Kamwe siwezi kuwaamini watu walioteuliwa na Rais katika nchi inayoitwa Tanzania

MWANAHARAKATI MWEMA

Senior Member
Dec 16, 2022
192
270
Natanguliza shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa kusamehe, pia nawashukuru wazazi wangu Kwa kunileta duniani na kuweza kupata uhai ambao Leo hii unanifanya naweza kufikiri Kwa mapana.

Leo katika kupitia pitia katika mitandao ya kijamii nimekutana na nukuu iliyonukuliwa wanahabari kutoka Kwa Hussein bashe aliyewahi kuteuliwa kuwa naibu waziri wa kilimo na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Magufuli ambae Kwa sasa ni marehemu, katika nukuu hiyo bashe ameeleza kwamba awamu ya tano "hakukuwa na ushindani wa kimawazo katika kilimo" kitu ambacho Mimi naona si kweli ndio maana naona hawa wateule wanatuyumbisha na vyema katiba mpya idaiwe Kwa namna yoyote ili kuondoa walamba asali na machawa.

Katika moja ya hotuba za Bashe baada ya kuteuliwa kuwa waziri alinukuliwa akisema kwamba baada ya uteuzi waunaibu waziri, kipindi ambacho korosho na mazao mengine yameyumba kutokana na wateja au wanunuzi Wa mazao hayo kususia kununua mazao, yeye kama naibu waziri aliitwa na rais na kumuomba kumshauri nini cha kufanya ambapo yeye alimshauri Rais kwamba serikali haitanunua tena mazao na wazo hilo Rais alilikubali mpaka Leo hii mifumo aliyopendekeza ndiyo inayofanya Kazi.

Katika uongozi wa Hayati Magufuli ndio uliomuamini bashe baada ya kuwa anaonekana bungeni akiwa anatoa hoja zenye tija na mwanga Kwa kilimo,marehemu alimuona akaona huyu atatufaa na anaifaa nchi na mipango mingi aliyoibuni aikuingiliwa na mpaka Leo hii bado ipo, yeye ndiye aliyemshauri marehemu kuanza kujenga mabwawa ya kilimo cha umwagiliaji ambacho Leo hii ndio kinatekelezwa lakini yote hayo Ni kutokana na uhuru aliopewa baada ya kuaminiwa, bashe kabla hajateuliwa alionekana mpinzani na sio mtanzania Ila JPM alimuamini.

Shida yangu Kwa wateule wenye maamuzi na mustakabali wa wizara au taasisi wanashindwa kufanya mambo Kwa wakati uliopo na kupenda kuongelea mambo ya nyuma Kwa kutaka kujipa uchawa husio na faida yoyote Kwa nini tuwe na viongozi vigeugeu ambao wanabdadilika kama kinyonga,kiongozi anabadilika kutokana na uongozi uliopo Kwanini husijiuzulu kama unaona hukubaliani na kiongozi wako, Kwanini uendelee kutekeleza mipango husiyokubaliananayo.

Katika nchi ambayo viongozi wake wamepevuka huwezi Kuta kiongozi hakubaliani na kiongozi wake wa akaendelea kukalia kiti,fanya Kwa vitendo jiuzuru watu wote tutajua kweli huyu hapendi upuuzi lakini kuendelea na kukaa Kimya si uongozi wala haufai kuwa kiongozi utabaki kuwa Chawa.

Namalizia Kwa kusema ili taifa letu liweze kupiga hatua Ni lazima tuwe na viongozi wenye maamuzi magumu na yenye tija na hata kama itaonekana hayana tija yapingwe Kwa nguvu zote na kama Kuna uwezekano wakujiuzulu ili kupinga uongozi zalimu bhasi mtu hasisite kufanya hivyo na kuja baadaye kuja kutupigia Kelele ambazo hakupi sifa za uongozi wa mfano, na mambo haya hadi wapinzani wameyabeba wao pia wamekuwa machawa.

Katiba inaeleza vyama vya siasa Ni haki yao kufanya mikutano ya kisiasa lakini wanalialia kumuomba Rais haki yako inadaiwa haiombwi mkome kuwa machawa tekelezeni wajibu wenu kwa mujibu wakatiba.

Asanteni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom