Kampuni za ukaguzi 'audit firms' mjiandae kufa kifo cha mende

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Wale wa kampuni za ukaguzi al maarufu kama audit firms kama pwc, delloite, kpmg, ey mkae mkijiandaa kufa. Hii nawapa tu tahadhari

Juzi mlimsikia CAG akisema amepunguza gharama za ukaguzi kutoka kwenye makampuni binafsi yaliyokua yakikagua taasisi za serikali kubwa kama benki kuu.

Makampuni makubwa ya serikali yamekua miaka na miaka yakikaguliwa na makampuni binafsi kwa sababu ofisi ya cag haina uwezo wa kufanya ukaguzi makampuni au taasisi zote za serikali, hivyo imekua ikitumia makampuni binafsi kufanya ukaguzi ila sasa cag anataka kuondokana na utegemezi wa makampuni binafsi kwenye kufanya ukaguzi.

Serikali imeahidi kuongezea rasilimali watu na rasilimali fedha ofisi ya cag ili iweze kufanya ukaguzi yenyewe, hivyo wenye kampuni binafsi za ukaguzi lazima muanze kufikiria namna nyingine ya kuongeza kipato maana mteja wenu mkubwa serikali anawakimbia huku private sector yetu sio stable and reliable, wafanya biashara wengi hawaandai hesabu na biashara zinaendeshwa kijaja janja, makampuni binafsi imara ya kueleweka ni machache, mjiandae na huo mtikisiko.
 
Kuongeza idadi ya wafanyakazi kwa ajili ya kazi za miezi mitatu ilihali wewe utawalipa miezi 12 pamoja na lizizo ya mwaka nao si uamuzi sahihi. Kitu muhimu ilikuwa na Serikali kuingilia namna audit firm zinavyotoza ada zake za ukaguzi au kutumia zaidi kampuni ndogo na za kati.

NB: Nami ni mdau wa hizo kampuni za ukaguzi
 
hata kama 25 hizo kampuni zina wafanyakazi wangapi? hapo ametatua au ameongeza tatzo la ajira
Tunabana matumizi ndugu! Hizo kampuni itabidi ziwe na contingent plan! Na ni kweli kila maamuzi yana faida na hasara! Kwa hili, lina faida kwa serikali!
 
umefikiria ni vijana wangapi watabaki mtaani kwa kukosa ajira?
 
Kwa ajira, kuna tatizo, lakini kwa matumizi ya serikali amepunguza! I also feel bad for those who are going to be out of business! Hata hivyo, makampuni yanahitaji kuwa na mbadala ili kujihakikishia usalama…sasa kama walibweteka na serikali tu as their solo customer, hii itakuwa mbaya sana kwao!
 
ki
umefikiria ni vijana wangapi watabaki mtaani kwa kukosa ajira?
kusema ukweli sijui wangapi watakosa ajira! Lakini mpaka CAG kufikia maamuzi hao, ameona kuna faida zaidi ya hasara!
 
Tunabana matumizi ndugu! Hizo kampuni itabidi ziwe na contingent plan! Na ni kweli kila maamuzi yana faida na hasara! Kwa hili, lina faida kwa serikali!

Unabana matumizi kwa kuongeza gharama? Ili aondoe outsourcing inabidi aajiri watu watakaofidia pengo la audit firms. Full time salaries vs buying services.
 
Wale wa kampuni za ukaguzi al maarufu kama audit firms kama pwc, delloite, kpmg, ey mkae mkijiandaa kufa. Hii nawapa tu tahadhari

Juzi mlimsikia CAG akisema amepunguza gharama za ukaguzi kutoka kwenye makampuni binafsi yaliyokua yakikagua taasisi za serikali kubwa kama benki kuu.

Makampuni makubwa ya serikali yamekua miaka na miaka yakikaguliwa na makampuni binafsi kwa sababu ofisi ya cag haina uwezo wa kufanya ukaguzi makampuni au taasisi zote za serikali, hivyo imekua ikitumia makampuni binafsi kufanya ukaguzi ila sasa cag anataka kuondokana na utegemezi wa makampuni binafsi kwenye kufanya ukaguzi.

Serikali imeahidi kuongezea rasilimali watu na rasilimali fedha ofisi ya cag ili iweze kufanya ukaguzi yenyewe, hivyo wenye kampuni binafsi za ukaguzi lazima muanze kufikiria namna nyingine ya kuongeza kipato maana mteja wenu mkubwa serikali anawakimbia huku private sector yetu sio stable and reliable, wafanya biashara wengi hawaandai hesabu na biashara zinaendeshwa kijaja janja, makampuni binafsi imara ya kueleweka ni machache, mjiandae na huo mtikisiko.

Makampuni na Mashirika ya binafsi tena ya kimataifa yapo ya kutosha hapa Tz na ndo wanafanya auditing huko na hata mapato yao ndiko wanakotegemea kuliko ktk mashirika ya Serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom