Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha!

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
4282090.jpg

Waziri Kapuya Saturday, March 27, 2010 4:49 AM
Katika hali isiyo ya kawaida kwa viongozi wa juu nchini kuonekana katika kumbi za starehe tena katika sare sambamba na waimbaji wa bendi, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya aliingia ukumbini na kuyarudi mapigo ya pekecha pekecha ya wana wa Akudo. Huku akiwa amevalia sare sawa na waimbaji wa bendi ya Akudo, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya alijitosa ukumbini na kuanza kuyarudi mapigo ya pekecha pekecha ya bendi ya Akudo Impact iliyokuwa ikitoa burudani kwenye ukumbi wa Msasani Beach.

Kapuya ambaye ndiye mmliki wa bendi hiyo alijimwaga stejini na kusakata muziki kwa nguvu zote huku jasho likimtoka akiwa pamoja na mpambe wake ambaye jina lake halikufahamika.

Kapuya anakuwa kiongozi wa pili wa juu serikalini kumiliki bendi wa kwanza alikuwa Waziri Mdhihiri Mdhihiri ambaye aliwahi kumiliki bendi ya Mchinga Sound ambayo baadaye ilivunjika.

Kutokana na jinsi anavyoithamini bendi yake, waziri Kapuya amefanikiwa kuifanya bendi ya Akudo iwe miongoni mwa bendi zinazopendwa sana nchini kiasi cha kuleta ushindani mkubwa katika medani ya muziki wa dansi hapa nchini.
 
Iyo mbna iko vizuri tu yeye kajimwaga wazi,je angeenda kujimwaga kwenye maficho kaweka mambo adharani''''''''''''''''''''
 
hapo kaonesha picha yake halisi, kwa hiyo hata maamuzi mengine anayoyafanya na atakayoyafanya ni lazima tuwe pia tunareflect back
 
Afu nasikia kwa sasa Akudo watakuwa kwenye kampeni za mgombea wa CCM...ulaji kwa mmiliki wa bendi...Sidhani kama inakatazwa kwa Public figures kujinafasi kwa raha zao wakiwa kwenye matamasha..mzuka ukipanda nawe unaupandisha tu!!
 
hapo kaonesha picha yake halisi, kwa hiyo hata maamuzi mengine anayoyafanya na atakayoyafanya ni lazima tuwe pia tunareflect back

nae pia ni binadamu, anahitaji kupumzika na kupata burudani....khaaa!!! watu wengine bana.....mkojeeeee?????
 
sio mbaya kama akiwa kazini anafanya kazi vizuri anaweza ku-socialize baada muda kazi kama mimi ninavyofanya sio kuendekeza UFISADI
 
Naona anajaribu kujiliwaza na joto la mgomo wa wafanyakazi hapo tarehe 05/05,sijui itakuwaje!
 
Naona anajaribu kujiliwaza na joto la mgomo wa wafanyakazi hapo tarehe 05/05,sijui itakuwaje!

Kwa tunaomjua ni alhaji anaependa raha/starehe ya wazi na si ya kinafki kama wengine!!!!! kula raha ila kumbuka mgomo uko palepale unaoweza kumwaga uwaziri wako:rolleyes:
 
Yeye pia ni bin-adam anahitaji kupumzika na kujinafasi.....hongera kwa kujipa raha mwenyewe but next time come out with your mrs. na sio mpambe!!!!
 
Ngoja arelease tension na kujikusanya manake siku zaja za kuomba kura atazunguka kwenye vumbi mpaka basi na atacheza tu ngoma za kienyeji!
 
Jamani mazoezi ya kampeni ndo yashaanza hayo! si wajua Obama na my waifu wake walidance wakati wa kampeni? nasikia tume ya uchaguzi TZ wanataka kuiingiza Dance kwenye utaratibu wa kampeni,sasa isije pigwa pekecha pekecha watu wakatuchezea twist..Natania,lakini nimeipenda hiyo kwa nini ujibane wakati uwezo wa kushambulia dance floor upo?
 
Maadamu anaselebuka baada ya muda wa kazi mimi nadhani haina shida. Kama mwimbaji moja aliwahi kusema kwamba RAHA JIPE MWENYEWE bwana
 
Mahali pake kabisa .... waziri wa maendeleo ya vijana, yes, mara moja moja rukhsa! plus he looks fit, pamoja na kuwa Waziri muda mrefu hajajaa kama BM .. kuku mzimaaa!
 
Mimi nampa Big Up kwanza anarelax bila ya kuogopa na pia anaitangaza biashara yake vema ati! Penda chako kwanza bana kuna maana gani ya kumiliki bendi halafu yeye hata mziki wake haujui?
 
Back
Top Bottom