Karagwe: Mnyauko na mabango ya mseveni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karagwe: Mnyauko na mabango ya mseveni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chitambikwa, Jan 10, 2011.

 1. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hivi karibuni nilienda karagwe ambayo ni moja ya wilaya hapa tanzania haijawahi kupata chakula cha msaada kutokana na kuwa na migomba mingi mizuri ,hari ya nzuri ya ikweta , udongo wenye rutuba na wingi sana wa mifugo hasa ng,ombe.

  Kwa sas kuna ugonjwa umeikumba migomba unaitwa Mnyauko viongozi wao hasemi chochote na wala inayojiita serikali haijawambia wananchi watakula nini. kahawa na migomba inanyauka na kwa sasa vigogo tu ndo wanakula ndizi.

  Kwenye mkutano mmoja wa hadhara katika kata ya kaisho watu wameanza kushutumiana waziwazi wakihoji ipo wapi serikali ,na mbunge wao ambaye wanadai anazima simu akipigiwa. Kila mtu kwa sasa anamwona mwenzake mchawi hasa kwa sababu watu waliamini Dr.Slaa atashinda uchaguzi na maisha yatakuwa mazuri.
  Wengine kwa hasira waliambizana kwa hasira mtakula CCM ngumi zikawaka. nilishutuka hasa sikuwahi kuoona hari kama hii huko nyuma nikajiuliza maswali yafuatayo.

  1. Mbunge wa kyerwa,karagwe mpo wapi?
  2. Serikali iko wapi karagwe?
  3. Bei nzuri ya kahawa ipo wapi?

  lakini mabango ya
  VOTE FOR MSEVENI
  YOU WANT ONOTHER RAP YEA! YEA! yametundikwa sehemu nyingi sana hapa

  na REDIO ZINAZISIKILIZWA NI ZA UGANDA, RWANDA NA MOJA YA HAPO KAYANGA .
   
 2. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  We acha porojo.
  Ugonjwa huo wa mnyaukoi bacteri ni wa siku nyingi kiasi ulitokea nchini uganda na wakulim wa huko wamekwisha elimishwa kuhusu namna ya kudhibiti huo ugonjwa.Mimi mwenyewe nilikuwa mmoja wa watu waliokuwa katika timu hiyo(sifanyi kazi serikalini) na huko Kaisho tulifika.

  Unachoweza kusema ni kuwa elimu hiyo haikuwafikia wananchi wengi na si kweli kwamba serikali imewasahau.

  Ushauri:Acha kuchanganya siasa na issue kama hizi na mambo ya siasa

  Karibu Karagwe,kagera na ukweli ni kuwa hata ugonjwa huo ushambuliwe mashamba yote lakini KARAGWE haiwezi kufafanana Singida,Tabora au Dodoma kwa ukame
   
 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  kweli karagwe ina hali nzuri ya hewa, ila ugonjwa huu wa mnyauko ni hatari. Nilisikiliza redio moja hivi karibuni (sikumbuki ni radio karagwe au radio fadeco), kuna mtu alisema yeye amegundua dawa ya ugonjwa huo kwa kuchanganya dawa mbalimbali za kuua magugu.
  Sasa kama mtu binafsi anaweza kuhangaika kupata dawa, idara ya kilimo yenye wataalamu imefanya juhudi gani?
  Suala la kuuliza wabunge wako wapi si la kisiasa zaidi katika hili, bali ni kutaka wabunge waonane na wananchi wao ili waelezwe nini wakaseme bungeni juu ya mnyauko nk.
  Tatizo la wabunge wetu kutowakilisha mawazo ya wananchi si la Karagwe na Kyerwa tu
   
 4. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Mbona dawa yake ipo ingawa inaogopesha kidogo kwani hasa ni kung'oa migomba yote iliyoshambuliwa na kifaa kinachotukika kukipitisha kwenye majivu/moto na mambo mengine ambayo suiwezi kuaeleza hapa(kumbuka me siyo mtaalamu wa kilimo)

  Pale Maruku kuna mtaalamu wa suala hili anaitwa Byabachwezi
  Siku za baadaye nitaeleza ni kwa nini tatizo hili,chanzo chake na ubutu kwa wataalamu hao
   
 5. C

  Campana JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wewe Mathias - Unamshambulia Chitambikwa kwa vile amekutangulia kuitoa habari hii Jamiiforums? Ungependa uipate kwanza uiuze kwenye media? Nadhani yuko sahihi. Ugonjwa wa migomba upo, na wabunge waliochaguliwa hawaonekani huko.
   
Loading...