Kampuni ya sasatel imekufa rasmi?

Kampuni ya sasatel imekufa rasmi?

oyaoya

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2012
Posts
277
Reaction score
39
Wakuu, hawa jamaa kuaniza tarehe 28.01.2014 bila taarifa yoyote:-
Wamefunga ofisi zao za makao makuu pale Masaki na kubakiza wafanyakazi wasiozidi wanne tu, nadhani wanalinda linda baadhi ya mali zilizosalia kabla ya kutokomea.

Ofisi yao inafunguliwa baada ya saa 5 asubuhi.

Simu zao zote za huduma kwa wateja na zinazoonekana kwenye mtandao wao http://www.sasatel.co.tz/contact-us.html hazipatikani.
Wafanyakazi waliosalia wamewajibu wateja kuwa wana matatizo ya umeme na wangerekebisha ndani ya siku tatu tu lakini ni zaidi ya wiki sasa hakuna huduma ya internet.

Kinachoumiza zaid wamechukua malipo yangu ya bundle ya internet ya miezi miwili kwa ajili ya kibanda changu cha internet na hakuna dalili ya kurudi huduma yao. Ni zaidi ya kurudishana nyuma wakuu.

TCRA tusaidieni katika hili.
 
Wameshindwa kwenye soko la ushindani
 
Sidhani kama soko lao lilikuwa gumu hivyo kwa kuwa walishafanikiwa kuanza kujitanua. Nilipumua na urasimu wa pale ttcl, lakini kwa hali hii itabidi tukawapigie tena magoti kwa mara nyingine.
Kama kuna anayeifahamu kampuni nyingine inayotoa huduma za internet kwa rauter tu bila ya kuwa na connection line atuwekee hapa wakuu...
 
Walikuja na visimu kama vya ttcl nao wamejifia.
 
Back
Top Bottom