kkarumekenge
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 1,708
- 1,026
Wakazi wengi mkoani Mwanza na bila shaka sehemu nyingine nchini wametapeliwa na kampuni iitwayo POS ambayo imechukua mamilioni ya fedha kutoka kwa wananchi wakishirikiana na benki moja nchini. Wahanga wa utapeli huo ambao ulibarikiwa na Waziri mmoja na halmashauri ya Jiji la Mwanza wamefika hadi kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, na baadhi ya matapeli hao kuwekwa ndani lakini waliachiwa katika mazingira ya kutatanisha. Kama ilivyokuwa DECI, matapeli hao walidai hata ofisi ya Waziri Mkuu inawatambua, na ndiyo sababu Waziri alikuja siku ya uzinduzi huko Kiseke, Mwanza. Walifungua ofisi Mwanza, lakini baada ya kutapeli ofisi hizo zimefungwa.