Hiyo kitu sitakaa nifanye maisha yangu. Ni udhalilishajiKampigie magoti akurudie.
Kijana pole sana....mie yamenikuta hayo.niliumia sana tena sana....ila nikaamua kumtumbua jipu tu hamna namna.....ila kikubwa nilivyoona haeleweki nikaamua kumuwekea vikwazo vya kiuchumi...........muacha pasipo mjulisha mwanaume hamwaachi binti kwa maneno magumu.ila usiwe wa kukupeleka peleka ukamrudia....Mungu atakupa mwema,mpole na mwenye mapenzi ya dhati kwako......MUACHE AENDE ATAKUKUMBUKA SANA atapotekwa na vijana wa mwendokasi
akikutana na vijana wa mwendo kasi!!Unavunjaje uchumba; kwao unawaelezaje; mahari vpUna airisha ndoa tu mkuu hamna namna au unasajili mwingine yule wa mkopo
anyway......Mahari ni material things mkuu umepoteza vingapi till now kwao c tatizo u will revial the fact kwamba no marriage at allUnavunjaje uchumba; kwao unawaelezaje; mahari vp
Wewe unaoa wazazi wake au unamuoa yeye? Mwanamke akishasema hakupendi jua anamaanisha. Habari ya uchumba au kuogopa kwao utawaambiaje itagharimu maisha yako na utajuta kuoa. Kosea sehemu zingine lakini usikosee kuoa utajuta.Unavunjaje uchumba; kwao unawaelezaje; mahari vp
Miongoni mwa watu nawish niwaone ni huyu dada aisee.Achana naye kijana saka ela kwanza.
We unadhani suraiya sasa hivi hamtamani diamond na kujutia alivyomuacha
Duuh ukweli kabisa....ana jikaka huko kalizimikia ila halimpendi, mapenzi ptuuuuu!Nitausema ukweli utakuuma kijana mwenzangu/Mdogo wangu ni hivii elewa Huyo binti anajihusisha kimapenzi na mwanaume mwingine ,binti anampenda jamaa ila jamaa hampendi binti hizo turn around unazoziona ni pale anapozinguliwa na jamaa ,inabidi aje kupoza kwako believe me atarudi kuja kuomba msamaha tena kwako.
Nini cha kufanya sasa kama gentleman jikite kwenye vitu vya msingi katika maisha yako haswa masuala ya kiuchumi let her go, usikumbatie kaa la moto hata ukilazimisha hatokufaa maishani kwako , atakusumbua ukilazimisha kumuoa huwezi kuendelea kuishikilia kamba inayovutwa na gari/ng'ombe kisa tu kung'ang'ania kuiweka kwenye uelekeo unataka wakati kamba inakuumiza mikono yako.
Msikilize Daddy Tiger kwanza, kama hujamuelewa niulize.
Huyo ni mchizi star wa reggae dancehall Jamaica anaitwa Tiger Man, alikuwa anasema hataki mapenzi ya kitoto "No Puppy Love".Evelyn Salt na Madame B hawaelewi kiingereza, hebu watafsirie waelewe kilichoimbwa.
Ndugu zangu wanajamvi habari za asubuhi.
Nimekuja hapa kuandika uzi huu nikiomba ushauri nikihitaji faraja kutoka kwenu.
Mimi ni kijana miaka 25, mwenzangu huyu 21, nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita, mwenzangu kaishia form 4. Tumekuwa kwenye mahusiano karibu mwaka na nusu. Niseme kweli nilimpenda sana na yeye alinipenda. Nilijitolea sana kwa hali na mali kwa moyo wote kumsaidia katika maisha yake nilimpenda kwa moyo wote. Hali ilibadilika miezi kadhaa tangu tuingie kwenye mahusiano.
Mwenzangu akabadilika ghafla kaanza kunifanyia vituko majibu machafu nikimkosea tena kosa dogo laki binadamu, mwenzangu anachukulia nimefanya makusudi anakuwa mkali ugomvi hauishi wiki nzima. SMS akawa hajibu hata calls zangu hapokei.
Nikachunguza mabadiliko haya nikagundua mitandao ya kijamii ndio imemponza. Nikasema ngoja nipunguze mapenzi. Akajirudi akawa mpole akawa anasema ananipenda. Nikarudisha tena mapenz tena kwake baada ya muda akarudia ile tabia majibu machafu kiburi cha wazi wazi.
Nikaenda kwa mama yake akasema nimvumilie kwa kuwa bado hajakuwa kiakili nikavumilia nikampa onyo akajirekebisha wiki mbili tu baada ya hapo karudia tena tabia ile ile ya kuto nisikiliza anataka asikilizwe yeye tu nikimshauri jambo anajifanya mjuaji sana, kiburi nje nje.
Mimi sikuwahi msaliti na despite ya vituko anavyo nifanyia nilizidi kumwonyesha upendo, mimi nilimlipa kwa mema sijawahi kulipiza kisasi kwake, mpaka ndugu zake walikuwa wakisifia upendo wangu kwake. Lakini mwenzangu alikuwa haoni hilo.
Kila tulipo kosana alitaka tuachane hata kama kosa ni dogo anataka tuachane. Nikikubali anakaa week 1 moja anaomba msamaha na kuahidi kubadilika lakini baada ya hapo tena anarudi madudu.
Jana usiku nilimpigia simu kumsalimia kumjulia hali akakata simu, nikamtumia SMS hajajibu. Nilipompigia mara ya pili akapokea nikamuuliza kwanini anafanya hivyo akasema hajisikii kuwa na mimi nikamuuliza kwanini, ni kosa gani nimekutenda akasema hakuna ila hajisikii tu na ananitakia maisha mema na mahusiano yaishe.
Sasa wadau sijamtenda baya lolote lakini yeye kaamua hivinifanyaje?
Naomben ushauri?