Kanye West Anataka Kubadilisha Jina Ili Aitwe YE

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,780
20,179


Msanii na Rapper maarufu Kanye West ameiomba mahakama ya jijini Los Angeles huko California nchini Marekani kubadilisha jina lake kutoka Kanye West na badala yake awe anajulikana kwa jina la Ye peke yake. Kanye ambaye jina lake kamili ni Kanye Omari West, ametuma maombi hayo rasmi akitaja sababu zake binafsi kuwa msukumo wa ombi hilo. Kanye anataka jina pekee liwe Ye bila ubini wowote.

Ombi hili la Kanye West linakuja miaka mitatu baada ya msanii huyo ambaye pia ni mbunifu wa mitindo ya mavazi na mgombea wa Urais mwaka jana aliwahi ku-tweet kwamba anatumaini kubadili jina lake baada ya kutoa albamu yake inayofuatia. Mara nyingi amekua akitumia jina Ye kwenye mitandao ya kijamii likiwa pia jina la album yake ya mwaka 2018.

Hivi sasa Kanye yupo katika mchakato wa kutalakiana na mkewe wa zamani, Kim Kardashian tangu wawili hao walipotangaza kutengana mwezi Februari mwaka Huu. Kanye pia yupo mbioni kuachia album yake mpya iliyopewa jina “DONDA” mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti. Kanye ana umri wa miaka 44.
 
Back
Top Bottom