Kaniacha bila sababu, moyo unaniuma

Kaniacha bila sababu, moyo unaniuma

Ushauri wangu kwako mhimu huyo kama si tabia yake ya asili nafikiri kwa muda wote tabia yake ulishaijua na kama si hivyo ujue huyo alishapata mshika dau mwingine hapo analinganisha anachopata upande wa pili na kwako!
 
Kiujumla hilo sio fungu lako kaa utulie ungoje watakuja wenyewe
 
Ndugu zangu wanajamvi habari za asubuhi.

Nimekuja hapa kuandika uzi huu nikiomba ushauri nikihitaji faraja kutoka kwenu.

Mimi ni kijana miaka 25, mwenzangu huyu 21, nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita, mwenzangu kaishia form 4. Tumekuwa kwenye mahusiano karibu mwaka na nusu. Niseme kweli nilimpenda sana na yeye alinipenda. Nilijitolea sana kwa hali na mali kwa moyo wote kumsaidia katika maisha yake nilimpenda kwa moyo wote. Hali ilibadilika miezi kadhaa tangu tuingie kwenye mahusiano.

Mwenzangu akabadilika ghafla kaanza kunifanyia vituko majibu machafu nikimkosea tena kosa dogo laki binadamu, mwenzangu anachukulia nimefanya makusudi anakuwa mkali ugomvi hauishi wiki nzima. SMS akawa hajibu hata calls zangu hapokei.

Nikachunguza mabadiliko haya nikagundua mitandao ya kijamii ndio imemponza. Nikasema ngoja nipunguze mapenzi. Akajirudi akawa mpole akawa anasema ananipenda. Nikarudisha tena mapenz tena kwake baada ya muda akarudia ile tabia majibu machafu kiburi cha wazi wazi.

Nikaenda kwa mama yake akasema nimvumilie kwa kuwa bado hajakuwa kiakili nikavumilia nikampa onyo akajirekebisha wiki mbili tu baada ya hapo karudia tena tabia ile ile ya kuto nisikiliza anataka asikilizwe yeye tu nikimshauri jambo anajifanya mjuaji sana, kiburi nje nje.

Mimi sikuwahi msaliti na despite ya vituko anavyo nifanyia nilizidi kumwonyesha upendo, mimi nilimlipa kwa mema sijawahi kulipiza kisasi kwake, mpaka ndugu zake walikuwa wakisifia upendo wangu kwake. Lakini mwenzangu alikuwa haoni hilo.

Kila tulipo kosana alitaka tuachane hata kama kosa ni dogo anataka tuachane. Nikikubali anakaa week 1 moja anaomba msamaha na kuahidi kubadilika lakini baada ya hapo tena anarudi madudu.

Jana usiku nilimpigia simu kumsalimia kumjulia hali akakata simu, nikamtumia SMS hajajibu. Nilipompigia mara ya pili akapokea nikamuuliza kwanini anafanya hivyo akasema hajisikii kuwa na mimi nikamuuliza kwanini, ni kosa gani nimekutenda akasema hakuna ila hajisikii tu na ananitakia maisha mema na mahusiano yaishe.

Sasa wadau sijamtenda baya lolote lakini yeye kaamua hivinifanyaje?

Naomben ushauri?
Umezidiwa kete na wajanja,

Tafuta wa darasa la saba kama wa 4 kakushinda
 
Nimefuata ushauri wenu wakuu.. maa dah.. mtu akioendwa anazingua... full malalamiko. Bora nikomae na maisha yangu tu.
 
hivi mbna unakua kama gari la mkaa wiki moja gereji week moja barabaran..... embu achana nae umri huo unasumbuliwa na kibinti cha early 20's........... na yet hujui nn cha kufanya.
sifa ya mwanaume ni kua na msimamo katika maamuzi kuwa hvyo bas.
Nimecheka kweli kweli comment yako!!
 
'Atakuwa ameanza kunywa mirinda nyeusi.."chunguza vizuri
 
Huyu msela asaiv ana miaka kati ya 30 au 30 na 1 (30-31yrs) kama sijakosea na binti kwa sasa ndo ana umri kama wa jamaa wa wakati huo yaani kati ya 24 - 25yrs kidogo kiakili amekomaa..


Sasa sijui walifikia wapi, sijui jamaa alipataga mwingine basi natumai wako pamoja huenda ndo mke wake wa sasa, na binti navyohisi kama aliachwa na jamaa basi atakua alipata mjuba na alizalishwa na either ana mtoto/watoto tayari..
 
Back
Top Bottom