Kanali ahukumiwa kunyongwa,Congo Dr

Kanali ahukumiwa kunyongwa,Congo Dr

Shy land

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
6,245
Reaction score
2,856
140103161553_drc_beni_624x351_afp.jpg

Waaandamaji wakipinga kuuawa kwa Kanal Ndala

10385377_795789023816038_1524887553296697821_n.jpg
Mahakama ya kijeshi Mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo imemhukumu kifo Kanali Birocho Nzanzu baada ya kubainika na makosa ya kutaka kumuua afisa wa jeshi la nchi hiyo aliyekuwa mstari wa mbele kutokomeza wapiganaji wa M23.

Kanal Mamadou Ndala anayedaiwa kuuawa na njama za Kanal Birocho Nzanzu

Afisa anayedaiwa kupangiwa njama za kuuawa ni Mamadou Ndala mabaye kwa kiasi kikubwa aliamini katika vita dhidi ya kundi hilo la wapiganaji na ambaye aliuawa mwezi januari mwaka huu. Hata hivyo hukumu hiyo imetolewa kwa watuhumiwa nane ambapo kati ya hao mmoja ndiye Kanali Ndala aliyehukumiwa kifo. Mahakama imebainisha kuwa Kanali Nzanzu amekuwa akitumiwa na waasi wa ADF kutoka Uganda kuandaa mauaji.

CHANZO:BBC
 
Duh! wewe uko shinyanga halafu kiingereza hujui sasa hizi habari unatoa wapi bro? maana hata kiswahili hujui,tehehehehehehe,nilikuwa nakutania tu mkuu.
 
Pitia habr ulipoixoma then ilete tena coz ni nzur bt lugha yako haielewek
 
Jf imejaa mapopompokwelii kiswahi chakawaida mnaitaji dictionary loh
 
Duu chamsing ni kuelewa tu zingine mbwembwe tu
 
Mahakama ya Kijeshi mjini Beni Mashariki mwa Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo imemhukumu Kanali Birocho Kossi adhabu ya kifo baada ya kubainika kuhusika na mauaji ya Kanali Mamadou Ndala mapema mwaka huu.

Uamuzi katika kesi ya watuhumiwa wa mauaji ya Kanali Mamadou Ndala umetolewa jana Jumatatu, Novemba 17.

Kanali Mamadou Ndala aliyeuawa Januari 2 mwaka 2014, baada ya gari aliyokuwemo kupigwa roketi na kuteketea kwa moto, anachukuliwa kama mmoja wa mashujaa wa vita dhidi ya waasi wa M23.

Watuhumiwa zaidi ya ishirini walifunguliwa mashta, ikiwa ni pamoja na raia wanane, maafisa wanne waandamizi wa jeshi la Congo na walinzi wawili wa zamani wa Kanali Mamadou Ndala.

Mahakama hiyo pia imewahukumu watu wengine 20 na tayari wamepelekwa Kinshasa.

Kesi hiyo ambayo ilidumu zaidi ya mwezi mmoja, ina washtakiwa 23. Kwa muda wa wiki sita Ofisi ya mashtaka ilikabiliwa na wakati mgumu ili iweze kutoa vithibitiho na ushahidi wa kutosha, kwa kuonesha iwapo watuhumiwa hao walishiriki moja kwa moja katika mauaji ya Mamadou Ndala Moustafa.

Katika hatua ya mwisho ya kesi hiyo, mtuhumiwa mmoja tu ndiye alituhumiwa moja kwa moja kuandaa shambulio hilo Januari 2 mwaka 2014. Kanali Birocho Nzanzu alinyooshewa kidole na mmoja wa walinzi wake pamoja na shahidi mmoja aliye kuwa mpiganaji wa waasi wa zamani wa M23 kwamba alikua kati ya jeshi la Congo na waasi wa Uganda ADF-Nalu kwa kuandaa shambulizi dhidi Mamadou Ndala Moustafa.

Wakati hayo yakijiri vituo vitano vya redio katika miji ya Beni na Butembo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimefungwa, kwa amri ya serikali ikivituhumu kuchangia kufanya uchochezi.

Kwa upande wake shirika la kutetea haki za waandishi wa habari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la “Journalistes en Danger” - JED limeelezea wasiwasi wake kuhusu hatua ya serikali ya nchi hiyo kuvifungia vituo vitano vya redio Mashariki mwa DRC ikiwa ni pamoja na vituo vya mji wa Beni na Butembo.

Aidha, shirika hilo limeiitaka serikali kuruhusu uchunguzi huru ufanyike kubaini tuhuma kuwa vituo hivyo vimechangia kufanya uchochezi, wakati vingine vilivyotajwa ni sasa zaidi ya mwaka mmoja havifanyi kazi na kusisitiza kuwa hatua iliyochukuliwa imefanyika kwa malengo maalum.

Wito kama huo pia umetolewa na raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoishi nchini Canada, wametaka uchunguzi huru kufanyika kuhusu kufungwa kwa vituo vitano vya redio mjini Beni na Butembo, kwa madai kuwa vinashirikiana na makundi ya waasi yanayosababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Hayo yakijiri ripoti mpya ya shirika la kimataifa la kutetea haki za bina damu human Right Watch imeituhumu polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwaua watu 51 wengi wao wakiwa ni vijana na wengine 33 wamlitoweka wakati wa operesheni kababmbe iliyoendeshwa na polisi dhidi ya uhuni katika mmji wa kinshasa tangu mwezi Novemba mwaka 2013 hadi Februari mwaka 2014.
 
Back
Top Bottom