Kanuni za chama kutaka kulazimisha kuwa Sheria na Kanuni za Nchi ni jambo hatari

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Wakuu amani iwe nanyi! Kwa Siku za hivi karibuni kumeibuka tetesi mbalimbali zinazosema kuwa mgombea mwanachama na makamu mwenyekiti wa chadema bara ndugu Tundu Lisu amevunja moja ya kanuni muhimu ya sheria za tume ya uchaguzi. Kanuni hiyo ni kwambaTundu Lisu ameanza kampeni kabla ya wakati na kama atakutwa na hatia atazuiliwa kugombea kwa mujibu wa kanuni hiyo. Swali nini maana ya kampeni? Wapi na muda gani neno kampeni litatumika?

Utaratibu wa kuanza kampeni mapema ni utaratibu wa CCM na wala haujawahi kuwa sheria wala kanuni ya tume ya uchaguzi, CCM wana kanuni zao kadha wa kadha mfano
> Mgombea wao kutopingwa na mwanachama yoyote atakapoteuliwa kugombea.
> Wagombea kuachiana kwa msingi wa udini ngazi ya urais kwa muda wa miaka kumi kumi.
> Mgombea kutoanza kampeni mapema, (hapa wanajua wao sijui watia nia walikuwa wanaongea nini mbele ya wajumbe).
Hivyo hakuna kitu kinachoitwa kuanza kampeni kabla ya muda, huo ni utaratibu wao kama chama na wala si sheria.

Nawatakia dominika njema.
 
hata magu alianza kampeni mapema kwa kugawa mahela, kama vipi wakatwe wote tumchague mzee wa ubwabwa.
 
Back
Top Bottom