Karamu ya mwisho na majigambo ya mtandao

Karamu ya mwisho na majigambo ya mtandao

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,898
Reaction score
828,493
Tarehe 12.8.2025 itaingia kwenye kumbukumbu za Tanganyika kwa mambo mengi

1. Majigambo ya nguvu ya mtandao kwamba wana watu wazito na wana ukwasi wa kutosha

2. Ithibati kamili kwamba chama kimetekwa na kundi maslahi linalojumuisha wevi, mafisadi, ma tycoon wa rushwa, watakatishaji pesa na mtandao unaoamua hatima ya Tanganyika huku kundi asili likibezwa na kupigwa vijembe vya kila aina

3. Kwamba uchaguzi umeshakwisha na hiyo ilikuwa hafla ya kupongezana

4. Watanganyika wasiojitambua waliobebwa kwenye mtumbwi wa vibengwo.. Walikuwa kenge kwenye msafara wa mamba! Kuna mmoja ahadi yake ikatajwa ya 5M kutoka Simiyu alimaindi vibaya sana..!

5. Chukizo jipya kwa walalahoi wanaokishabikia chama kinachoendeshwa na tabaka fulani.. Hilo ndio linakula mema ya Tanganyika (keki ya Tanganyika)

6. Sifa, ubabe, show offs, kejeli za waalikwa..

7. Kilichoitwa harambee ni KARAMU YA MWISHO kwa chama! hakitakaa kifanye tukio kama hili tena maana limekuwa chukizo na dhihaka kubwa mbele za macho ya Mungu na Watanganyika pia.. Huu ndio mwisho na hakuna mwisho mwingine zaidi ya huu.
 
Tone tone mnaiona iko sawa, ila harambee ya CCM ndio haiko sawa? Tone tone unamuweka Lemma ambaye ana tuhuma za wizi wa magari Arusha?
Kama huelewi kilichoandikwa kaa kimya kuficha upumbavu wako
IMG-20250812-WA0004.jpg
 
Bahati mbaya hata nzi kutokana na hali yake na asili yake pia anaweza kujisifia kuhudhuria karamu ya wafalme kwa vile amelamba makombo yaliyodondoka chini.
Ni aibu fisadi anakuibia wewe pesa za kurekebishia hospitali yenu ya rufaa hadi mzazi wako akapoteza maisha halafu anachangia 10B nawe unashangilia.
Ukiitwa bwege utashangaa? Walipo hao majizi na mafisadi kila mmoja ujue wenye njaa na ufukara wapo elfu moja! Sasa Watanzania mbona tunakuwa mafala hivi?
Nani wa kuja kutuondolea hawa kama sio wenyewe?
Yaani tumekuwa wa kukebehiwa na Azim Dewji hadharani? Halafu tunachekelea?
TUMELOGWA!
 
Bahati mbaya hata nzi kutokana na hali yake na asili yake pia anaweza kujisifia kuhudhuria karamu ya wafalme kwa vile amelamba makombo yaliyodondoka chini.📌🔨💪🏿✌🏿
 
Back
Top Bottom