Kanisa la wala nyasi, wengi wataka kujiunga

Kanisa la wala nyasi, wengi wataka kujiunga

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,957
attachment.php



BAADHI ya wananchi jijini Dar wamejitokeza na kuomba kujiunga na kanisa ambalo waumini wake wanakula nyasi.



attachment.php


Waumini wakila nyasi.
​
Kanisa hilo ambalo makao yake makuu ni Afrika Kusini linaloitwa Rabboni Centre Ministries gazeti hili liliandika katika toleo lake lililopita kuwa limeingia nchini na lipo maeneo ya Upanga jijini Dar.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili mara baada ya kusoma habari hiyo walisema wanatamani kujiunga.
"Mimi nataka kujiunga na kanisa hilo kwa sababu tunataka wokovu," alisema mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Amos.

attachment.php


Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Frida Mandade alisema ana hamu ya kujiunga na kanisa hilo kwa sababu zake binafsi.

Kanisa la Rabboni Centre Ministries lina makao yake makuu Pretoria nchini Afrika Kusini na linaongozwa na mtu anayejiita Mchungaji na Nabii Daniel Lesego ambaye alilianisha mwaka 2002.

attachment.php


Wakati wa mfungo waumini wa kanisa hilo wametajwa kuwa huwa wanaishia kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo kwa imani kuwa Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni. chanzo.GPL



 

Attachments

  • 1WALANYASI1.jpg
    1WALANYASI1.jpg
    67.4 KB · Views: 3,562
  • 2WALANYASI2.jpg
    2WALANYASI2.jpg
    70.9 KB · Views: 3,581
  • nyasi.jpg
    nyasi.jpg
    65.1 KB · Views: 3,596
  • walanyasi.jpg
    walanyasi.jpg
    68.6 KB · Views: 3,494
Last edited by a moderator:
Daah Jamanii!

Imani hizi zitatufanya tule hata visivyoliwa .
 
Haina sababu kujua kwann...hizi ni zama alizozitaja yesu.. na hawa ndio manabii wa uongo..
 
Halafu mimi nashindwa kuelewa mtu ktk msimamo wako, mtu mzima hasa, pengine umesomaa au hata hujasoma ila unajitambua unakubali kubadili......Wewe umezaliwa ktk Dini maybe Roman Catholic unaacha kwenda kanisa hili unaenda kwa Dr. Getrude, Au umezaliwa Ukiwa Lutheran unaenda ktk kanisa jipya ambalo ni la leo, au Muslim unabadili unakuwa Christian...Why usiwe na msimamo? Ulivyomdhaifu ktk nafsi yako ndipo Shetani na manabii wa uongo watakavyocheza na nafsi yako...
Simama pale ulipo, Umezaliwa hivyo, tenda mema hakuna dini inayoamrisha uovu, Mungu mwenyewe siku ya siku atajua akupe mema gani sababu ndiyo dini uliyozaliwa nayo...Acha kutangatanga ewe binadamu, Katika maandiko tulishaambiwa Manabii wa uongo watakuja, je unamjua huyo nabii wa uongo atakuwa nani?

Kutanga tanga huko kutakusababisha uangukie kwa manabii hawa




Haina sababu kujua kwann...hizi ni zama alizozitaja yesu.. na hawa ndio manabii wa uongo..
 
Haina sababu kujua kwann...hizi ni zama alizozitaja yesu.. na hawa ndio manabii wa uongo..

Hilo umelisema wewe!
Huyo Kiongozi wa kanisa hilo kasoma mpaka katafuna bibilia.

Akikutazama wewe na yeye atasema Wewe na Kanisa lako ndio manabii vizuka!

Siku hizi Ukristo ni Usanii tu.
Mimi mwenyewe niko ktkt ya mipango ya kufungua kanisa mjini!
Niko kwenye hatua za mwisho mwisho.
Na mimi baada ya miezi sita lzm nitembee na Helicopter.
 
Wakianza kubadili makaratasi kua fedha naomba mnijulishe nijiunge wadau maana fedha naitafuta sana ila kwa njia isiyo ya uhalifu.
 
Asiyejua maana haambiwi maana na itakuja siku nayo tutasikia kuna dini mpya hiyo nao ni ya kula mavi na tena nimesikia kuna dini mpya hiyo ni ya kuabudu kwake ni uchi kama tulivozaliwa na hii naona bado kufika na itafika tu kidogo kigogo au wana pima upepo wa wabongo uko vipi
 
Hilo umelisema wewe!
Huyo Kiongozi wa kanisa hilo kasoma mpaka katafuna bibilia.

Akikutazama wewe na yeye atasema Wewe na Kanisa lako ndio manabii vizuka!

Siku hizi Ukristo ni Usanii tu.
Mimi mwenyewe niko ktkt ya mipango ya kufungua kanisa mjini!
Niko kwenye hatua za mwisho mwisho.
Na mimi baada ya miezi sita lzm nitembee na Helicopter.

Ahaa kumbe mapovu yote hayo sababu ni kutembelea Chopper, duh!!!
 
Ahaa kumbe mapovu yote hayo sababu ni kutembelea Chopper, duh!!!

Sio mpaka nitaje kila kitu!
Nikidhapata Chopper na vingine vinafuata kwa wingi tu! Km vile mabangaloo na Wanakondoo wadogowadogo wakutafuna.

Na mimi ndio ntakuwa Mtoa pepo niliebarikiwa na yesu mia kwa mia!
 
Haloo chonde chonde ukiipta hiyo nijulishe na mm tukaanzishe ujasilia mali huko huko. Penye hela pana njia
Wakianza kubadili makaratasi kua fedha naomba mnijulishe nijiunge wadau maana fedha naitafuta sana ila kwa njia isiyo ya uhalifu.
 
mbona wanawake ni wengi sana hapo kwenye picha kuliko wanaume?
 
Ole wao wanyama waishio kwa kutegemea majani
 
Back
Top Bottom