Kampuni ya POS yatapeli mamilioni Mwanza

kkarumekenge

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
1,708
1,026
Wakazi wengi mkoani Mwanza na bila shaka sehemu nyingine nchini wametapeliwa na kampuni iitwayo POS ambayo imechukua mamilioni ya fedha kutoka kwa wananchi wakishirikiana na benki moja nchini. Wahanga wa utapeli huo ambao ulibarikiwa na Waziri mmoja na halmashauri ya Jiji la Mwanza wamefika hadi kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, na baadhi ya matapeli hao kuwekwa ndani lakini waliachiwa katika mazingira ya kutatanisha. Kama ilivyokuwa DECI, matapeli hao walidai hata ofisi ya Waziri Mkuu inawatambua, na ndiyo sababu Waziri alikuja siku ya uzinduzi huko Kiseke, Mwanza. Walifungua ofisi Mwanza, lakini baada ya kutapeli ofisi hizo zimefungwa.
 
Ungefunguka Zaidi Mkuu, utapeli wa namna gani ulifanyikaje, Hiyo kampuni ilikuwa inatoa huduma gani na kwa malengo gani na Benki walihusikaje?

Pole kwa wahanga lakini kupenda hela ya haraka haraka kuliwaponza, Kwanini watu hawajifunzi kupitia yaliyopita kama DECI, Powerclub, sijui Mega...na nyinginezo nyingi na hata RIFARO nayo nasikia chalii
 
DAH! NIKO MWANZA LAKINI SIJUI KITU HICHO, WASIOJISHUGHULISHA LAZIMA WALIZWE KWA KUPENDA SHORT CUT .
 
Poleni wapenda vitonga.Sasa hivi pesa ngumu hiyo hiyo kidogo kila mtu anaitaka nani wa kukupa wewe mipesa kiulaini

Mtapeliwe tu maana kupenda ulaini kumewazidia
 
Back
Top Bottom