Tatizo la approach yako ni kwamba unashambulia watu waliomuamini Captain Tesha badala ya kuchambua mazingira yaliyomfanya ajitokeze na kutoa kauli ile.
Hii ni logical fallacy ya ad hominem, badala ya kushughulika na hoja, unashambulia watu binafsi.
Captain Tesha alifanya jambo la kipekee na la ujasiri.
Kumbuka Tesha alitumia jina lake halisi, hakujificha, na alitoa ujumbe wa matumaini kwa wananchi waliokuwa wamekata tamaa kutokana na matukio ya utekaji na mauaji.
Katika mazingira ambayo kusema ukweli kunaweza kukugharimu uhai wako, kitendo cha kujitokeza hadharani ni cha kuenziwa.
Kutorudi tena hakumaanishi alidanganya, kuna sababu nyingi za msingi zinazoweza kumfanya ashindwe kurudi, ikiwemo vitisho kwa familia yake au shinikizo kutoka vyombo vya dola.
Hizi ni sababu ambazo mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kuelewa.
Ni rahisi kwako kubeza ukiwa salama nyuma ya fake ID, bila sura, bila jina, na bila familia yako kujulikana.
Lakini ni vigumu kujitokeza hadharani na kupaza sauti dhidi ya utawala unaotumia nguvu.
Mwa hiyo kubeza jitihada za Tesha naona ni unafiki kwa sababu hujafanya hata nusu ya kile alichothubutu kufanya.
Tesha ali play part yake na alitoa mchango wake wa kipekee na tunamshukuru kwa hilo kwasababu sio wote wanaweza.
Hata kama hakurudi mara ya pili, sababu zake zinaweza kuwa nzito na za msingi.
Halafu hoja yako kwamba “mapinduzi hayatangazwi kabla” haina mashiko kwa sababu historia imetuonesha mara nyingi watu waliotoa onyo au kauli za matumaini kabla ya mabadiliko makubwa.
Thomas Sankara alitoa hotuba kali kabla ya mapinduzi ya Burkina Faso, Martin Luther King Jr. alitangaza ndoto ya “I Have a Dream” kabla ya mabadiliko ya kisheria kutokea Marekani. Kauli za onyo na matumaini mara nyingi hutangulia vitendo.
Kwa hiyo, Tesha kutoa onyo hakumfanyi awe muongo, bali ni sehemu ya harakati za kuamsha hamasa na fikra za wananchi.
Hapa hoja yenye mantiki ni kwamba Tesha alitoa mchango wake na raia wengi wana appreciate so kubeza jitihada zake ni kupuuza mazingira halisi ya gharama za kisiasa katika jamii.