Kanunua gari amtongoze mke wangu. Nimfanyeje?

Asante sana kwa ushauri , ila mimi naishi kiuhulasia sina hofu ukweli kama umenizidi kimaisha hata mbele ya mke wangu nitakusifia kwamba upo vizuri kimaisha , mke wangu ana karama ya kichungaji pia na mara kadhaa tumeshaalikwa kwa wazito zaidi ya huyu jirani yangu nayemtafakari tukawaombea na kote huko tukawa salama , sijawahi pata tishio kama hili mimi ambaye pia nina karama ya kitume nachoona , ni vita ya shetani na huduma yangu kupitia huyu jirani , nitasonga mbele sina hofu yoyote nachotafuta kwenu ni ushauri kwa usalama wa mke wangu na ndio usalama wa ndoa yangu pia , kwa sisi tulioamua kuishi maisha ya kihuduma tuko tofauti tunavyoondesha maisha.
Usijali Mimi nina pesa kuliko huyo Jirani yako,akimchukua Mkeo wwe nifahamishe,nitamnyanganya Mkeo na kumrudisha kwako!! Inaonekana Mkeo anapenda pesa sana!!
 
Hii ni vita kati ya Mungu ambae hayupo vs land cruiser!
MUNGU yupo, tatizo ni kwamba kuna mambo hutakiwi kuyapeleka kiroho.

Kitendo cha yeye kumwambia hili cruiser la jirani ni kwa ajili yako unatakiwa utafunwe hivyo tusali ili kunusuru ndoa ni kosa.

Alichokifanya ni kutengeneza curiosity kwa kiumbe dhaifu mkewe, sasa hivi kila akiliona hilo cruiser kuna mambo yatapita kichwani. Hapo bado hajafatwa.

Hii vita si ya kiroho. Ni ya mwili na nyama.
 
Tena nachoshukuru zaidi mke wangu nikipomwambia kwanza alikasirika akaniambia tukamshtaki , nilikataa ushauri wa kushtaki toka mke wangu maana nijua ukimshitaki atakana tu , mtaanza kuleta mashaidi mtapoteza muda pia niliona adui mkuu shetani atakakuwa ameshinda hila yake ya kuua huduma ya maombi inayoshamiri katika familia yangu , na tayari tumeanza kuaminiwa na baadhi ya majirani na mialiko midogo midogo ya kuhuduma na mpaka sasa mimi ndio nimekuwa
mstari wa mbele nikimwambia hili ni somo na kipimo Mungu anatupa atuone tutavuka vp ili Mungu atuvushe kwenda hatua ya juu zaidi kuhuduma , mke wangu amenielewa .
Wwe usiwe Mjinga Ngombe limejileta hilo,Kaa chini na Mkeo mpange deal mpige Mpunga, watu wengine sijui kwa nini hampendi kujua neema zenu ziliko!!
 
Na vipi endapo jirani yako alikua anapiga stories na hao wadau/majirani akawaambia kua anampango wa kuvuta land cruiser nao kwa mbwembwe kabisa land cruiser sijui Prado ilivyofika wakakwambia si unaona kaleta Prado alisema akiileta anakula mke wako. Wewe nae bila kutafakari umepata wenge kua mke wako anaenda Liwa rasmi.

Kwanini usifanyie uchunguzi hili suala upande wa majirani? Mtumishi, Angalia usije chonganishwa na maneno ya wananzengo!!!
 
Wakuu habari za majukumu,

Kwanza kabisa mnisamehe bure kwa kuleta mada badala ya kuongolea mambo ya kimaendeleo lakini kutokana na suala lenyewe kunikosesha amani nimeona nilileta humu, maana nimeona si busara kulipeleka kwenye vikao rasmi katika jamii ngazi husika.

Ni hivi, jirani yangu ambaye ni kama kaka kwangu maana amenizidi umri, anaishi nyumba ya tatu kutoka nyumbani kwangu. Ana mke na watoto nami nina mke na watoto. Huu mtaa wetu ni makazi mapya ndio tunaanza kuhamia wengi tuliokenga huku pembezoni ya jiji la Dar. Yeye alitangulia kuhamia kwenye nyumba yake kama miaka 14 iliyopita mimi nimeingia kwenye nyumba baada ya kukamilika miaka 6 iliyopita, tangu nimehamia huku wengi huku ni pilika pilika za maisha, asubuhi tuiamka ni kuwahi kazini au wengine kwenye biashara zao, watoto wengi huku wanakuja kuchukuliwa na mabasi ya shule zao wengine kama mimi nimekiwekea utaratibu wa mimi a mke wangu kuwapeleka na gari shulenj watoto na kuwapatia tukitoka kazini na turudi wote kama familia nyumbani.

Pale mtaani wengi maisha kama ya kizungu fulani hivi kila mmoja yupo bussy na familia yake lakini tunashirikia vizuri kama masuala ya ulinzi wa mtaa, tumeajiri walinzi kutoka kampuni ya ulinzi tunachangishana mtaani tunawalipa watulindie nyumba zetu na mali zetu.

Na mimi nashukuru Mungu nyumbani kwangu tunautaraatibu wa kufanya maombi kila siku jioni na jumamosi mpaka

Majirani wengi wamevutiwa na kuja nyumbani kushiriki ibada kwa makanisa yapo mbali hivyo hasa jumamosi kwangi panakuwa kama jumuiya hivi , wengi wakija wanakuja mume na mke wengine wanakuja na watoto wao, huyu jirani yangu yeye kama asipokija peke yake basi atakuja na watoto au mke wake anaweza kuja na watoto jamaa siku hiyo hatahudhuria ibada.

Baada ya muda, jioni moja baada ya kurudi kazini nimetoka kwa matembezi kidogo tukakuta njiani akiwa peke tukasalimiana kwa bashasha kama majirani, ghafla akaniomba kama nina mda kidogo ana jambo anataka kunishirikisha, nikamwambia karibu, tukaenda kuna ki pub pale mtaani, akaanza kunipongeza jinsi navyoishi vizuri na familia yangu anavutiwa sana ila yeye ana mgogoro mzito na mkewe na ndoa yake ipo ukingoni kuvunjika, ana dai mke wake ni mkorofi sana, amelazimisha awatunze wazee wake zaidi mpaka amewajengea nyumba huko kijijini bado haridhiki, wanaishi maisha ya gubu lisilo na kichwa wala miguu.

Mbaya zaidi akaniambia tangu mimi na famiia yangu imehamia hapa, mke wake amekuwa kila siku akimsimanga na kumshangaa yeye kwa nini aishi kwa amani na kuelewana, jamaa anasema mke wake anavutiwa na amani iliyopo katika familia yangu, sasa akamalizia kwa kuniomba ushauri siri yangu ni nini, nikamjibu kirahisi tu , ndoa hupangwa na Mungu na sisi ni mali ya Mungu, mume ni mali ya Mungu, mke ni mali ya Mungu watoto ni mali ya Mungu, vyote tulivyo navyo.

Ni mali ya Mungu ndio maana tukifa tunaacha vyote, hivyo nikamsihi ajiwekee utaratibu wa kumuomba Mungu aliyemsaidia kumpa hiyo familia nikamwambia ukimuomba Mungu kwa bidii , Mungu atafanya maajabu yake na nikamwambia, nipo tayari kutenga muda jioni wa kumzoesha jinsi ya kutengeneza ibada nyumbani, akashukuru tukaagana.

Cha ajabu baada ya kama wiki, jamaa akaanza kuninunia, na familia yake wote wakawa hawaji kwenye jumuiya, nilipofuatilia baada ya mwezi nikaambiwa na mairani wengine kwamba, mke wake aliondoka na watoto kamuacha jamaa kwenye nyumba peke yake, nilishtuka nikampigia simu jirani yangu huyu akaniambia ni kweli mke wake ameondoka na watoto ila akanijibu atanitafuta tutaongea zaidi.

Sasa habari nilizozipata pale mtaani , eti jamaa ananilalamikia mimi kwamba yeye anamasha mazuri kunishinda mimi inawakuwaje mimi nina amani na familia wakati nina kipato kidogo nyumba sio nzuri sana kama yake, gari yangu moja, yeye ana nyumba 4 gari mbili, hivyo atauza nyumba yake moja ipo Mabibo atanunua Land Cruiser ataanza kumtongoza mke wangu.

Na pesa itakayobaki akiuza nyumba ya Mabibo atatumia kumhonga mke wangu, na kwenda naye kwenye mahoteli, niliposikia hivyo, kama kawaida yangu, nikarud nyumbani nikamwambia mke wangu tusali nikamwambia yule jirani wa nyumba ya tatu ana nia mbaya na ndoa yetu, nikamwambia wazi mke wangu kwamba huyu jamaa kaapa kusambaratisha ndoa yetu, hivyo nikamwambia tuwe waangalifu na tuzidishe maombi. Nikajifungua chumbani na mke wangu tulisali kama nusu saa hivi na hilo tumeliongeza kwenye ratiba ya maomb yetu kifamilia.

SASA WAKUU NAOMBENI USHAURI WENU MAANA KWELI JAMAA WIKI ILIYOPITA NIMEONA GARI MPYA PRADO FULL TINTED IKITOKA NYUMBANI KWAKE, kwa upande wangu namshangaa jirani yangu kama nilichoaambiwa na ninachomshuhidia nikitarajia angetumia muda wake kushughulika na mkewe na watoto waliondoka kwake anataka kuhamishia hasira yake kubomoa ndoa yangu wakati mimi sina mashindano ya kimaisha na yeyote.

Najaribu kumpotezea nashindwa, kuanza kumsikilizia mke wangu ambaye nimesota naye tangu hatuna kitu mpaka leo tuna watoto, nyumba, kagari na vimiradi vya hapa na pale naona ni kumkoseha mke wangu maana watu hao weye majumba, maprado, matajiri, vigogo wapo wengi tu na mke wangu ni mtu anayejiheshimu, mzuri wa wastani si mbabaikaji na nikianza kumwekea wasiwasi ni kukaribisha matatizo ambayo hayajawahi kuwepo katika maisha yetu na mke wangu wa miaka 16 wa ndoa yetu.
Sema wewe ni dalali unamuuza mke kijanja pia hongera umepata mbinu ya kupiga hela kupitia mke hovyo kbs wewe useless.
 
Hizo ni changamoto za kimaisha na kwenye ndoa. Cha kufanya ni hivi
1. Zidisha kufanya ibada
2. Acha huo utaratibu wa kufanya maombi ya pamoja hiyo weekend kwa kuwakaribisha majirani hapo kwenu.
3. Ongeza mahaba kwa mkeo na ukaribu.
4. Ukiona jamaa anazidi basi unaweza hama hayo mazingira ila kuepusha shari.
5. Kitu cha mwisho usioneshe uwoga mbele ya mkeo. Fanya mkeo akuone wewe ndo una umuhimu zaidi kuliko yeye. Once akiona wewe una hofu ya kumpoteza basi anaweza kukupanda kichwani kirahi. Zingatia hilo sana.
 
1.Acha umbea, ulivyoona jamaa ajaja kwako, ukaanza kumfutilia tatizo nini, na katengana na mkewe. Wewe ilikuwa inakuhusu nini!?
2. Acha inferiority complex. Hujiamini, sababu jamaa ana gari ndo unakuwa na hofu. Kwani wakati mnaoana huyo mkeo halikuwa hatongozwi na wenye magari, au uko kazini o kwenye biashara?

4.Unapenda sana kusikiliza maneno, kama jamaa hajasema hayo maneno, ni majirani tu wametengeneza je?.
Kupenda maneno hulka za kina mama, wanaume tuda deal na fact mkuu.

Alafu kama hunampango wa kuwa mchungaji au nabii wa uongo, hiyo jumuiya nyumbani kwako yanini?. Na wakitoa sadaka unazipeleka wapi?
Ishi maisha yako na familia yako, acha kujilinganisha
 
Mke ana tabia gani kwanza????

Kuna wanawake wa aina tatu

1.Malaya

2.wenye msimamo haba

3.Sio malaya

Kama mkeo yupo kundi la aina moja au mbili basi una shida.

Ila kama yupo kundi namba tatu hamna shida nilichojifunza mimi kuhusu hawa wanwake ninkwamba kuna wanawake sio malaya jmhata mumewe akiwa na michepuko mia yeye sio malaya na wala sio asili yake

Kuna wanawake malaya hata uki jaribu kumpa kila kitu bado atatamani wanaume wengine na kuna wanawake inategemea na mnaishije,leo anatulia kesho kicheche kesho kutwa anatulia

Kikubwa umemwambia mkeo basi haina shida tabia yake ndo itaamua ndoa yako iweje Muombe Mungu amkinge na kulogwa mapenzi tu ila mwisho wa siku ni yeye mkeo ana tabia gani?????

Asili yake ni ipi?????
 
1.Acha umbea, ulivyoona jamaa ajaja kwako, ukaanza kumfutilia tatizo nini, na katengana na mkewe. Wewe ilikuwa inakuhusu nini!?
2. Acha inferiority complex. Hujiamini, sababu jamaa ana gari ndo unakuwa na hofu. Kwani wakati mnaoana huyo mkeo halikuwa hatongozwi na wenye magari, au uko kazini o kwenye biashara?

4.Unapenda sana kusikiliza maneno, kama jamaa hajasema hayo maneno, ni majirani tu wametengeneza je?.
Kupenda maneno hulka za kina mama, wanaume tuda deal na fact mkuu.

Alafu kama hunampango wa kuwa mchungaji au nabii wa uongo, hiyo jumuiya nyumbani kwako yanini?. Na wakitoa sadaka unazipeleka wapi?
Ishi maisha yako na familia yako, acha kujilinganisha
Duh! Kumbe Kusali Jumuia za Nyumbani kunakuwaga na Mpunga wa Sadaka!? Basi itakua Jirani anatowaga Sadaka ndefu sana,alafu Mke wa Jamaa anamsifiaga sana akiwa na Mumewe mpaka Mume anaumia ndani kwa ndani!!
 
😂😂, si ndo maana alianza kumuulizia baada ya kuona kondoo aliyenona kawa mtoro
 
Wakuu habari za majukumu,

Kwanza kabisa mnisamehe bure kwa kuleta mada badala ya kuongolea mambo ya kimaendeleo lakini kutokana na suala lenyewe kunikosesha amani nimeona nilileta humu, maana nimeona si busara kulipeleka kwenye vikao rasmi katika jamii ngazi husika.

Ni hivi, jirani yangu ambaye ni kama kaka kwangu maana amenizidi umri, anaishi nyumba ya tatu kutoka nyumbani kwangu. Ana mke na watoto nami nina mke na watoto. Huu mtaa wetu ni makazi mapya ndio tunaanza kuhamia wengi tuliokenga huku pembezoni ya jiji la Dar. Yeye alitangulia kuhamia kwenye nyumba yake kama miaka 14 iliyopita mimi nimeingia kwenye nyumba baada ya kukamilika miaka 6 iliyopita, tangu nimehamia huku wengi huku ni pilika pilika za maisha, asubuhi tuiamka ni kuwahi kazini au wengine kwenye biashara zao, watoto wengi huku wanakuja kuchukuliwa na mabasi ya shule zao wengine kama mimi nimekiwekea utaratibu wa mimi a mke wangu kuwapeleka na gari shulenj watoto na kuwapatia tukitoka kazini na turudi wote kama familia nyumbani.

Pale mtaani wengi maisha kama ya kizungu fulani hivi kila mmoja yupo bussy na familia yake lakini tunashirikia vizuri kama masuala ya ulinzi wa mtaa, tumeajiri walinzi kutoka kampuni ya ulinzi tunachangishana mtaani tunawalipa watulindie nyumba zetu na mali zetu.

Na mimi nashukuru Mungu nyumbani kwangu tunautaraatibu wa kufanya maombi kila siku jioni na jumamosi mpaka

Majirani wengi wamevutiwa na kuja nyumbani kushiriki ibada kwa makanisa yapo mbali hivyo hasa jumamosi kwangi panakuwa kama jumuiya hivi , wengi wakija wanakuja mume na mke wengine wanakuja na watoto wao, huyu jirani yangu yeye kama asipokija peke yake basi atakuja na watoto au mke wake anaweza kuja na watoto jamaa siku hiyo hatahudhuria ibada.

Baada ya muda, jioni moja baada ya kurudi kazini nimetoka kwa matembezi kidogo tukakuta njiani akiwa peke tukasalimiana kwa bashasha kama majirani, ghafla akaniomba kama nina mda kidogo ana jambo anataka kunishirikisha, nikamwambia karibu, tukaenda kuna ki pub pale mtaani, akaanza kunipongeza jinsi navyoishi vizuri na familia yangu anavutiwa sana ila yeye ana mgogoro mzito na mkewe na ndoa yake ipo ukingoni kuvunjika, ana dai mke wake ni mkorofi sana, amelazimisha awatunze wazee wake zaidi mpaka amewajengea nyumba huko kijijini bado haridhiki, wanaishi maisha ya gubu lisilo na kichwa wala miguu.

Mbaya zaidi akaniambia tangu mimi na famiia yangu imehamia hapa, mke wake amekuwa kila siku akimsimanga na kumshangaa yeye kwa nini aishi kwa amani na kuelewana, jamaa anasema mke wake anavutiwa na amani iliyopo katika familia yangu, sasa akamalizia kwa kuniomba ushauri siri yangu ni nini, nikamjibu kirahisi tu , ndoa hupangwa na Mungu na sisi ni mali ya Mungu, mume ni mali ya Mungu, mke ni mali ya Mungu watoto ni mali ya Mungu, vyote tulivyonavyo

Ni mali ya Mungu ndio maana tukifa tunaacha vyote, hivyo nikamsihi ajiwekee utaratibu wa kumuomba Mungu aliyemsaidia kumpa hiyo familia nikamwambia ukimuomba Mungu kwa bidii , Mungu atafanya maajabu yake na nikamwambia, nipo tayari kutenga muda jioni wa kumzoesha jinsi ya kutengeneza ibada nyumbani, akashukuru tukaagana.

Cha ajabu baada ya kama wiki, jamaa akaanza kuninunia, na familia yake wote wakawa hawaji kwenye jumuiya, nilipofuatilia baada ya mwezi nikaambiwa na mairani wengine kwamba, mke wake aliondoka na watoto kamuacha jamaa kwenye nyumba peke yake, nilishtuka nikampigia simu jirani yangu huyu akaniambia ni kweli mke wake ameondoka na watoto ila akanijibu atanitafuta tutaongea zaidi

Sasa habari nilizozipata pale mtaani , eti jamaa ananilalamikia mimi kwamba yeye anamasha mazuri kunishinda mimi inawakuwaje mimi nina amani na familia wakati nina kipato kidogo nyumba sio nzuri sana kama yake, gari yangu moja, yeye ana nyumba 4 gari mbili, hivyo atauza nyumba yake moja ipo Mabibo atanunua Land Cruiser ataanza kumtongoza mke wangu.

Na pesa itakayobaki akiuza nyumba ya Mabibo atatumia kumhonga mke wangu, na kwenda naye kwenye mahoteli, niliposikia hivyo, kama kawaida yangu, nikarud nyumbani nikamwambia mke wangu tusali nikamwambia yule jirani wa nyumba ya tatu ana nia mbaya na ndoa yetu, nikamwambia wazi mke wangu kwamba huyu jamaa kaapa kusambaratisha ndoa yetu, hivyo nikamwambia tuwe waangalifu na tuzidishe maombi. Nikajifungua chumbani na mke wangu tulisali kama nusu saa hivi na hilo tumeliongeza kwenye ratiba ya maomb yetu kifamilia.

SASA WAKUU NAOMBENI USHAURI WENU MAANA KWELI JAMAA WIKI ILIYOPITA NIMEONA GARI MPYA PRADO FULL TINTED IKITOKA NYUMBANI KWAKE, kwa upande wangu namshangaa jirani yangu kama nilichoaambiwa na ninachomshuhidia nikitarajia angetumia muda wake kushughulika na mkewe na watoto waliondoka kwake anataka kuhamishia hasira yake kubomoa ndoa yangu wakati mimi sina mashindano ya kimaisha na yeyote.

Najaribu kumpotezea nashindwa, kuanza kumsikilizia mke wangu ambaye nimesota naye tangu hatuna kitu mpaka leo tuna watoto, nyumba, kagari na vimiradi vya hapa na pale naona ni kumkoseha mke wangu maana watu hao weye majumba, maprado, matajiri, vigogo wapo wengi tu na mke wangu ni mtu anayejiheshimu, mzuri wa wastani si mbabaikaji na nikianza kumwekea wasiwasi ni kukaribisha matatizo ambayo hayajawahi kuwepo katika maisha yetu na mke wangu wa miaka 16 wa ndoa yetu.
Mkuu mbona swala jepesi hilo..

Wewe si umepeleka kesi kwa Mungu?na unamuamini? Basi acha atashughulika nayo.Unadhani unaweza kuoambana na za ya Mungu awezavyo?basi acha Mungu aamue maana wote nyinyi male yake.
 
Haaaa haaaa, bar mi nikaa wewe kunywa bia yako mi nitakugongesha cheers ya pepsi yangu halafu maisha yataendelea [emoji16]
Yanatokeaga maajabu mnajikuta mmelewa wote,yeye kalewa bia wew umelewa pepsi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
ulipo mpa siri ya mafanikio yako ndo ulipo haribu, nahisi anatumia udhaifu wako kukunyong`onyesha
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Huo mtaa mnaishi Kiswahili sana. Mnahitaji reality TV mtuburudishe
Nitakuwa wa kwanza kulipia King'amuzi husika. 😂 😂 😂 😂

Mwanamke akiwa mapepe wala halihitajiki gari masela kumbandua,jamaa anajua kaoa mke wa aina gani.
 
Wasiwasi wako ni nini? Je kuna mtu anaweza kutangaza mtaani kwamba anataka kufanya kitu kama hicho kweli? Jitafakari mzee baba nahisi kama una tatizo la kisaikolojia
 
Why mtu wa maombi uwe unasikiliza majungu? Kwa akili yako mtu atatangaza kabisa hadharani nimeuza nyumba ili nimtongoze Mke wa fulani?

Usikute zote ni hisia zako tu. Kama unamuamini Mke usingeanzisha thread. Unless unamjua mkeo alivyo mapepe..

Huo mtaa mnaishi Kiswahili sana. Mnahitaji reality TV mtuburudishe
Ametuaibisha wana maombi

Sent from my TECNO K9 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom