Kaniacha bila sababu, moyo unaniuma

Kaniacha bila sababu, moyo unaniuma

Ndugu zangu wanajamvi habari za asubuhi.

Nimekuja hapa kuandika uzi huu nikiomba ushauri nikihitaji faraja kutoka kwenu.

Mimi ni kijana miaka 25, mwenzangu huyu 21, nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita, mwenzangu kaishia form 4. Tumekuwa kwenye mahusiano karibu mwaka na nusu. Niseme kweli nilimpenda sana na yeye alinipenda. Nilijitolea sana kwa hali na mali kwa moyo wote kumsaidia katika maisha yake nilimpenda kwa moyo wote. Hali ilibadilika miezi kadhaa tangu tuingie kwenye mahusiano.

Mwenzangu akabadilika ghafla kaanza kunifanyia vituko majibu machafu nikimkosea tena kosa dogo laki binadamu, mwenzangu anachukulia nimefanya makusudi anakuwa mkali ugomvi hauishi wiki nzima. SMS akawa hajibu hata calls zangu hapokei.

Nikachunguza mabadiliko haya nikagundua mitandao ya kijamii ndio imemponza. Nikasema ngoja nipunguze mapenzi. Akajirudi akawa mpole akawa anasema ananipenda. Nikarudisha tena mapenz tena kwake baada ya muda akarudia ile tabia majibu machafu kiburi cha wazi wazi.

Nikaenda kwa mama yake akasema nimvumilie kwa kuwa bado hajakuwa kiakili nikavumilia nikampa onyo akajirekebisha wiki mbili tu baada ya hapo karudia tena tabia ile ile ya kuto nisikiliza anataka asikilizwe yeye tu nikimshauri jambo anajifanya mjuaji sana, kiburi nje nje.

Mimi sikuwahi msaliti na despite ya vituko anavyo nifanyia nilizidi kumwonyesha upendo, mimi nilimlipa kwa mema sijawahi kulipiza kisasi kwake, mpaka ndugu zake walikuwa wakisifia upendo wangu kwake. Lakini mwenzangu alikuwa haoni hilo.

Kila tulipo kosana alitaka tuachane hata kama kosa ni dogo anataka tuachane. Nikikubali anakaa week 1 moja anaomba msamaha na kuahidi kubadilika lakini baada ya hapo tena anarudi madudu.

Jana usiku nilimpigia simu kumsalimia kumjulia hali akakata simu, nikamtumia SMS hajajibu. Nilipompigia mara ya pili akapokea nikamuuliza kwanini anafanya hivyo akasema hajisikii kuwa na mimi nikamuuliza kwanini, ni kosa gani nimekutenda akasema hakuna ila hajisikii tu na ananitakia maisha mema na mahusiano yaishe.

Sasa wadau sijamtenda baya lolote lakini yeye kaamua hivinifanyaje?

Naomben ushauri?
Kwa yale uloyatenda ukifikiri ni mazuri yeye aliyaona mabaya. Mfano umefanya naye tendo la ndoa kabla ya kuoana, huoni kwamba hilo ni baya? Yako mengi ulotenda ambayo ni mabaya sana. Usirudie kujidanganya kwamba mtu anakupenda.
 
Hahahaa hii mistari inakufaa
Kero na mashaaaka tele
Ugomvi kutwa nzimaaa
 
Ndugu zangu wanajamvi habari za asubuhi.

Nimekuja hapa kuandika uzi huu nikiomba ushauri nikihitaji faraja kutoka kwenu.

Mimi ni kijana miaka 25, mwenzangu huyu 21, nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita, mwenzangu kaishia form 4. Tumekuwa kwenye mahusiano karibu mwaka na nusu. Niseme kweli nilimpenda sana na yeye alinipenda. Nilijitolea sana kwa hali na mali kwa moyo wote kumsaidia katika maisha yake nilimpenda kwa moyo wote. Hali ilibadilika miezi kadhaa tangu tuingie kwenye mahusiano.

Mwenzangu akabadilika ghafla kaanza kunifanyia vituko majibu machafu nikimkosea tena kosa dogo laki binadamu, mwenzangu anachukulia nimefanya makusudi anakuwa mkali ugomvi hauishi wiki nzima. SMS akawa hajibu hata calls zangu hapokei.

Nikachunguza mabadiliko haya nikagundua mitandao ya kijamii ndio imemponza. Nikasema ngoja nipunguze mapenzi. Akajirudi akawa mpole akawa anasema ananipenda. Nikarudisha tena mapenz tena kwake baada ya muda akarudia ile tabia majibu machafu kiburi cha wazi wazi.

Nikaenda kwa mama yake akasema nimvumilie kwa kuwa bado hajakuwa kiakili nikavumilia nikampa onyo akajirekebisha wiki mbili tu baada ya hapo karudia tena tabia ile ile ya kuto nisikiliza anataka asikilizwe yeye tu nikimshauri jambo anajifanya mjuaji sana, kiburi nje nje.

Mimi sikuwahi msaliti na despite ya vituko anavyo nifanyia nilizidi kumwonyesha upendo, mimi nilimlipa kwa mema sijawahi kulipiza kisasi kwake, mpaka ndugu zake walikuwa wakisifia upendo wangu kwake. Lakini mwenzangu alikuwa haoni hilo.

Kila tulipo kosana alitaka tuachane hata kama kosa ni dogo anataka tuachane. Nikikubali anakaa week 1 moja anaomba msamaha na kuahidi kubadilika lakini baada ya hapo tena anarudi madudu.

Jana usiku nilimpigia simu kumsalimia kumjulia hali akakata simu, nikamtumia SMS hajajibu. Nilipompigia mara ya pili akapokea nikamuuliza kwanini anafanya hivyo akasema hajisikii kuwa na mimi nikamuuliza kwanini, ni kosa gani nimekutenda akasema hakuna ila hajisikii tu na ananitakia maisha mema na mahusiano yaishe.

Sasa wadau sijamtenda baya lolote lakini yeye kaamua hivinifanyaje?

Naomben ushauri?

jichunguze kwanza je mnaendana sio unalaumu tu labda huyo sio type yako.
 
Hata mm gash wangu wa kitambo aliniziungua kama ivo nkapiga chini,nkapata wa rangi yangu aaah safi,bro huyo kwa maoni yangu hakufai basi
 
Nilitaka nikupuuze tu kwa kuleta hii mada yako eti unaumia sana kisa umeacha na msichana wako.....kwani ulimuoa sasa anadai kugawana mali? Wewe inaonyesha uelewa wako katika masuala ya mahusiano ni level ya mbio za Kobe. Mzito kuelewa mambo.....pia huna maamuzi sijui utakuja kuwa baba wa namna gani baadaye. Acha kujilegeza mwanamke anapenda mwanaume IMARA sio wewe umemaliza college/university bado unashindwa kufanya decision jambo dogo kabisa.

Mwambie hako kasichana kako wewe ni shenzi kuanzia leo sitaki MAHUSIANO na wewe. Ukishindwa endelea kulialia.
 
aisee' ndugu" huyo mpenzi wako atakuumiza kichwa" inaonekana huyo mpenzi wako anampenda mwanaume mwingine zaidi ya wewe" na huyo mwanaume hampendi kabisa huyo mpenzi wako tena inaonekana akisha mtafuna anakua hana muda nae ndio maana mpenzi wako ukimchunia anarudia kukuomba msamaha" lakini yule jamaa akirudisha tena mawasiliano kwa mpenzi wako kwa sababu ya kumaliza haja yake ya mwili demu wako akua jeuri" tahadhari ukiendelea kum'nga'ngania utakuja kupandikiziwa mimba ndio utachanganyikiwa zaidi kuliko sasa" ushuri wangu ni wewe kuachanae kabisa" siku moja akili yako itazoea na utamuona wa kawaida kama una nafasi ya kufanya kazi za nguvu zifanye ili kuuchosha mwili na ukifika home we' ni usingizi tu' asubui ukiamka hivyo hivyo akili itazoea na kisha ataondoka mawazoni kwako!
 
Poleeee mkuu kwan kupendapenda ndio nn mkuu mind ur honourable time and happy life kwan yye nan til akuendeshe kama gari bovu au wwe story mingiii practical - ve
 
Ushaniudhi... Umesomea nini na umesoma wap??
Kuna mambo mengi sana ya kufanya japo mapenzi yapo ila sio kwa style hii!

FYI, statistics zinaonesha kua wanawake wako/ wanaweza kua zaid mara 3 ya wanaume.
Wakwako yupo somewhere waiting for u... mimi pia namsubiria wakwanguu maana sitaki ujinga tenaa
 
Huyo hakufai na inawezekana kunajamaa mwingine yeye anayemkubali zaidii kuliko ww tafuta mwingine utampata tu na huyo utamsaahau kabisa
 
Ndugu zangu.. nimeongea nae leo mchana. Kaniambia kosa langu ni kwa sababu nilimuuzi jana ucku wakati nilipomuuliza kwa nini hakupokea simu wala kujibu sms yangu? Eti ndio kosa... langu.

Alafu.. yeye kaniambia kuwa mimi huwa namletea stress sana. Nikijiangalia ni stress gani sizioni. sion sababu.. sioni chanzo ya mimi kumletea stress...

Nimekuwa nikimsaidia sana.. kwenye shughuli zake.. mpaka ndugu zake wanashangaa..
mapenz yangu.. misaada yangu leo inaitwa stress...?

Huyu si alikuwa ananitafutia tu sababu ya kuniacha?
 
Bora alivyokuambia ukweli kuliko aendelee kukupotezea muda.
Hata hivo vituko anafanya ili umuache lakini kwakuwa unampenda unavumilia na muda mwingine yawezekana anakuonea huruma ndo mana anakuomba msamaha.
Anakwambia hajisikii kuwa na wewe lakini kunasababu zinazomfanya awe hivo ila tu hataki au hawezi kukwambia kwakua utajisikia vibaya sana.
Muache afanye anavyotaka na wewe kuwa bizzy na shughyli zako wala usimtafute.
Akili zikimrudia atakutafuta wakati huo keshachelewa na wewe umemove on.
Feitty.. yaani inauma unampendanmtu alafu anakuona kikaragosi.
Ila basi yameshatokea.. labda Mungu kaniepushia tatizo
 
Back
Top Bottom