Kanisa la weusi lachomwa moto Mississippi, Marekani

amygdala

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,082
997
_92235257_1e2f2202-91ac-4576-af16-8e20f511f04b.jpg

Image copyright HOPEWELL BAPTIST CHURCH
Polisi katika jimbo la Marekani la Mississippi wanasema wanachunguza uhalifu wa chuki baada ya Kanisa linalotumiwa na watu weusi kuteketezwa na kisha kuchorwa maneno ya kusema: "Mpigie kura Trump".

Kanisa hilo linalopatikana eneo la Greenville lilijengwa miaka 111 iliyopita.

Msimamizi wa kituo cha zima Moto alisema kuwa moto katika Kanisa la Hopewell Missionary Baptist Church uliwashwa makusudi.

Shambulio hilo limetokea wiki moja kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika Jumanne wiki ijayo.

Maafisa wanasema ujumbe ulioandikwa kwenye jumba hilo ni wa kuzua hofu.

Meya wa Greenville, Mississippi amesema kisa hitendo hicho ni cha "chuki na woga" na s"shambulio la moja kwa moja dhidi ya uhuru wa watu kuabudu".

Kisa hicho kinawakumbusha watu kuhusu visa vya kuchomwa moto kwa makanisa ya watu weusi miaka ya 1950 na 1960, watu weusi waliokuwa wanapigania haki zao.

Maafisa wa FBI wakishirikiana na wachunguzi wa jinai wa jimbo la Mississippi kwa sasa wanaendelea na uchunguzi
Kanisa la weusi lachomwa moto Mississippi, Marekani - BBC Swahili
 
Hao ni watu wa bibi Clinton

Ni kweli mkuu, wanataka Black American wawashuku wafuasi wa TRUMP ili wampe kura Clinton wanacho sahau ni kwamba Blacks are not all that stupid wanajua lengo la kuchoma Kanisa lao lililenga nini.

Inaelejea Bi Clinton mambo ayamwendei vizuri licha ya kuwa supported na MSM nafikiri opinion polls zinazo mpendelea yeye ni za kuchonga tu, hali alisi kwenye grassroot ni tofauti kidogo ndiyo maana wana panick na kubuni mbinu za kujaribu kuonyesha kwamba Trump anashirikiana ba watu wabaguzi wa rangi.

Kama Clinton atashinda itakuwa kwa margin ndogo sana, actually latest news ni kwamba polls zinaonyesha wana run neck to neck - sasa hii sio habari nzuri kwa Hillary.

Binafsi naona kuna uwezekano mkubwa wa kurudia kuhesabu kura kwenye majimbo fulani - Hillary anaweza kuwa mbele kidogo kwenye popular votes, lakini akakosa Urais kama yaliyo mtokea Al Gore.
 
Nijibu chemshabongo hii, Nani aliyeplot mabomu ya Arusha: kanisani na kwenye mkutano wa chadema
mwiguluu atusaidie swali hili! ........(kesho mkienda kwenye mkutano wa chadema mtakufa)
 
Ukiangalia yanayoendelea marekani kuchomeana makanisani kukashifiana hofu ya kuiba kura ni wazi kuwa taifa hili kubwa kusiasa kiuchumi na kijeshi linaelekea kuanguka
 
Back
Top Bottom