kariakoo na na maeneo mengine na kumwagiwa vyakula vyao au kuchukuliwa vitu vyao...yie hao hao munao lalamika sasa mlikuwa wa kwanza kuitukana serikali kwa kuwaonea hao wamachinga na mama ntilie..narudia kusema aliye turoga alikufa zamani sana nchi hii
 
Wakuu hali ni mbaya kariakoo na viunga vyake, wamachinga wamefunga mitaa yote na baraza zote, hili jambo mkuu baba alizungumzie, hii nchi ni yetu wote, sio wamachinga peke yao. Muheshimiwa baba tuonee huruma na sisi wengine tunaotumia barabara za maeneo ya kariakoo na viunga vyake, wamachinga kwa sasa wamekuwa na jeuri kuliko hata FFU(Fanya Fujo Uone).

Kama kariakoo na viunga vyake vimekuwa ni soko rasmi la wamachinga basi serikali ipige marufuku magari kupita maeneo hayo kwa usalama wa watu na mali zao, maana msukumano uliopo wa wamachinga na waenda kwa miguu ni hatari sana kwenye magari.

Mkuu baba jaribu tu hata kutoka kimya kimya upite maeneo ya kariakoo na viunga vyake uone wananchi tunavyotembea kwa mateso tukihatarisha maisha yetu kwa kugongwa na magari.
Msiwabuguzi waacheni wafanye biashara
 
Hahahaha mbavu zangu jamani /chukua balimi moja ntakulipia
Hii nchi bana
Unaua biashara kubwa zenye kuleta kodi nyingi na kuajiri watu wengi kwa mkupuo huku zikilipa wafanyakazi wake mamilioni ya mishahara.
Halafu unazalisha machinga wa kutosha wa kuuza vibanio vya kuanikia nguo na sumu ya panya.

Baadaye unapita majukwaani unalaani "Urais ni terrible job"
 
Kariakoo ndio penye biashara huko posta mpya ubishoo tu. Asiyetaka usumbufu wanaweza kununua mahitaji online sio lazima waende kariakoo.
 
Maajabu ya kariakoo
Kuzunguka na kurudi kwenye duka ulilotoka bila kujijua ni kitu cha kawaida, ila
Kutafuta tena duka ulilotoka si jambo la kawaida,
kununua bidhaa uliyoifuata ni 50/50,
Kurudi hujavurugwa kichwa kwa namna yoyote ile n 50/50,
Kurudi mda uliopanga ni 0/100
 
Kariakoo ni shida kwa kweli. Sijui hata wale wenye maduka rasmi kama wanafanya biashara vizuri. Kwa kuwa Rais ni taasisi na ana macho/masikio mengi, ngoja tuwe na subira. Maoni yetu yatamfikia one day.
 
Ni Tanzania tuu ndio utakutana na uholela huu hakuna popote duniani kuna taifa la kimachinga,
 
Back
Top Bottom