Kamwaga na mitandao ya kijamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamwaga na mitandao ya kijamii

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Oct 7, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jana nilimsikia kupitia kituo cha Television cha ITV Msemaji(ovyo) wa Simba (Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara) Bwana Ezekiel Kamwaga akiujulisha uma wa watanzania hatua wanazojiandaa kuchukua kama team dhidi ya watumia mitandao ya kijamii wote wanaochangia hoja ambazo pengine hazimfurahishi yeye,Viongozi wenzake,na team anayoitumikia kwa ujumla.
  Lazima niseme kama ilivyo siku zote jana Kamwaga ameendelea kuongeza shauku yangu ya kutaka kumjua vizuri background yake,elimu yake na mambo kadhaa yanayoweza kujenga weredi wa mtu, Kamwaga aliyekuwa aki'respond to swali la Mwandishi wa habari aliyetaka kujua maoni yake kuhusiana na Haruna Moshi "Boban" baada ya kumchezea rafu iliyoonekana kuwa mbaya mchezaji wa Yanga Kelvin Yondani,aliishia kulaumu watu wanaomshutumu Boban kwa mchezo ule na kumtolea maneno aliyoyaita makali kwenye mitandao ya Kijamii huku akitoa ahadi ya kuwashughulikia, nanukuu "..Simba sasa tunajiandaa kuwashughulikia wale wote wanaomtolea maneno makali mchezaji wetu Haruna Moshi,tumeshaongea na Mwanasheria wetu na tutachukua hatua...." mwisho wa kunukuu.
  Kwanza sijajua hivi huu "utumbo" anaouongeaga mara ka mara Msemaji(ovyo) wa hii team huwa ni official taarifa za Club au ni matamshi yake binafsi? Binafsi nafikiri hili ni tatizo kama si la Kamwaga binafsi basi ni la safu nzima ya uongozi wa mabingwa hawa,haiwezekani wawe na mahaba yaliyopitiliza kwa baadhi ya Wachezaji wao kiasi cha kutoona matatizo yao hata pale yanapojionyesha wazi, issue ya utovu wa nidhamu kwa Haruna Moshi "Boban" siyo ya kwanza,aliwahi kumkung'uta ngumi mchezaji mwenzake mbele ya wachezaji wenzake na baadhi ya viongozi na hakufanywa kitu,haya juzi kamvunja mfupa gani sijui beki tegemeo wa team ya Taifa wakati mwenyewe Haruna Moshi akijutia suala lile na kunukuliwa na vyombo vya habari mbalimbali uongozi wa Simba kupitia Msema(ovyo) huyo wanaona ndo kwanza mchezaji wao anaonewa,mi nilitegemea uongozi wa Simba ungekuwa wa kwanza kukaripia tukio lile kwani licha ya kumsababishia matatizo mchezaji wa team ya Taifa lingeweza hata kuigharimu team yake kama Mwamuzi angekuwa fair,je huku si kuficha maradhi ambapo mwisho wake kila mtu anaujua?
  Anyway mambo ya Ngoswe namwaachia Ngoswe mwenyewe lkn ninachotaka kumshauri Bwana Kamwaga huu ni wakati wa kuitumia nafasi hii ya kuwa Mwajiriwa wa team ya Dar-es-salaam kwa kuongeza elimu kidogo ili aweze kuongeza weredi wake,elimu ni factor muhimu sana katika kuongeza upeo wa mtu kuelewa,Dsm kuna centre nyingi sana anaweza ku'reseat kama alikuwa hajamalizana na NECTA issue za Credit na mambo mengine ya namna hiyo au kama alikuwa ameshasogeasogea kwenye level ya mbele mathalani Certificate zao zile za Journalism si vibaya akaanza mchakato wa kuitafuta Diploma na kuendelea mbele zaidi, hii itamsaidia kuongeza ufahamu wa yeye kama Msemaji wa team anatakiwa aisemee nini team yake na nini asiisemee,asiangalie umri Wahenga walisema elimu haina mwisho.

  Nawasilisha!
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  Anaropoka kama Mtatiro.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 3. M

  Masuke JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hivi wewe na viongozi wako wale wa zamani na wa sasa mlishawahi kuomba radhi kwenye ishu yenu ya wachezaji ya kumpiga refa au wewe kila siku mbio mbio kwenye TV kumsikiliza Kamwaga kasema nini, halafu tena mbio mbio kwenye computa yako kuja kutujulisha humu JF?
   
 4. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kaka usione Viongozi waliwapigania wapunguziwe adhabu,waliadhibiwa wale,wote walikatwa mishahara kama ulikuwa hufahamu muulize Stephano Mwasyika hata juzi Msuva amepewa onyo kali kwa kufanya kosa la kizembe lililomsababishia card nyekundu inanishangaza kuona Viongozi wenu ndo kwanza wanalalamikia Card za Okwi na Maftah na juzi tena issue ya Boban mnatuchimba mikwara eti Mwanasheria,Uanasheria si fani tu kama ilivyo fani nyingine yeyote ya kitaalamu?
   
 5. M

  Masuke JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Sina taarifa kama waliadhibiwa lakini kwa nini haikusikika kuomba radhi hata siku moja, hata wachezaji wenyewe isipokuwa Niyonzima pekee ndo aliomba radhi, lakini ni kuadhibiwa kimya kimya fuatilia hii link wadau wa Simba wanavyopendekeza kwa wachezaji waliopewa red card.
  Sare yaikoroga Simba
   
 6. j

  joel amani Senior Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aibu tupu soka letu,huyu boban kila leo anamatukio ya ajabu hasa kuumiza wenzake nashangaa simba viongozi wa simba hawamchukulii hatua kali,nafikiri wanaogopa atawavutia mibangi ili nao watembelee kichapo kitakatifu
   
 7. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ndo nakupa taarifa Mtani,wale wote waliadhibiwa kwa kukatwa mishahara, unajua hii michezaji ya kibongo ni kama watoto,imagine una toto lako tukutu kila siku linaharibu huko mtaani kesi zikija kwako unalitetea na kuwatisha wale wanaokuja kulishtakia kwako wewe Mzazi wake hapo utakuwa unajenga au unabomoa? hiyo approach ya FOS ndo good approach ya ku'maintain discipline ya wachezaji generally,lkn umemsikia hapo Maha(Rage) ndo maana mimi nasemaga siku zote Rage,Kaburu na Kamwaga lao 1 siku zote.
  Kuhusu wachezaji wa Yanga Mwasyika na Niyonzima kwa nyakati tofauti waliomba radhi Kaka, kwa kawaida unapoomba radhi baada ya kuharibu maana yake ni kuwa unakiri kukosea na unaomba radhi kwa huko kukosea kwako,ni dalili 1 wapo ya ukomavu.
   
 8. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kamwaga,boban naskia wote washkaji wa kijiwe kimoja nafikiri umenielewa wanashare nini hawa.
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ungeenda kupitia blog ya bin zubeiry ungeweza jua kabisa akili za wanayanga ni moja dunia nzima kutwa kuongea usimba na kutoongelea uyanga wao ngoja tuone wale waamuzi waliotolewa nduki kisa simba kupewa droo na linesmen..
   
 10. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kamwaga hana akili hata kidogo,sijajua kama kweli professional yake ni JOURNALISM?!,Nasema siamini kwa sababu matamshi yake hayana uwiano hata kidogo na hata hiyo level yake aliyonayo.

  Kwanza aliponishangaza ni kauli yake ya kuchukua hatua dhidi ya mitandao ya kijamii kama vile JF!!!!!!!!

  Kwa kifupi Anselm umesema vizuri sana katika tenzi zako na sitaki kutia doa,naamini Huyu msema hovyo atakua amesoma.
   
 11. m

  mzalendoasilia Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu nadhani unaugomvi binafsi na huyu Msemaji wa club! Kimsingi sioni hoja yoyote zaidi ya kudhihirisha unazi wako kwa Yanga ! Unasema unawasiwasi na elimu ya huyu bwana , lakini hata mimi nawasiwasi na UELEWA WAKO WEWE BINAFSI PIA! Hivi wewe katika maisha yako rafu pekee uliyowahi kuiona ni ya Haruna Moshi kwa Yondani? Ni mara ngapi mechi za simba na yanga wachezaji wa simba wameumizwa bila Yanga kama Klabu kuomba samahani? unakumbuka mwinyi Kazimoto alipoumizwa , je nyinyi Yanga mliomba samahani? Then unazungumzia nidhamu ya wachezaji na viongozi wa simba, ama kweli nyani haonin kundule! Hivi sio nyinyi Yanga mliompiga mwamuzi kwenye mechi na Azam na bado hakuna kiongozi wa yanga aliyeomba samahani zaidi ya kuwatetea wachezaji wenu? Na bado hao viongozi wa TFF sababu wote ni Yanga wenzako wakawafungia mechi chache tu kinyume na kanuni! Hivi kosa la kupiga refa adhabu yake ni kukosa mechi 3? Siuoni usomi wako hata kidogo kama huna kumbukumbu ndogo tu kama hizi nilizokupa! Ungekuwa na elimu kama unavyojinasibu usingeegemea upande wowote ila kuwasema wote simba na yanga wanamatatizo watu wangekuelewa. Sioni hoja za kimsingi zaidi ya kum attack personally huyu bwana. Msomi hujenga hoja kwa facts and references na si kusukumwa na mapenzi yake binafsi! Inawezekana huyu bwana anamapungufu yake hatukataai but na wewe umeonyesha mapungufu makubwa ktk kujenga hoja hivyo nakushauri na wewe ukatafute chuo urudie masomo!
   
 12. m

  mourad77 Senior Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 178
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Acheni malumbano yasio na tija hili jitu sijui KAMWAGA sijui KAZOA halina akili hata kidogo ni mipandikizi ya MSOMALI tu wanasimba wenyewe wanalishangaa jitu hata kuongea haliwezi utafikiri linatafuna pariki yaani nawashanga ssana wandishi wa habari yani dude kama hili linawaita eti kufanya press confres nawe unaeenda jitu hata kuongea haliwezi lipo lipo tu kazi kuongea pumba kila siku Matola mwenyewe kocha wa timu B ya simba kalalamika rafu ya Boban kaongea na vyombo vya habari aende basi akamshtaki pia namalizia kusema MHARAGE Katuletea mijitu ya ajabu huyu KAMWANGA NA MAESTRO Hawa uwezo wa kuwa katika klabu kama Simba warudi mikoani walikotoka Kigoma na Ruvuma hawajalijuwa jiji bado saana tunahitaji watu wenye Elimu zao sio wapuzi kama hawa
   
 13. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu hii ya kwako sasa ndo "personal attack" kwangu mimi binafsi,nahisi wewe kama si Kamwaga mwenyewe basi ni moja kati ya Vibaraka wa ule utatu wa Msimbazi (Rage,Kaburu na Kamwaga),whoever you may be nataka nikueleze yafuatayo:- Kuhusiana na issue ya Kazimoto ninasikitika sana watu wa Simba wenyewe aidha hamuijui vizuri au mnajaribu kupotosha hadhira kuhusiana na jambo lile,binafsi nimeshalitolea maelezo sana kwenye posts nyingine humu ndani na wenzako wameanza kulielewa kiasi kwamba hawaliongelei tena,please go and read hayo maelezo usiongeze wingi wa maneno kwenye thread bila sababu. Hapo kwenye kujenga hoja kwa facts umenifurahisha sana,ukisoma vizuri hoja yangu unatakiwa uelewe yafuatayo:-
  1.Asingekuwa ni KILAZA huyu Msemaji(ovyo) wenu ange'respond kwa swali la msingi aliloulizwa na Mwandishi badala ya kuchimba mkwara usiokuwa ni kichwa wala miguu,hivi kulikuwa na umuhimu gani wa kuchimba mkwara ikiwa swala lilikuwa wazi na Mtendaji mwenyewe alishakiri na kuomba radhi na watu walisha'appreciate na kumsamehe na kupunguza kama si kuacha kabisa kumshambulia?
  2.Kwenye hoja yangu ya msingi nilionyesha mashaka yangu juu ya taarifa anazozitoaga huyo Msemaji(ovyo) wenu kama zinakuwa ni official taarifa za Club au matamshi yake binafsi, na jana nimedhihirisha kuwa huyu Jamaa yeye huwa anajitapikia tu,wakati juzi aliutangazia Uma kuwa beki Shomari Kapombe aliumizwa vibaya na Said Bahanuzi na angekosa mchezo wa jana kwa kuwa ni Majeruhi, jana Kapombe alikuwa uwanjani physically fit and at his best,mi nilifikiri alikuwa anawasilisha taarifa aliyopewa na benchi la ufundi kumbe alikuwa anawasilisha taarifa waliyoiandaa yeye na Mkewe, kwa kutofuta ujinga vizuri mwenyewe aliamini kwa kudanganya hivyo angesaidia ku'neutralize kosa la Boban, watu wangesema mbona Kapombe mwenyewe kaumizwa na Bahanuzi...
  3.Si mara ya kwanza kwa Kamwaga kuja na taarifa isiyoingia kwenye vichwa vya watu timamu,nitakukumbusha 1 tu aliwahi ku'report tukio la Mwenyekiti wake kunywa kahawa saa 4 asubuhi katikati ya Mfungo,enh......!!!! aren't these the facts Mkuu? niambie katika hizi 3 ni ipi haikuhusu/haimhusu Kamwaga (if you are not the one)
  Naomba nikusahihishe kidogo; hoja yangu haikulenga kumtaka Kamwaga aombe radhi,radhi ilishaombwa na mkosaji na ilishapokelewa kwahiyo binafsi sioni msingi wa hoja yako kuwa Viongozi wa Yanga nao hawakuomba radhi,ni kweli viongozi wa Yanga hawakuomba radhi ila wakosaji wenyewe(Mwasyika na Niyonzima) waliomba radhi kama alivyofanya Boban,walichofanya Viongozi wa Yanga ni kuwaadhibu in addition to zile adhabu za Kamati ya nidhamu,unapomwadhibu mkosaji unamfundisha next time asirudie upumbavu mwingine kama ule na ndo maana umeona upole wa wachezaji wa Yanga kwenye mechi ya juzi licha ya kuwa ilikuwa na hali kama ile mechi yao na Azam,ni ksbb waliadhibiwa na sasa wamejifunza kupiga/kupigana siyo ujanja...lkn hili Viongozi wenu wamekuwa hawalifanyi na Jamii inapojaribu kuonya wanakuja mbele ya Jamii na kuwatetea,sasa hapo hammalizi matatizo bali mnayafanya sugu,fikiria Boban peke yake indisciplinary issues ngapi ame'conduct na Viongozi wa Simba ndo kwanza wanampigia makofi,aliwahi kumpiga mchezaji mwenzake ngumi hakuchukuliwa hatua,akawahi kupanda kuchukua medali nje ya jezi ya team yake(na pensi yake chafuchafu) hawakumchukulia hatua,akatoka nje ya uwanja kabisa baada ya kupigwa sub,still bado Viongozi wakakaa kimya juzi katika tukio lililoonekana la makusudi amemwumiza mchezaji wa team ya Taifa wamekaa kimya,watu wanasema naye kumsaidia ndo kwanza Kiongozi mmoja anaitisha press kuwatishia wanaomkosoa,hizo ni akili au matope?na hizo ni baadhi tu,zile za kuondoka kambini ndo za kumwaga hakuna hatua yeyote inayochukuliwa,hivi unategemea mchezaji huyu ambaye kila mtu anakubaliana na kipaji chake atajirekebisha lini? Haya Okwi juzi kapiga mtu Kiwiko kapigwa red,ka'miss mechi 3 jana karudi uwanjani kavua jezi baada ya kufunga goli kapigwa yellow...cards za kujitakia kabisa,kwa Viongozi wenu shwari,sanasana utasikia tu kuna mkono wa mtu,mtu kiwiko anapiga mwenyewe,jezi anavua mwenyewe akipewa card fedha za Manji,wapi na wapi?
  Namalizia kwa kusema sina ugomvi na Kamwaga,sina ugomvi na Kiongozi yeyote wa Simba,hapa tunajadili michezo kwa uwazi kumbuka JF is a place where we dare to talk openly!
   
 14. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,366
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180

  Mkuu, naomba kutofautiana na wewe kwa kiasi kukubwa kwa kile ninachokiona kutoka kwako ikiwemo ubinafsi, unazi uliopindukia na hoja za kashfa zisizo la lazima.

  1. Kamwaga amesema Simba inawasiliana na wanasheria wake kuangalia namna ya kushughulikia watu wote wanaomtolea MANENO MAKALI mchezaji wao. Maneno makali ni kama vile kashfa, matusi, na maneno mengine yasiyo ya staha. Hapa ikumbukwe kuwa Kamwaga hajasema Boban hakucheza rafu, anachopinga ni mchezaji wao kusemewa maneneo ya kudhalilisha wakati kilichotokea ni tukio la kimchezo.

  2. Hoja yako ya kusema yawezekana tatizo la kamwaga ni la safu nzima ya uongozi wa Simba, inaweza kuwa na mashiko lakini haiwezi kukamilika bila kuangalia kinachotokea upande wa pili yaani Yanga. Bado siamini kama timu kongwe kuliko zote haijaomba radhi umma wa watanzania kwa kitendo kisicho cha kiungwana cha kumpiga refa Israel Nkongo pasipo sababu za msingi. Si uongozi wala mashabiki wanaojutia tukio lile. Hebu tuwe wa kweli, ni kipi kinachotakiwa kukemewa na viongozi kati ya tukio la rafu ya Boban na kipigo cha wachezaji kwa refa?

  3. Elimu ya Kamwaga - haiongezi tija kwenye hoja yako. Hata wenye elimu kubwa wanaweza kuzungumza kitu ambacho wewe hukipendi na ni dhahiri utakipinga. Naamini Kamwaga angezumza jambo unalolipenda usingechunguza elimu yake na badala yake ungesifia. Natamani tuwe tunatoa mawazo yetu bila kukashifiana, kudhalilishana au kutukanana.  Ninachokisema hapa ni kuwa upenzi wa Simba na Yanga wakati mwingine unawapunguzia wengi uwezo wa kuona hali halisi kiasi kwamba kila kinachofanywa na wapinzani ni kibaya tu na chao ni sahihi tu. Hili haliwezi kutufikisha popote. Ukweli ni kwamba Simba na Yanga zina changamoto kubwa za kuitumia hamasa na sapoti kubwa ya washabiki waliopo katika hali ya faida zaidi kuliko kutumia nguvu kubwa ya kubadilisha hali halisi.
   
 15. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu sina desturi ya kutoa kashfa,anyway inawezekana wewe ukawa unatafsiri kama kashfa wakati mimi naona ni sentesi/habari adirifu, Kaka usije kukuta the way ninavyomu'identify Bwn Kamwaga kama Msemaji(ovyo) wewe kwako unachukulia kashfa,embu nisaidie ni jinsi gani unaweza kumu'identify mtu ambaye kila mara anakuja kuueleza Uma habari fulani ambayo baadaye huja kudhihirika siyo ya kweli?
  Msingi mkuu wa hoja yangu haukuwa Kamwaga kukanusha Boban hakucheza rafu, msingi mkuu ulikuwa yale majibu na maelezo aliyoyatoa yalikuwa yanajibu swali aliloulizwa na Mtangazaji? na pale kwenye majibu yale ndo mashaka yangu juu ya weredi wa huyu Jamaa yanaposimamia.
  Vyote viwili vinatakiwa kukemewa Mkuu.Ni kweli Viongozi wa Yanga hawakusikika kuja kuomba radhi mbele ya hadhira lkn pia hawakusikika kuja kutetea utumbo ule wa wachezaji wao mbele ya media, mfano juzi Msuva kafanya kosa la kizembe umemsikia Mwana Yanga gani akimtetea? hakuna...na uongozi umempa onyo kali,sasa embu tuangalie upande wa 2..ni mara ngapi Viongozi wenu wamesikika wakitetea vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa ndani na nje ya uwanja na wachezaji wenu?
  Hapa si suala la fulani anazungumza jambo nisilolipenda kwahiyo lazima nitalipinga, hapa ni kuangalia wingi wa habari "matapishi" zinazotolewa na huyu aliyepewa dhamana za kuisemea 1 ya team kubwa kabisa Africa Mashariki kama si Africa nzima,wingi huo ndo unaonipa mashaka juu ya uelimikaji wa Mtoa habari huyu,I might be wrong lkn ni mashaka yanayo bling kwenye kichwa changu.
  Namalizia kwa kusema ni kweli mapenzi kwa upande fulani huweza kumfanya mtu asione mabaya yanayokuwa comitted either na team yake au Viongozi wake,lkn nataka kukuhakikishia kuwa mimi si mtu wa aina hiyo,mimi huongelea hata mapungufu yanayoihusu team na Viongozi wangu katu siegemei upande mmoja.
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Mashabiki wa YANGA bwana..........:lol::lol::eyebrows::eyebrows::embarassed2::embarassed2:
   
 17. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,098
  Likes Received: 1,482
  Trophy Points: 280
  Ingawa nimekuwa nikitofautiana mambo mengi na msemaji wa Simba kuanzia pesa za rambirambi za mafisango na pesa za zawadi za timu b ya Simba lakini mada yako umeiwasilisha kiushabiki zaidi kwanini umeshindwa kukemea kitendo cha Mwinyi Kazimoto kukanyagwa akiwa chini tena ameanguka au Ngasa kukatwa akiwa hana mpira na wote hao ni wachezaji wa timu ya Taifa kama Mwasika angeadhibiwa kama unavyosema sidhani kama angerudia utovu wa nidhamu na pia sijasikia kauli yoyote ya viongozi wa Yanga wakizungumzia matendo hayo ambayo wote tunajua hayakuwa ya kiuanamichezo kwani michezo hujenga upendo na urafiki
   
 18. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,286
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mashabiki wa yanga siwatofautishi na washabiki wa sisiemu, akili zao zinafanana kwenye kufikiri,
   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  no no nooooo.........
   
 20. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #20
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,286
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hata jezi za timu yenu yanga na bendera za sisiemu zinafanana, so don't say no
   
Loading...