Kardinali Pengo: Maisha yamekuwa nafuu sana awamu hii

cjilo

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
884
250
Leo wakati najiandaa kwenda kanisani ibada ya pili nikasema ngoja niweke redio yetu Tumaini.

Baba Askofu akitoa salamu za Xmas kwa waumini alisema kuwa yeye anaona maisha yana nafuu sana, labda kwa wale ambao walizoea kupata fedha ambazo si halali ndio wanaolalamika.

Kukazia hilo akasema mavuno ya mwaka huu waliweka target ya kukusanya kiasi kikubwa cha fedha, watu watatu wakamfuata wakati akitangaza malengo hayo na kumuuliza hizo hela zitapatikanaje wakati watu hawana hela baba askofu?

Anasema yeye hakuwajali na akawaambia fedha zitapatikana na kweli zikapatikana sasa leo anasema akisikia watu wanalalamika anashangaa wakati malengo yao yalitimia.

Akaendelea kusema kuwa awamu hii kwake ni nafuu sana kwani akipanda ndege kwenda kwao kwa shirika la ATCL ni karibu nusu ya nauli ambayo mashirika mengine yanatoza, kwa hiyo awamu hii yeye anaona ina unafuu sana.
Nikakumbuka na issue ya katiba mpya namna alivyoharibu na kupingana na baraza la maaskofu wakatoliki, nikasikitika sana kwa kweli nikaona kama kuna wa dini tofauti amesikiliza mda huo basi tutakuwa tumedharaurika sana sisi waamini.

Basi nikazima redio kwa upole na kuelekea zangu kanisani huku nikiwaza ule ukali wa maaskofu haupo tena awamu hii?

Ushauri:TEC imzuie askofu huyu kutoa matamko badala yake kauli nzito kama hizi ziwe zinatolewa na TEC au zipate baraka zake. TEC imuonye askofu huyu pia itoe tamko kauli ile ni ya Askofu bimafsi wala si kanisa katoliki.
Akhsante.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,984
2,000
Ni ngumu mtu mweusi kukata tawi alilo kalia........."Unafiki ni sifa ya viongozi wote wa siasa na wa dini mbinguni ni kugumu sana kufika hasa unapukuwa mcha Mungu na unayetaka kumkosoa ndio maslahi yako"

Sio Pengo tu Wapi mabalaza yaliyokuwa yakikaa kila baada ya mwezi mara dodoma Arusha Dar......
 

haa mym

JF-Expert Member
Jul 7, 2014
4,469
2,000
Ndio maana sina wasiwasi na hawamu hii najua mtakosoa sana ila kwenye imani letu linakua moja aijarishi ni chama gani au dhehebu gani.
 

LebronWade

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,615
2,000
Unafiki ni sifa muhimu sana kwa kiongozi yeyote wa Africa...pia Africa kwetu hapa DINI na SIASA ni mtu na mkewe...

Pengo anatia huruma sana...

Yaani hii dunia,everybody wants to stick a dick to a common mwananchi,sijui wanatatubakisha wapi...

Ndio maana siamini dini yoyote na wala mungu yoyote au shetani yeyote...all these are spooky businesses!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom