Lakini sasa ni wakati umefika pia kama mzazi/mlezi jitahidi uanze kujifunza kujua hizi mambo.
Mimi kijana wangu mwaka juzi hakufanya vizuri sana kidato cha nne, then akatamani kusomea MARINE courses. Then nilikaanae nikamwambia advantage na disadvantages zake, mwisho nikamshauri aanzie veta akasome MTM course kwa miaka miwili, then ataomba Diploma kusomea MECHANICAL engineering ambayo kwake itakua nzuri kwa kuanzia ama kujiajiri na kuajiriwa pia.
Saizi anaendelea njema na masomo anayafurahia pia amekua ananipa mipaango yake ya baadae, hii ikinionyesha kwamba kijana ameanza kuiandaa future plan yake.