Kanisa la anglikana kuna ulaji asikwambie m2

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,946
22,096
HUYU NI MCHUNGAJI WA 6 KWA TUHUMA ZA FEDHA KWENYE HILI KANISA
SASA UKIWA NA AKILI NZURIWAWEZA JUA MAKAO MAKUU WANAKULAJE KAMA WA CHINI WAKO HIVI

Wachungaji Anglikana wamkataa Askofu wao Send to a friend Monday, 14 March 2011 21:30 0diggsdigg

Frederick Katulanda, Mwanza
KANISA la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Victoria Nyanza limeingia katika mgogoro mwingine baada ya wachungaji 32 kutoa tamko la kumkataa Askofu Boniface Kwangu.
Katika tamko lao ambalo lilisomwa na Mchungaji Marco Iseke mbele ya wachungaji wenzake, viongozi hao wameamua kumkataa Askofu huyo kwa madai kwamba ameshindwa kuongoza, ikiwa ni pamoja na kutumia vibaya fedha na mali za kanisa, hivyo kumtaka akabidhi mamlaka ya ofisi hiyo kwa Askofu Mkuu.

Walidai kuwa kutokana na uongozi mbovu, amesababisha uadui na makundi ya kikabila na hivyo kulifanya kanisa kuwa na utengano kati ya wachungaji, waumini na wazee wa kanisa.
“Ametumia vibaya fedha za kanisa kwa kukarabati nyumba yake anayoishi kwa kiasi cha Sh60 milioni badala ya Sh20 milioni zilizoidhinishwa na kanisa na kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi miezi saba sasa bila ya sababu za msingi licha ya kuwa kanisa limekuwa likipokea Sh3.4 milioni kutoka katika mradi wao wa Shule ya Isamilo,” walidai katika tamko lao.

Aidha, walidai kuwa Askofu huyo amebadili katiba ya kanisa iliyopo na kutunga mpya kwa maslahi yake, huku wakiwahadaa wajumbe wa Sinodi kuwa ilitungwa na Jimbo.“Wamewahadaa waumini kuchangia Sh15 milioni za ununuzi wa gari la kanisa lakini gari hilo amelinunua kwa fedha Sh20 milioni kutoka katika mradi wetu wa Shule ya Isamilo na fedha za waumini hatujui kazitumia kwa nini,” walidai.
Akijibu madai hayo, Askofu Kwangu alisema hatambui tamko hilo na kusema kuwa, waliolitoa ni wale ambao walitimuliwa katika kanisa hilo... “Sijalisoma hilo tamko lao, lakini nitafuatilia na kujua chimbuko lao, nikishalisoma basi nitajiandaa kutoa tamko langu na mimi kwa sasa inatosha kusema tu kuwa silitambui.”

Awali, akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa wachungaji hao, Samuel Kahene alisema wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na kanisa lao kujikuta likiingia katika migogoro na kesi zake kufunguliwa polisi bila ya hatua zozote kuchukuliwa na Msajili wa Kanisa.
Alisema licha ya kuandika barua zaidi ya 10 kwa Msajili wa Kanisa, Katibu Mkuu wa Kanisa la Anglikana na Askofu Mkuu, hali imeendelea kuwa mbaya, huku Kanisa likizidi kuingia katika mgogoro na kwamba sasa baadhi ya waumini wameanza kujiengua na kujiunga na kanisa jipya la Kiinjili la Kianglikana Tanzania.

“Askofu wetu amekiuka Katiba ya Dayosisi ya Victoria Nyanza, Katiba ya Kanisa la Anglikana Tanzania na viapo vyake kwa Askofu Mkuu wa Kanisa. Ameshindwa kusimamia maadili ya kanisa hivyo tunamuomba ajiuzulu na aikabidhi dayosisi mikononi mwa Askofu Mkuu,” alieleza mwenyekiti huyo wa wachungaji.
 
Back
Top Bottom