Hakuna pesa inayotosha ndio maana maisha yetu ni ya kutafuta pesa mpaka tunakufa.
Leo ni siku ya 53 tangu hayati mwendazake atwaliwe kutoka maisha haya... Wafaidikaji wa utawala wake wakajipa kandarasi ya kulinda 'mazuri' yake huku wakipambana mitandaoni na kila aliyejaribu kukosoa utawala wa hayati mwendazake. Hii si kandarasi ndogo hata kidogo.
Kuweza kuiendesha kwa mafanikio mpaka ufikie lengo kunahitaji oganaizesheni kubwa ya pamoja, rasilimali watu, na vyanzo vya uhakika vya mapato.
Vikundi tarajiwa kwa maana ya rasilimali watu vilivyotegemewa kuifanya hii kandarasi ni LMB7, MATAGA na kikundi kidogo cha SKM GANG! Lakini kwa bahati mbaya kabisa watatu hawa wakakosa ushirikiano na kuanza kuhitilafiana na kutuhumiana wao kwa wao
Ili uweze kuendesha kampeni ya mafanikio .. Ukiachana na mpango kazi wa mradi wako ... Pesa za kuwezesha na watu wa kufanya kazi ni muhimu sana.
Na hizo pesa lazima zipatikane toka chanzo cha uhakika na endelevu
Mwanzoni baada tu ya kifo mradi ulienda vizuri sana, wafanya kampeni za kulinda legacy walilipwa bila kigugumizi na walipaji walitoa bila kusita....lakini kadiri muda ulivyosogea ukweli mchungu na wa kuogofya sana ulianza kujifunua. Kwamba malipo yanayotoka hayana monitoring ya kueleweka
Kwamba kila sent itokayo hakuna replacement yake tena kwakuwa mfadhili mkuu hayupo tena.
Kwamba malipo yanatofautiana kwa watu wanaofanya kazi moja..kuna wanaopata zaidi na kuna wanaopata kiduchu. Kwamba uhitaji wa cash ni mkubwa sana kuliko matarajio na hakuna vyanzo vya mapato.
Chini ya siku 100 tayari wanapumulia mashine. Kilichobaki sasa hakuna umoja wala kandarasi ya kulinda legacy tena.. Kila mtu na lwake! Wanachoangalia sasa ni maslahi binafsi.. Kuliko kushupaa kulinda legacy ya mfu Yenye gharama kubwa ni heri kulinda chochote alichovuna toka utawala wa hayati mwendazake.
Ni wazi kuna baadhi yao ni wafaidikaji wakubwa wa miradi binafsi ya marehemu waliopewa kuisimamia, ambayo kimsingi ni ya familia ya mwendazake! Si ajabu kati yao kuna walio busy kutaka kuitaifisha na kuigeuza ya kwao.. Na hapa ndio wanachimbana na kutofautiana.
Joto la kulinda legacy linapoa kwa kasi ya aina yake na ikigonga siku ya 100 litakuwa tayari baridi kabisa... Tena ile YABISI... Halafu tutaenda kuizika legacy kwenye makaburi ya sahau.
JPM alikufanya nini??🤣🤣🤣🤣
Trust me, maana ni rahisi kabisa akasahaulika na wala usimwandike, fact kwamba unamwandika unamkumbuka aidha alibana mianya ya kula kwako au alikuadhibu,
kama ulikuwa clean kwa JPM ...hakuwa na shida
Furaha yako ni kifo?? wewe, watoto wako mke wako watakufa tu....tena kimya kimya
Soon utakosa hoja humu maana mama atakuwa wa moto na wewe utakuwa wa vuguvugu, jiandae kupiga U turn kubwa sana ya maisha humu...maana una wafuasi wengi wazuri na watakupa likes mpaka unakufa,
Ila as a man nje ya jukwaa hili huna uwezo wowote, hauna uwezo wa ku impact kitu, kubadilisha system, hauna uwezo wa kujiandaa kuwa rais, waziri, mbunge, diwani...nje ya hapa...ni mpiga soga exactly kama vijiwe vya karata na bao magomeni!! yes you are
Hiyo kandarasi hautaweza kuizuia mtaani, acha kujipa moyo, hauna nguvu ya kuwashinda watanzania ambao hata leo hii wanamkumbuka na kumtaja JPM...nenda utube, nenda insta, nenda kila mahali...he is there to stay for long long time and You are the witness...utaandika habari za JPM kama faraja yako ya kujifariji alichokufanya
Utamkumbuka JPM ukiwa kanisani, utamwota, utatafuta kila title ya kumdhalilisha, ili mradi tu YUKO akilini mwako na anaishi sana tu
Utawatafuta wenzako wawili watatu mtamsema vibaya, mtajipa moyo na faraja kudhalilisha wengine...unajua kwa nini, hamna la kuandika, hamna mnachoona, mmekata tamaa, desperation iko wazi kuwa hata mama Samia, hauna la kumfanya wala kumkosoa hata akikupiga kidole cha jichoni kwa sababu...your brain is tuned mbaya wako ni JPM!!!!!!!?
Hautakuja kumsema Samia vibaya, simply kwa sababu ushakuwa kilema wa chuki kwa JPM...in so doing utakosa weledi wa kusimama kama mtu mwenye akili timamu, ila kama zombie ambae ashaharibiwa na sumu
Utadhania mwendazake kapotea, utapita mtaani mwakani utakuta wanamsifia mahali, utakuta mtu kaanzisha thread humu kamkumbuka...utafanya nini? Utaumia sana sana sana, ili kujipa amani na moyoni...utaanzisha thread ya kumwandika vibaya...wenye akili na kifungo kama chako mtapeana moyo weee..
He is there to stay, wewe ni shahidi wa kwanza, kama hatatoka akilini mwako kwa mabaya, yuko ambaye hatamtoka kwa mazuri...na sio lazima uwaone mitandaoni what a stupid mind?
Mimi nitampenda JPM mpaka kesho, na povu, vijembe, matusi, dhihaka ruksa...ila ndio hivyo na mimi ni kilema kama wewe!!!🤣💯