Kampuni ya uwindaji ya Ortello matatani Arusha.................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,620
2,000
Mashirika yaungana kuishtaki OBC

na Ramadhani Siwayombe, Arusha

amka2.gif
MGOGORO wa ardhi kati ya wafugaji wa Kimasai walioko Loliondo na Mwekezaji wa Kampuni ya Ottelo Busines Cooperation (OBC), limechukua sura mpya baada ya mashirika manne yasiyo ya kiserikali kufungua kesi ya Kikatiba mahakamani kupinga zoezi la kuwahamisha wafugaji hao. Wafugaji hao wako wilayani Ngorongoro mkoani Arusha, waliondolewa kwa nguvu baada ya OBS kuchoma moto maboma na wanyama wao ili kuwaondoa eneo hilo.
Mashirika hayo ni Pingo's Forum, Ngorongoro Non Govemental Organisation Network (NGONET), Ujamaa CRT na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Mashirika hayo yanawakilishwa mahakamani na mawakili watatu ambao ni Fulgence Masawe kutoka LHRC, Daimu Halfan wa kampuni ya uwakili ya Mpoki na Clarence Kipogoto kutoka Shirika la Legal and Development Consultancy.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Loliondo, Eliasi Wawalai, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ngorongoro na Kampuni ya Uwindaji ya OBC.
Akizungumza na waandishi baada ya kufungua kesi hiyo juzi, Mkurugenzi wa Pingo’s Forum Edward Porokwa, alisema lengo la muungano huo ni ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na OBC.
Alisema katika kesi hiyo wanaitaka mahakama itoe tamko kuwa zoezi zima lililofanyika kuanzia Julai 4 mwaka jana la kuwaondoa wafugaji katika maeneo yao kuwa ni batili.
Alifafanua kuwa wanataka mahakama iseme matukio hayo yamekiuka kipengele cha 14, 16 na 24 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kukiuka sheria ya wanyama pori ya mwaka 1974 na sheria ya Ardhi namba 113 vifungu vya 17 kifungu cha 1 na 27. 

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,062
0

Hizo NGO na mawakili wanataka kuvuta mshiko tu. Kwani kesi itashindwa.

Walioondolewa walikuwa wamevamia, wale waliopo awali walishalipwa na wakahama na masharti waliyoweka mwanzoni ya kupatiwa maji, shule na zahanati yote yalitimizwa na ziada, miaka kadhaa nyuma.

Hao walioondolewa na vibanda vyao kuchomwa moto, walivamia kinyemela baada ya kuona wenzao walifaidika wakadhani na wao watakula mshiko. Hawakuwapo kwenye listi rasmi za kumbu kumbu ya wakaazi wa maeneo hayo waliokwisha fidiwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom