magufuli oyeeee soma hapa AJALI iliyotokea eneo la Changarawe, Mafinga
Jumatano iliyopita, bado ndiyo habari yenye
kuendelea kujadiliwa kila kona ya Mkoa wa Mbeya.
Ni ajali iliyoua watu 50, leo hii ni vilio kila kona ya Jiji
la Mbeya. Ni wazi itaendelea kubaki katika
kumbukumbu za wakazi wa mikoa ya Mbeya, Iringa
na Njombe kwa miaka mingi ijayo.
Watu wengi waliofariki katika ajali hiyo ni wakazi wa
Jiji la Mbeya, lakini wenye kutoka maeneo
mbalimbali ya mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya
yenyewe.
Siku za Ijumaa, Jumamosi na hadi Jumapili zilikuwa
na pilikapilika za kusafirisha miili ya marehemu na
mazishi, kutoka Mafinga hadi Mbeya na baadaye
kwenye maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo kwa ajili
ya mazishi.
Nini hasa sababu ya ajali?
Ni swali lenye kuumiza vichwa vya wakazi wa Jiji
la Mbeya na ndilo lililotawala mazungumzo ya
wakazi wa jiji hilo, tangu kutokea kwa ajali hiyo.
Mengi yamezungumzwa kuhusiana na ajali hiyo,
wapo wenye kuamini kuwa imesababishwa na
ushirikina, wakiamini kuwa ni ajali iliyohusishwa na
utoaji kafara. Hawa yawezekana ni kutokana na
kutoamini kwamba yawezekana kutokea kwa ajali
kama ile, yenye kuteketeza watu wengi kwa wakati
mmoja kutokea.
Lakini zipo sababu za kisayansi zenye kutumika
kuielezea ajali ile, zikiwemo mwendo kasi, ubovu wa
barabara na uzembe. Hata hivyo, sababu kuu
iliyozungumzwa zaidi ni ubovu wa barabara,
kwamba ajali ilisababishwa na dereva wa lori
alipolazimika kulikwepa shimo kwenye eneo hilo la
barabara.
Miongoni mwa wenye kusimamia sababu ya ubovu
wa barabara ni pamoja na Kamanda wa Jeshi la
Polisi mkoani Iringa, Ramadhan Mungi, ambaye
alinukuliwa akisema: Hapa tusitafute mchawi,
katika hii ajali chanzo kikubwa ni ubovu wa
barabara, hivyo ni jukumu la mamlaka husika
kurekebisha.