Kanunua gari amtongoze mke wangu. Nimfanyeje?

Steelomega

Senior Member
Aug 22, 2020
125
144
Wakuu habari za majukumu,

Kwanza kabisa mnisamehe bure kwa kuleta mada badala ya kuongolea mambo ya kimaendeleo lakini kutokana na suala lenyewe kunikosesha amani nimeona nilileta humu, maana nimeona si busara kulipeleka kwenye vikao rasmi katika jamii ngazi husika.

Ni hivi, jirani yangu ambaye ni kama kaka kwangu maana amenizidi umri, anaishi nyumba ya tatu kutoka nyumbani kwangu. Ana mke na watoto nami nina mke na watoto. Huu mtaa wetu ni makazi mapya ndio tunaanza kuhamia wengi tuliokenga huku pembezoni ya jiji la Dar. Yeye alitangulia kuhamia kwenye nyumba yake kama miaka 14 iliyopita mimi nimeingia kwenye nyumba baada ya kukamilika miaka 6 iliyopita, tangu nimehamia huku wengi huku ni pilika pilika za maisha, asubuhi tuiamka ni kuwahi kazini au wengine kwenye biashara zao, watoto wengi huku wanakuja kuchukuliwa na mabasi ya shule zao wengine kama mimi nimekiwekea utaratibu wa mimi a mke wangu kuwapeleka na gari shulenj watoto na kuwapatia tukitoka kazini na turudi wote kama familia nyumbani.

Pale mtaani wengi maisha kama ya kizungu fulani hivi kila mmoja yupo bussy na familia yake lakini tunashirikia vizuri kama masuala ya ulinzi wa mtaa, tumeajiri walinzi kutoka kampuni ya ulinzi tunachangishana mtaani tunawalipa watulindie nyumba zetu na mali zetu.

Na mimi nashukuru Mungu nyumbani kwangu tunautaraatibu wa kufanya maombi kila siku jioni na jumamosi mpaka

Majirani wengi wamevutiwa na kuja nyumbani kushiriki ibada kwa makanisa yapo mbali hivyo hasa jumamosi kwangi panakuwa kama jumuiya hivi , wengi wakija wanakuja mume na mke wengine wanakuja na watoto wao, huyu jirani yangu yeye kama asipokija peke yake basi atakuja na watoto au mke wake anaweza kuja na watoto jamaa siku hiyo hatahudhuria ibada.

Baada ya muda, jioni moja baada ya kurudi kazini nimetoka kwa matembezi kidogo tukakuta njiani akiwa peke tukasalimiana kwa bashasha kama majirani, ghafla akaniomba kama nina mda kidogo ana jambo anataka kunishirikisha, nikamwambia karibu, tukaenda kuna ki pub pale mtaani, akaanza kunipongeza jinsi navyoishi vizuri na familia yangu anavutiwa sana ila yeye ana mgogoro mzito na mkewe na ndoa yake ipo ukingoni kuvunjika, ana dai mke wake ni mkorofi sana, amelazimisha awatunze wazee wake zaidi mpaka amewajengea nyumba huko kijijini bado haridhiki, wanaishi maisha ya gubu lisilo na kichwa wala miguu.

Mbaya zaidi akaniambia tangu mimi na famiia yangu imehamia hapa, mke wake amekuwa kila siku akimsimanga na kumshangaa yeye kwa nini aishi kwa amani na kuelewana, jamaa anasema mke wake anavutiwa na amani iliyopo katika familia yangu, sasa akamalizia kwa kuniomba ushauri siri yangu ni nini, nikamjibu kirahisi tu , ndoa hupangwa na Mungu na sisi ni mali ya Mungu, mume ni mali ya Mungu, mke ni mali ya Mungu watoto ni mali ya Mungu, vyote tulivyonavyo

Ni mali ya Mungu ndio maana tukifa tunaacha vyote, hivyo nikamsihi ajiwekee utaratibu wa kumuomba Mungu aliyemsaidia kumpa hiyo familia nikamwambia ukimuomba Mungu kwa bidii , Mungu atafanya maajabu yake na nikamwambia, nipo tayari kutenga muda jioni wa kumzoesha jinsi ya kutengeneza ibada nyumbani, akashukuru tukaagana.

Cha ajabu baada ya kama wiki, jamaa akaanza kuninunia, na familia yake wote wakawa hawaji kwenye jumuiya, nilipofuatilia baada ya mwezi nikaambiwa na mairani wengine kwamba, mke wake aliondoka na watoto kamuacha jamaa kwenye nyumba peke yake, nilishtuka nikampigia simu jirani yangu huyu akaniambia ni kweli mke wake ameondoka na watoto ila akanijibu atanitafuta tutaongea zaidi

Sasa habari nilizozipata pale mtaani , eti jamaa ananilalamikia mimi kwamba yeye anamasha mazuri kunishinda mimi inawakuwaje mimi nina amani na familia wakati nina kipato kidogo nyumba sio nzuri sana kama yake, gari yangu moja, yeye ana nyumba 4 gari mbili, hivyo atauza nyumba yake moja ipo Mabibo atanunua Land Cruiser ataanza kumtongoza mke wangu.

Na pesa itakayobaki akiuza nyumba ya Mabibo atatumia kumhonga mke wangu, na kwenda naye kwenye mahoteli, niliposikia hivyo, kama kawaida yangu, nikarud nyumbani nikamwambia mke wangu tusali nikamwambia yule jirani wa nyumba ya tatu ana nia mbaya na ndoa yetu, nikamwambia wazi mke wangu kwamba huyu jamaa kaapa kusambaratisha ndoa yetu, hivyo nikamwambia tuwe waangalifu na tuzidishe maombi. Nikajifungua chumbani na mke wangu tulisali kama nusu saa hivi na hilo tumeliongeza kwenye ratiba ya maomb yetu kifamilia.

SASA WAKUU NAOMBENI USHAURI WENU MAANA KWELI JAMAA WIKI ILIYOPITA NIMEONA GARI MPYA PRADO FULL TINTED IKITOKA NYUMBANI KWAKE, kwa upande wangu namshangaa jirani yangu kama nilichoaambiwa na ninachomshuhidia nikitarajia angetumia muda wake kushughulika na mkewe na watoto waliondoka kwake anataka kuhamishia hasira yake kubomoa ndoa yangu wakati mimi sina mashindano ya kimaisha na yeyote.

Najaribu kumpotezea nashindwa, kuanza kumsikilizia mke wangu ambaye nimesota naye tangu hatuna kitu mpaka leo tuna watoto, nyumba, kagari na vimiradi vya hapa na pale naona ni kumkoseha mke wangu maana watu hao weye majumba, maprado, matajiri, vigogo wapo wengi tu na mke wangu ni mtu anayejiheshimu, mzuri wa wastani si mbabaikaji na nikianza kumwekea wasiwasi ni kukaribisha matatizo ambayo hayajawahi kuwepo katika maisha yetu na mke wangu wa miaka 16 wa ndoa yetu.
 
Why mtu wa maombi uwe unasikiliza majungu? Kwa akili yako mtu atatangaza kabisa hadharani nimeuza nyumba ili nimtongoze Mke wa fulani?

Usikute zote ni hisia zako tu. Kama unamuamini Mke usingeanzisha thread. Unless unamjua mkeo alivyo mapepe..

Huo mtaa mnaishi Kiswahili sana. Mnahitaji reality TV mtuburudishe
 
Why mtu wa maombi uwe unasikiliza majungu?
Kwa akili yako mtu atatangaza kabisa hadharani nimeuza nyumba ili nimtongoze Mke WA fulani??

Usikute zote ni hisia zako tu..
Kama unamuamini Mke usingeanzisha thread.
Unless unamjua mkeo alivyo mapepe..

Huo mtaa mnaishi Kiswahili sana..
Mnahitaji reality TV mtuburudishe
 
Why mtu wa maombi uwe unasikiliza majungu?
Kwa akili yako mtu atatangaza kabisa hadharani nimeuza nyumba ili nimtongoze Mke WA fulani??

Usikute zote ni hisia zako tu..
Kama unamuamini Mke usingeanzisha thread.
Unless unamjua mkeo alivyo mapepe..

Huo mtaa mnaishi Kiswahili sana..
Mnahitaji reality TV mtuburudishe

Asante sana kwa ushauri wako , mke wangu sio mapepe , ila nakubali kukaribisha jumuiya nyumbani unaweza kutafsiri kama maisha ya kiswahili na kukaribisha watu nyumbani kwako usiowajua vizuri nakubali ni hatari sema ni sababu ya maisha ya kiibada ambayo familia yangu tumejiwekea tangu zamani na wenyewe tunafurahia maisha yetu , nimeleta uzi sababu ni mara ya kwanza katika maisha yangu mtu kutishia maisha ya ndoa yangu , kuwa na imani hakukufanyi kutokuwa na wasiwasi , Mungu alimtokea Musa live wakaongea live , lakini Musa bado aliingiwa na woga pale Mungu alipomtaka akawanasue wanaisrael katika mikono ya Farao, Yesu pamoja na kujua yeye ni mwana wa Mungu lakini ilipomlazimu apandishwe msalabani aliogopa , sembuse mmj mtu ajitatape huko anataka kunikomoa kwa kumchukua mke wangu ki ukweli sijakomaa sana kiimani mpaka niweze kuchukulia poa maana mimi.

Ibada ni ziada tu baada ya kazi, naomba ushauri zaidi na asante kwa ushauri wako.
 
Jiamini mtoto wa kiume. Hapo umeshaonesha udhaifu kwa mkeo kitendo cha kumuonesha mke kuwa unaogopa akiibiwa ni tatizo tayari umeliunda mwenyewe.

Subiria show maana mke ataanza kuhisi you are less of a man. Ulitakiwa uwe Alpha, unaonesha uoga kwa mwanaume mwenzio mbele ya mkeo. Thats stupid!
 
........ Wasubiri Tuttyfrutty na Katoto kazuri waamke.

They are the best advisers so far!
 
We Una shida, Kwani unafikiri mke wako atongozwagi na watu wengine?

Yani una Miaka 16 ya ndoa una Kuwa na Mawazo hayo! We na jamaa wote ni shida
 
Jiamini mtoto wa kiume. Hapo umeshaonesha udhaifu kwa mkeo kitendo cha kumuonesha mke kuwa unaogopa akiibiwa ni tatizo tayari umeliunda mwenyewe.

Subiria show maana mke ataanza kuhisi you are less of a man. Ulitakiwa uwe Alpha, unaonesha uoga kwa mwanaume mwenzio mbele ya mkeo. Thats stupid!

Asante sana kwa ushauri , ila mimi naishi kiuhulasia sina hofu ukweli kama umenizidi kimaisha hata mbele ya mke wangu nitakusifia kwamba upo vizuri kimaisha , mke wangu ana karama ya kichungaji pia na mara kadhaa tumeshaalikwa kwa wazito zaidi ya huyu jirani yangu nayemtafakari tukawaombea na kote huko tukawa salama , sijawahi pata tishio kama hili mimi ambaye pia nina karama ya kitume nachoona , ni vita ya shetani na huduma yangu kupitia huyu jirani , nitasonga mbele sina hofu yoyote nachotafuta kwenu ni ushauri kwa usalama wa mke wangu na ndio usalama wa ndoa yangu pia , kwa sisi tulioamua kuishi maisha ya kihuduma tuko tofauti tunavyoondesha maisha.
 
We Una shida, Kwani unafikiri mke wako atongozwagi na watu wengine?

Yani una Miaka 16 ya ndoa una Kuwa na Mawazo hayo! We na jamaa wote ni shida

Miaka 16 ni mingi kweli lakini katika ndoa ni kama siku 1 tu kwani nilichojifunza kuhusu ndoa uwingi wa miaka ya ndoa si kigezo kikuu cha kupima uwezo wenu kuendesha ndoa , wapo wazee wanashindwa kuelewana baada ya maisha kustaafu kazi kuanza , nimeshuhudia ndoa ya wazee waliodumu miaka 45 wamezeeka , katangulia baba kustaafu anamwambia mkewe warudi kijijini , mkewe kagoma , mke akamwambja mumewe atangulie kijijini yeye aliyestaafu na miaka 60 mke akadai yeye ana miaka 53 akifikisha miaka 55 atastaafu kwa hiari atamfuata kijijini, mume akakasirika akaenda kijijini na alipofika akaoa mke mwingine huko kijijini , mke mjini kusikia akabaki anashangaa , usidharau mtu anapoomba ushauri , lakini asante kwa ushauri wako.
 
Steelomega acha mke agongwe Wewe! Hujui hiyo ni sunnah. Unataka ule wewe tuu kwani kinaisha. JIRANI kaza uzi gonga mzigo huoo. Malabuku.
 
Miaka 16 ni mingi kweli lakini katika ndoa ni kama siku 1 tu kwani nilichojifunza kuhusu ndoa uwingi wa miaka ya ndoa si kigezo kikuu cha kupima uwezo wenu kuendesha ndoa , wapo wazee wanashindwa kuelewana baada ya maisha kustaafu kazi kuanza , nimeshuhudia ndoa ya wazee waliodumu miaka 45 wamezeeka , katangulia baba kustaafu anamwambia mkewe warudi kijijini , mkewe kagoma , mke akamwambja mumewe atangulie kijijini yeye aliyestaafu na miaka 60 mke akadai yeye ana miaka 53 akifikisha miaka 55 atastaafu kwa hiari atamfuata kijijini, mume akakasirika akaenda kijijini na alipofika akaoa mke mwingine huko kijijini , mke mjini kusikia akabaki anashangaa , usidharau mtu anapoomba ushauri , lakini asante kwa ushauri wako.

Ndugu yangu katika maelezo yako umeeleza siri zote za kufanikiwa kwenye ndoa nazo ni:

1. Be a provider, mhudumie mke.
2. Mwombe Mungu sana sana!
3. Mpende na kumjali.
4. Mle vizuri na sio kibinafsi!

Baada ya hapo kama atachukuliwa ni tabia yake na hauna cha lufanya! Siwezi amini kama kuna mwanaume atanunua gari na kujitapa kwa ajili ya mke wa mtu, labda kichaa tu!
 
Ndugu yangu katika maelezo yako umeeleza siri zote za kufanikiwa kwenye ndoa nazo ni:

1. Be a provider, mhudumie mke.
2. Mwombe Mungu sana sana!
3. Mpende na kumjali.
4. Mle vizuri na sio kibinafsi!

Baada ya hapo kama atachukuliwa ni tabia yake na hauna cha lufanya! Siwezi amini kama kuna mwanaume atanunua gari na kujitapa kwa ajili ya mke wa mtu, labda kichaa tu!

Asante sana Mzee , Uttoh , umenishauri kiutu uzima haswaa , napokea ushauri wako wote, barikiwa sana Mzee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom