Wewe pambana na mke wako! Ukioona hana msimamo ujue hafai kuwa mke.
Imeandikwa Usilipize kisasi.Kwanza anza mchakato wa kununua bastola na ajue kuwa unayo.akimgonga mkeo nawe mtafute mkeww aliyeondoka umgonge be ngoma droo
Wazungu wanasema "Knowing your enemy, half the battle is finished". Kwa hiyo mkuu huna haja ya kuhangaika naye wewe zidisha maombi,fanya mambo yako,acha kumfikiria huyo jirani yako,ataumbuka mwenyewe.
Mfano wako wa uongo alafu unasema umeokoka.watu waliidumu ndoani kwa miaka 45 hawana umri huo uliotajaMiaka 16 ni mingi kweli lakini katika ndoa ni kama siku 1 tu kwani nilichojifunza kuhusu ndoa uwingi wa miaka ya ndoa si kigezo kikuu cha kupima uwezo wenu kuendesha ndoa , wapo wazee wanashindwa kuelewana baada ya maisha kustaafu kazi kuanza , nimeshuhudia ndoa ya wazee waliodumu miaka 45 wamezeeka , katangulia baba kustaafu anamwambia mkewe warudi kijijini , mkewe kagoma , mke akamwambja mumewe atangulie kijijini yeye aliyestaafu na miaka 60 mke akadai yeye ana miaka 53 akifikisha miaka 55 atastaafu kwa hiari atamfuata kijijini, mume akakasirika akaenda kijijini na alipofika akaoa mke mwingine huko kijijini , mke mjini kusikia akabaki anashangaa , usidharau mtu anapoomba ushauri , lakini asante kwa ushauri wako.
acha uwoga
Mada za kitoto hizi.
Nunua nawe gari
Unaishi kwa manungu na maneno ya watu...utaumia dunia ya watu hii...fanya yako duniani muda mchache achana na ya watu....inawezekana anaekuamnia ndo anammega mke wako...Asante sana kwa ushauri wako , mke wangu sio mapepe , ila nakubali kukaribisha jumuiya nyumbani unaweza kutafsiri kama maisha ya kiswahili na kukaribisha watu nyumbani kwako usiowajua vizuri nakubali ni hatari sema ni sababu ya maisha ya kiibada ambayo familia yangu tumejiwekea tangu zamani na wenyewe tunafurahia maisha yetu , nimeleta uzi sababu ni mara ya kwanza katika maisha yangu mtu kutishia maisha ya ndoa yangu , kuwa na imani hakukufanyi kutokuwa na wasiwasi , Mungu alimtokea Musa live wakaongea live , lakini Musa bado aliingiwa na woga pale Mungu alipomtaka akawanasue wanaisrael katika
mikono ya Farao, Yesu pamoja na kujua yeye ni mwana wa Mungu lakini ilipomlazimu apandishwe msalabani aliogopa , sembuse mmj mtu ajitatape huko anataka kunikomoa kwa kumchukua mke wangu ki ukweli sijakomaa sana kiimani mpaka niweze kuchukulia poa maana mimi
Ibada ni ziada tu baada ya kazi, naomba ushauri zaidi na asante kwa ushauri wako.
Umefunga mjadalaWhy mtu wa maombi uwe unasikiliza majungu? Kwa akili yako mtu atatangaza kabisa hadharani nimeuza nyumba ili nimtongoze Mke wa fulani?
Usikute zote ni hisia zako tu. Kama unamuamini Mke usingeanzisha thread. Unless unamjua mkeo alivyo mapepe..
Huo mtaa mnaishi Kiswahili sana. Mnahitaji reality TV mtuburudishe