Kariakoo kuna nini?

Kariakoo kuna nini?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,260
Imeshakuwa kama kamchezo kwa viongozi mbalimbali kuitumia Kariakoo kama mfano mbaya pale wanapotaka kufananisha na jambo baya
Awali kabisa alikuwa Makamba. Nikaja kumsikia tena jamaa mmoja akiitwa Komba. Yupo PWC kama auditor. likuwa katika kipindi cha kippima joto ijumaa iliyopita-itv. sasa tena huyu mama Makinda. Msiwe kama watu wa Kariakoo. Watu wa Kariakoo ni kina nani hao? Ni wale wanaoishi pale au wale wanaofanya biashara na kununua?

KWa mtazamo wangu, kama Kariakoo isingekuwa sehemu ya biashara basi pagekuwa patulivu sana. Pangekuwa ni makazi tu ya watu hivyo kutokuwa na pilika zilizopo sasa. sasa tatizo ni pale sehemu hiyo kuwa ya kibiashara. kama wewe msomaji hujapita kariakoo leo utapita wiki ijayo. nami kadhalika. Kwa mantiki hiyo wale wa Kariakoo wanaopigiwa mfano na hawa viongozi ni MIMI na WEWE!! sisi ndio watu wa Kariakoo maana ile sehemu ni eneo lisilokwepeka kufika.

Mnakubaliana na hawa waropokaji?
 
nafikiri wanamaanisha order.
kariakoo kuna vurugu hivi...
watu wengi na eneo dogo...
 
Kariakoo ninayoijua mimi
pita mida ya kuanzia saa moja usiku na kuendelea, ni sehemu iliyotulia kama masaki au obey, papo kimya, wenyeji wamekaa vibarazani wanakula urojo,mishkaki au kahawa.
hamna kelele, so pieceful place to live.ukikuta kikundi cha wavulana wamekaa sio kwamba wanavuta bangi, ni story tu za hapa na pale.
ni sehemu ambayo hautasikia kuna mwanamke ka kabwa, mwanamke unaweza kunatembea usiku wa manane bila ya wasiwasi.

Kariakoo wanaoijua hao viongozi na wale ambao hawajahi kuishi kariakoo ni ile yakuanzia saa 10 alfajiri mpaka saa 12 jioni.
kariakoo yenye kelele, msongamano wa magari, vurugu za wapiga debe na wafanya biashara ambao hao wote ni wakuja wametokea vitongoji au mikoa mengine.
 
si vizuri lakini. wanaishushia hadhi kariakoo
 
Kwa nini watolee mfano kariakoo tu wakati kuna sehemu nyingi kuna vurugu lakini hawazisemi?
 
si vizuri lakini. wanaishushia hadhi kariakoo

hakuna mwenye ubavu wa kuishusha hadhi kariakoo

wao wenyewe walipofika dar mara ya kwanza,walikuwa wanajiuliza
kariakoo ndio wapi...

actually kariakoo ndio eneo maarufu kuliko yote tanzania

na soko la kariakoo ndio kitu maarufu kuliko mtu yeyote wala kitu chochote kingine daresalaam

so wanajifanya tu wanapajua kariakoo,inawapa ujiko huko vijijini kwao
 
kariakoo ni sawa na manhattan islands ya marekani
hapa east africa....

kuna wafanyabiashara kutoka zambia.malawi,commoro,drc.
kenya,uganda,msumbiji.south africa,china,thailand.uk ,us,india
na karibu nchi zote tunazofanya nazo biashara....

pesa inayozunguka kariakoo kwa siku,
liquid ,ni nyingi mno.zaidi ya mra elfu moja ya transaction za daresaalam stock exchange
na pengine mara nyingi ya liquid inayotumika bot....kwa siku...

tungekuwa na viongozi wenye akili,kariakoo ni tayari eneo la kimataifa la kibiashara..

wangeweke facilities nyingi na kuhakikisha usafi wa eneo.....

wanachojua wao ni kuponda tu...
hivi kuna mtu anaeweza tafuta data,kama simu ngapi zinauzwa kariakoo kwa siku?????
suruali???????mashati????????
pesa kiasi gani inazunguka kwa siku????????
 
Imeshakuwa kama kamchezo kwa viongozi mbalimbali kuitumia Kariakoo kama mfano mbaya pale wanapotaka kufananisha na jambo baya
Awali kabisa alikuwa Makamba. Nikaja kumsikia tena jamaa mmoja akiitwa Komba. Yupo PWC kama auditor. likuwa katika kipindi cha kippima joto ijumaa iliyopita-itv. sasa tena huyu mama Makinda. Msiwe kama watu wa Kariakoo. Watu wa Kariakoo ni kina nani hao? Ni wale wanaoishi pale au wale wanaofanya biashara na kununua?

KWa mtazamo wangu, kama Kariakoo isingekuwa sehemu ya biashara basi pagekuwa patulivu sana. Pangekuwa ni makazi tu ya watu hivyo kutokuwa na pilika zilizopo sasa. sasa tatizo ni pale sehemu hiyo kuwa ya kibiashara. kama wewe msomaji hujapita kariakoo leo utapita wiki ijayo. nami kadhalika. Kwa mantiki hiyo wale wa Kariakoo wanaopigiwa mfano na hawa viongozi ni MIMI na WEWE!! sisi ndio watu wa Kariakoo maana ile sehemu ni eneo lisilokwepeka kufika.

Mnakubaliana na hawa waropokaji?

Nashangaa kwa nini viongozi wa serikali wanapasema vibaya Kariakoo wakati data rasmi zinaonesha Kariakoo kuna transaction ya over 10 billion inafanyika kila siku! Kwa maana hiyo Kariakoo ni muhimu sana kwa uchumi wetu kuliko wanavyofikiri
 
ni zaidi ya hapo...
bilioni kumi ni ndogo..
 
kariakoo ni sawa na manhattan islands ya marekani
hapa east africa....

kuna wafanyabiashara kutoka zambia.malawi,commoro,drc.
kenya,uganda,msumbiji.south africa,china,thailand.uk ,us,india
na karibu nchi zote tunazofanya nazo biashara....

pesa inayozunguka kariakoo kwa siku,
liquid ,ni nyingi mno.zaidi ya mra elfu moja ya transaction za daresaalam stock exchange
na pengine mara nyingi ya liquid inayotumika bot....kwa siku...

tungekuwa na viongozi wenye akili,kariakoo ni tayari eneo la kimataifa la kibiashara..

wangeweke facilities nyingi na kuhakikisha usafi wa eneo.....

wanachojua wao ni kuponda tu...
hivi kuna mtu anaeweza tafuta data,kama simu ngapi zinauzwa kariakoo kwa siku?????
suruali???????mashati????????
pesa kiasi gani inazunguka kwa siku????????
huu ujumbe ungemfikia huyo mama nadhani angebadili mtazamo
 
Nashangaa kwa nini viongozi wa serikali wanapasema vibaya Kariakoo wakati data rasmi zinaonesha Kariakoo kuna transaction ya over 10 billion inafanyika kila siku! Kwa maana hiyo Kariakoo ni muhimu sana kwa uchumi wetu kuliko wanavyofikiri
ni sawa na Guanzou (sijui kama ni sahihi) ya China
 
Wanaoisema Kariakoo vibaya ni wakuja. Wivu tu umewajaa, wanatamani na kule udongini kwao, kungekuwa kama Kariakoo.
 
dah! nimemsikia vizuri muda huu kupitia mlimani tv. kasema wabunge wajiheshimu na wasiwe kama watu wa Kariakoo. Kwa mantiki hiyo hajaichukulia Kariakoo kama sehemu ya pilika bali sehemu ya fujo na ya watu wasiojiheshimu. Haya mamaa wa Sinza mfunga barabara
 
Back
Top Bottom