Kardinali Pengo: Maisha yamekuwa nafuu sana awamu hii

Amri ya mpende jirani yako kama nafsi yako,hii ndo amri itakayo waangusha wengi kuuona ufalme wa Mungu,huyo ni Askofu anayekula na kusaza wakati majirani zake wanashindia mlo mmoja na pahala pengine wanashindia na kulalia uji,then yeye anakuja na kusema kuna nafuu??????????????.Labda kwake na watu wa aina yake siyo kwangu na raia ninao ishi nao huku mitaani.
 
Kwa hiyo hutaki?
 
Kwa hiyo hutaki?
 
Ngoja kuna Siku nitapiga picha nitaitupia humuu muone nyumbani kwa akina pengo , pamoja na umaarufu wote wa pengo ila kwao mmmmmmh huwezi amini , ni wengine wanaamini pengo Alisha laaniwa kwa kutojari kwao , ni mnafiki sana huyo subirini nitawletea full story ya pengo
 
Wa dini gan mkuu. Hivi we umeona kitu gani kimekuwa hakipatikan kwako. Heb tueleze kinaga ubaga. Labda mshahara wako umepungua. Au kuna bidhaa hazipatikan au tatizo ni nn. Au labda bidhaa zimepanda bei. Heb tamka watu wakusikie. Tatizo ni nn. Kitu gan kimepunguzwa kwako. Mm ambae nilikuwa nategemea kipato changu halali naona mambo yamekuwa rahisi sana. Huduma zimekuwa rahis sana kupatikana na zenye ubora kabisa
 
Fisadi ni fisadi..! Chama kitakachoweka fisadi kama mgombea 2020 kisahau kushinda!Rai hii iende kwa vyama vyote...
 
PengO hana akili. Aache mambo kis.enge

Hivi anajua ugumu wa maisha.

Labda anamaana awamu hii kuna unafuu wa maisha ya kikristo maana MAGUFULI AMEWAWEKA WAKRISTO WENGI ZAIDI KWENYE UONGOZI (MORE THAN 92%) KULIKO AWAMU ZINGINE ZOZOTE
Tumia busara unavyo comment mkuu
 
......
......Salute
 
Toka askofu Pengo alipokwenda kinyume na baraza la maakofu katoliki (TEC) na TCC kipindi cha kuandaa katiba mpya nimebaki namwangalia tu lakini simwelewi kabisa kuhusu kazi ya kanisa ambayo ni kushughulikia uzima wa mwili na roho.Kwa upande wa uzima wa mwili maana yake hapo siasa inaingia.Hivyo ni wajibu wa kanisa kuangalia hata siasa ya nchi inaendaje kwani siasa ndio maisha ktk nyanja zote zana maisha yaani elimu,utamaduni,na uchumi. Kama taifa tulihitataji katiba mpya ili kutoa muelekeo bora wa maisha ya kimwili ambapo wananchi wote walitoa maoni ambayo baadaye yalipingwa na kikundi cha watu/chama na yeye akaunga mkono kikundi hichokinyume na maoni ya wananchi na maazimio ya TEC na TCC. Hali hiyo ndio iliyomuibua askofu Gwajima na kufanya mambo yake.Sasa wakati tunasahau hayo yaliyopita leo anasema maisha yamekuwa rahisi kwa kigezo cha yeye kupanda ndege kwa bei rahisi bila kumwangalia mwananchi wa chini ambaye hawazi wala kufikiria kupanda ndege wakati hata basi linamshinda hivyo kukimbilia treni ambayo haijaboreshwa mpaka sasa. Hapo ndipo mimi naposhindwa kumwelewa kiongozi wangu wa imani kuwa amesimamia kwa sisi wanakondoo au kwa wateule wachache kinyume na biblia ambayi inataka ukombozi wa wote
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…