Kardinali Pengo: Maisha yamekuwa nafuu sana awamu hii

Amri ya mpende jirani yako kama nafsi yako,hii ndo amri itakayo waangusha wengi kuuona ufalme wa Mungu,huyo ni Askofu anayekula na kusaza wakati majirani zake wanashindia mlo mmoja na pahala pengine wanashindia na kulalia uji,then yeye anakuja na kusema kuna nafuu??????????????.Labda kwake na watu wa aina yake siyo kwangu na raia ninao ishi nao huku mitaani.
 
Leo wakati najiandaa kwenda kanisani ibada ya pili nikasema ngoja niweke redio yetu tumaini.
Baba Askofu akitoa salamu za xmas kwa waumini alisema kuwa yeye anaona maisha yana nafuu sana, labda kwa wale ambao walizoea kupata fedha ambazo si halali ndio wanaolalamika, kukazia hilo akasema mavuno ya mwaka huu waliweka target ya kukusanya kiasi kikubwa cha fedha, watu watatu wakamfuata wakati akitangaza malengo hayo na kumuuliza hizo ela zitapatikanaje wakati watu hawana ela baba askofu? Anasema yeye hakuwajali na akawambia fedha zitapatikana na kweli zikapatikana sasa leo anasema akisikia watu wanalalamika anashangaa wakati malengo yao yalitimia.
Akaendelea kusema kuwa awamu hii kwake ni nafuu sana kwani akipanda ndege kwenda kwao kwa shirika la atcl ni karibu nusu ya nauli ambayo mashirika mengine yanatoza, kwa hiyo awamu hii yeye anaona inaunafuu sana.
Basi nikazima redio kwa upole na kuelekea zangu kanisani huku nikiwaza ule ukali wa maaskofu haupo tena awamu hii?
Kwa hiyo hutaki?
 
Ngoja kuna Siku nitapiga picha nitaitupia humuu muone nyumbani kwa akina pengo , pamoja na umaarufu wote wa pengo ila kwao mmmmmmh huwezi amini , ni wengine wanaamini pengo Alisha laaniwa kwa kutojari kwao , ni mnafiki sana huyo subirini nitawletea full story ya pengo
 
Wa dini gan mkuu. Hivi we umeona kitu gani kimekuwa hakipatikan kwako. Heb tueleze kinaga ubaga. Labda mshahara wako umepungua. Au kuna bidhaa hazipatikan au tatizo ni nn. Au labda bidhaa zimepanda bei. Heb tamka watu wakusikie. Tatizo ni nn. Kitu gan kimepunguzwa kwako. Mm ambae nilikuwa nategemea kipato changu halali naona mambo yamekuwa rahisi sana. Huduma zimekuwa rahis sana kupatikana na zenye ubora kabisa
 
PengO hana akili. Aache mambo kis.enge

Hivi anajua ugumu wa maisha.

Labda anamaana awamu hii kuna unafuu wa maisha ya kikristo maana MAGUFULI AMEWAWEKA WAKRISTO WENGI ZAIDI KWENYE UONGOZI (MORE THAN 92%) KULIKO AWAMU ZINGINE ZOZOTE
Tumia busara unavyo comment mkuu
 
Unafiki ni sifa muhimu sana kwa kiongozi yeyote wa Africa...pia Africa kwetu hapa DINI na SIASA ni mtu na mkewe...

Pengo anatia huruma sana...

Yaani hii dunia,everybody wants to stick a dick to a common mwananchi,sijui wanatatubakisha wapi...

Ndio maana siamini dini yoyote na wala mungu yoyote au shetani yeyote...all these are spooky businesses!
......
......Salute
 
Toka askofu Pengo alipokwenda kinyume na baraza la maakofu katoliki (TEC) na TCC kipindi cha kuandaa katiba mpya nimebaki namwangalia tu lakini simwelewi kabisa kuhusu kazi ya kanisa ambayo ni kushughulikia uzima wa mwili na roho.Kwa upande wa uzima wa mwili maana yake hapo siasa inaingia.Hivyo ni wajibu wa kanisa kuangalia hata siasa ya nchi inaendaje kwani siasa ndio maisha ktk nyanja zote zana maisha yaani elimu,utamaduni,na uchumi. Kama taifa tulihitataji katiba mpya ili kutoa muelekeo bora wa maisha ya kimwili ambapo wananchi wote walitoa maoni ambayo baadaye yalipingwa na kikundi cha watu/chama na yeye akaunga mkono kikundi hichokinyume na maoni ya wananchi na maazimio ya TEC na TCC. Hali hiyo ndio iliyomuibua askofu Gwajima na kufanya mambo yake.Sasa wakati tunasahau hayo yaliyopita leo anasema maisha yamekuwa rahisi kwa kigezo cha yeye kupanda ndege kwa bei rahisi bila kumwangalia mwananchi wa chini ambaye hawazi wala kufikiria kupanda ndege wakati hata basi linamshinda hivyo kukimbilia treni ambayo haijaboreshwa mpaka sasa. Hapo ndipo mimi naposhindwa kumwelewa kiongozi wangu wa imani kuwa amesimamia kwa sisi wanakondoo au kwa wateule wachache kinyume na biblia ambayi inataka ukombozi wa wote
.
 
54 Reactions
Reply
Back
Top Bottom