Kamwe usilazimishe mahusiano/ndoa

Kamwe usilazimishe mahusiano/ndoa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,810
Reaction score
831,011
917ac30939667155c502f39d145c1f2a.jpg

Tunapozungumzia hizi habari wengi wetu tutakimbilia kuwanyooshea vidole wanawake lakini kuna wanaume pia wana hizo tabia

Ndoa na mahusiano ni taasisi moja kubwa sana! Walioko kwenye mahusiano kwa sasa no matter mnapendanaje wengi wenu hamtaoana! Wakwenu wapo na wengine saa hii nao wakiota ndoto kama za kwenu

Ndoa bila kujali imani zetu ni kiunganishi cha kiroho kisihia na fikra za ndani kabisa, ndoa ni mwanzo wa msingi unaokuja kujengewa kuta imara

Kiroho ndoa yako ipo! Mtu wako yupo! Mahusiano yako yapo! Ambayo yatakuja kuwakutanisha bila kutumia nguvu na kulazimisha vitu au hata kutumia nguvu za giza.

Mabinti msibebe mimba kama sababu ya ndoa, wazazi na walezi msipange fumanizi ili kuhalalisha ndoa za mkeka, wandugu msitumie ushawishi wenu nguvu ya fedha na ahadi za kazi nk ili ndoa ifungwe

Kufungwa kwa ndoa ni jambo la kwanza na wanandoa kudumu kwenye ndoa na kuishi maisha ya mafanikio ni kitu kingine kabisa
Wala hakuna haja ya kupoteza muda na fedha kwenda kwa wanajimu wa nyota na watabiri ati kuona kama mtaweza kuishi pamoja.

Utabiri na unajibu hutoa majibu ya jumla tu kutokana na hesabu za nyota na majira ya nyakati, ni vitu vinavyobadilika kila wakati
Jipange na maisha huku ukijibidiisha na kazi, ukiwa na hakika kwamba wako sahihi uliyepangiwa atakuja katika muda sahihi uliopangwa na nguvu iliyo juu yetu sote

Ndoa nyingi zimevurugika na kuharibika kabisa kwa sababu ya kulazimisha mambo...!!!ndoa imeonekana ni taasisi ngumu kwa ajili ya kulazimisha mahusiano...! Kila jambo lina mahali pake Mtu wake na wakati wake!

Soon tutapata couples zilizokutana/kutanishwa na JF! Utashangaa na kujiuliza imekuwaje? Makutano ya mtandaoni! Ni kwa vile ndivyo ilivyopangwa iwe! Tuwaombee, nawe waombee pia! Wako pia hayuko mbali ni muda tu haujafika kama hayuko JF au pale kazini kwako, yuko mahali pengine kona ya mabibo! Vumilia yuaja...! Nakuombea
 
Ilo nalo neno nina boyfriend ni mwaka Wa saba huu, hata nyumbani kwao hataki kunipeleka, najuana na marafiki zake tu..najipa moyo eti namsubiri akiwa tayari ila naona muda kwake haufiki..nazeeka buree...mambo haya magumu sana
 
That's too much lakini endelea kujitafakari
 
Mahusiano huzaliwa na kulelewa kama mtoto hadi yakomae
Mahusiano ni kama mbegu ipandwayo , inahitaji matunzo ili imee na kustawi hata ikomaze matunda
Mahusiano ya muda mfupi inabidi wahusika wawe wamejiridhisha beyond doubts kwamba tuanze hivihivi ila tutaleana! Tutapalilia magugu na kunyweshea huu mche!tutaulinda kwa hali na mali kwa mvua na kiangazi...Mahusiano kama haya yanawezekana JF tu huko kwingine ni ngumu kwakuwa ndani ya JF watu ni wakomavu na wanaojitambua
 
Mshana hii thread umeniandikia mimi nini?
 
Back
Top Bottom