Kanigeuka kisa kapata kazi

Kanigeuka kisa kapata kazi

Mr mgeni

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
1,222
Reaction score
812
Habari zenu wana jf,

Najuta ni kiherehere cha moyo wangu kukupenda,kukuthamini na jukujali.

Wana jf naombeni msaada,ni mpenzi wangu yapata 1&half year katika mahusiano ni binti ambaye tulifahamiana nae siku moja alipokuja na mama yake mdogo ofisini kwangu kupata huduma,

huyu mama yake mdogo ni mtu ninaefahamiana nae hivyo basi akaona haina budi kunitambulisha kwa mwanae nami nikaona ni vizuri kuanzia hapo binti yule alianza kunizoea na kuonesha dalili zote za kunitaka hata baadhi ya siku hufunga safari na kuja kunisalimia.

nami sikua na hiyana huwa sipendi kumkwaza mtu nikawa nampa ushirikiano tu mzur.

kutokana na ubize wa kazi yangu muda wa story huwa sina nikamwambia kama hutojali uwe unakuja saa 12jioni muda ambao nipo off ila sijui kama mama yako mdogo atakubali akasema hilo halina shida nikimwambia nakuja kwako hawezi kunikatalia kiukweli hilo jibu lake lilinipa ulakini!!

Basi jioni tukawa tunaenda sehemu ya utulivu tunapiga story sana tunapata chakula then tunaondoka tuliendelea hivyo kwa muda mrefu huwa anakuwa kama na kitu cha kutaka kuniambia lakini anashindwa kila usiku lazima anipigie simu na asubuhi lazima aniulize umeamkaje.

kutokana na tabia zake nzuri alizozionesha kwangu nikaona pengine Mungu ndo kanionesha mke mwema nikamtongoza japo sikutumia nguvu hata kidogo alitabasam na kufurahi nakumbuka alinikumbatia na kunipiga busu hadi nilihisi kuwewesuka kwa joto lake.

Nikawa namhudumia kila alichokitaka nilimpatia na alinipenda na kuniheshimu kama mume wake.

Nakumbuka aligombana na mama yake mdogo akawa kahamia kwa dada yake ni mbali kidogo huko nadhani maisha yalikuwa ya shida,alikuwa akinipigia simu "leo baby sijala"nikawa namsaidia akiugua namtumia pesa za matibabu,

SASA basi miezi miwili imepita kapata kazi basi ni dharau mwanzo mwisho simu hapigi,text hanitumii hata nikimtext baada ya masaa mawili ndo anareply tena shortly wiki tatu zimepita kanipigia simu anaumwa bila hiyana nikaenda kumuona na nilimpa kila kitu anachohitaji mgonjwa sikutaka maongezi nikaondoka zangu hadi leo sijawasiliana nae sababu ninahasira nae sana na ninataka nimfanyie kitu ambacho hatakisahau ili iwe fundisho au nyie wanajamvi mnanishauri nini?
 
Wanawake asilimia kubwa ndio walivyo usishangae kabisa. Hapo boss wake anakula vitu . Nina bro wangu yeye alimtafutia binti kazi kwenye kampuni anayofanya yeye baada ya huyo Dada kuwa amepigika mda mrefu sana skani kwa kihelehele cha kudhani ataonekana wa thamani kwa mrembo huyo na labda hatimaye atapewa papuchi akamuombea kazi kwa kuaminika kwake binti akapata kazi lol kitambo kidogo boss wao akapenda kitu kilikuwa chombo kweli sitanii mara gafla ukaribu ukafa kazi wamepewa kusimamia binti haonekani kasimama na boss wanapiga story full binti kitabasamu jamaa kakunja sura tu hana la kufanya wala nini. Kikubwa tuishi nao kwa akili sana usijiingize kichwa kichwa na wala usiwe na uchungu naye let her go wala usihesabu uliyomfanyia kwani fedha utafutwaaa. Pole sana utapata mwingine mzuri.
 
^^
Ni kweli inuma, Inatia hasira, Inaweka wazi ulidanganywa, Inavunja moyo....
Lakini ndiyo mapenzi, utaumia, utalia, utadanganywa. Kila mmoja hupitia haya. Nyakati kama hizo ziwapo mbele zako kuna njia moja nzuri. Nayo ni KUTOFANYA CHOCHOTE amini ataumia sana. Songa mbele ujue kuwa giza likizidi kumekaribia kupambazuka
^^
 
Hupaswi kulipa kisasi Mr unaingilia majukumu ya Mungu .Pia ni vyema ukasonga mbele hilo halikuwa fungu lako ni bora kajionesha mapema makucha yake na kila mtu achukue ustaarabu wake maana kila jambo linatokea kwasababu mwambie Mungu akupe kitu moyo wako unahitaji!
 
Kuna watu wanawahudumia wanawake mpaka unashangaa huyu hana ndugu au karogwa na mwishowe wanatibuana na kuachana songambele achana na mambo ya visasi unaweza kujuta baadae!
 
Hapo mr Mgeni unakosea usioange kulipiza kisasi!hilo ndilo pekee naweza kusema!
mkuu najiuliza maswali mengi sana na majibu sipati ndipo hasira zinaponipanda zaidi na ili moyo wangu uridhike nami nimtende kama alivyonitenda.
 
kapata aliyekuzidi kete huko ofisini sa we unajilazimishia ya nini... wanawake wengi mwache aendeleee... wewe si wa type yake shida ndo zilimfanya akupende.......ndioyo ile shukrani ya punda ni mateke.... ki digital umeshapikwa kisendal ... endelea na maisha yako kijana ....
 
Wanawake asilimia kubwa ndio walivyo usishangae kabisa. Hapo boss wake anakula vitu . Nina bro wangu yeye alimtafutia binti kazi kwenye kampuni anayofanya yeye baada ya huyo Dada kuwa amepigika mda mrefu sana skani kwa kihelehele cha kudhani ataonekana wa thamani kwa mrembo huyo na labda hatimaye atapewa papuchi akamuombea kazi kwa kuaminika kwake binti akapata kazi lol kitambo kidogo boss wao akapenda kitu kilikuwa chombo kweli sitanii mara gafla ukaribu ukafa kazi wamepewa kusimamia binti haonekani kasimama na boss wanapiga story full binti kitabasamu jamaa kakunja sura tu hana la kufanya wala nini. Kikubwa tuishi nao kwa akili sana usijiingize kichwa kichwa na wala usiwe na uchungu naye let her go wala usihesabu uliyomfanyia kwani fedha utafutwaaa. Pole sana utapata mwingine mzuri.
hapana mkuu nimemfanyia mambo mengi sana nikipiga hesabu harakaharaka yaani ni pesa ya kununua kiwanja kabisa sidhani kama moyo wangu utaridhika nikimuacha hivihivi
 
^^
Ni kweli inuma, Inatia hasira, Inaweka wazi ulidanganywa, Inavunja moyo....
Lakini ndiyo mapenzi, utaumia, utalia, utadanganywa. Kila mmoja hupitia haya. Nyakati kama hizo ziwapo mbele zako kuna njia moja nzuri. Nayo ni KUTOFANYA CHOCHOTE amini ataumia sana. Songa mbele ujue kuwa giza likizidi kumekaribia kupambazuka
^^
kwa alichonitenda inaniuma sana kusahau inahitaji msaada wa ziada na lengo langu nikukomesha dharau zake nina kila sababu ya kufanya hivyo
 
mkuu najiuliza maswali mengi sana na majibu sipati ndipo hasira zinaponipanda zaidi na ili moyo wangu uridhike nami nimtende kama alivyonitenda.

The best revenge is to let by gone be by gone!
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    38.9 KB · Views: 375
  • image.jpg
    image.jpg
    9.7 KB · Views: 331
kapata aliyekuzidi kete huko ofisini sa we unajilazimishia ya nini... wanawake wengi mwache aendeleee... wewe si wa type yake shida ndo zilimfanya akupende.......ndioyo ile shukrani ya punda ni mateke.... ki digital umeshapikwa kisendal ... endelea na maisha yako kijana ....
tatizo dharau zimepitiliza nikimuacha hivihivi ataniona mi zuzu
 
Pole sana me nafikili usilipize kisasi muachie mora yote hayo

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huwa wanasema awali ni awali tu. Wewe usifanye kitu chochote tena usimwonyeshe kuwa unahasria nae wekaa kimya sometime mjulie hali kama binadamu mwenzio na sio kama mpenzi ipo siku atakuja kukupigia magoti na kukuomba msamaha na hapo ndipo atakuwa kashachelewa. na ndio maana kuna msemo wasema pata pesa tujue tabia yako so ukimjua mtu jina huwezi muuliza waitwa nani!!
 
Mkuu we kausha tu.mwenyeww iko siku atajutia kwa alilofanya
wazo lako ni zuri mkuu ila naimani ungekuwa wewe kwa hili usingetaka ushauri ungetake action mojakwamoja kwa sababu inauma asikuambie mtu
 
Back
Top Bottom