Kampuni ya Irvine ya Zimbabwe yaingia kuwekeza Tanzania

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,861
Ni rasmi Sasa kile kilio Cha Wafugaji wa Tanzania kukosa vifaranga kinaenda kuwa Historia Kufuatia Kampuni ya Cobb kutoka Ulaya ambayo ni Maarufu Kwa ufugaji na uzalishaji wa vifaranga wa kuku aina ya Broilers kuamua kuingia Africa.

Na mlango na mahala waliochagua ni Tanzania ambapo watawekeza mradi mkubwa wa ku supply broiler chickens Afrika Mashariki yote na Kati Kwa Kushirikiana na mshirika wake wa kutoka kampuni ya Irvine ya Zimbabwe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Cobb ni kwamba gharama kubwa za usafirishaji na masharti yaliyowekwa huko Ulaya yamesababisha waambie kuanza uzalishaji hapa hapa Tanzania Kwa Ajili ya soko la ndani na la Afrika.
Screenshot_20231011-142419.jpg
Screenshot_20231011-142448.jpg


My Take
Ni wakati wa Watanzania kuchangamkia Fursa badala ya kulalamika na kujirundika kwenye mikutano ya Machadema ambao hakuna Cha maana Huwa wanawasaidia.

Samia Anazidi kufungua fursa Kwa kuileta Dunia Kwa Watanzania ,kazi kwenu kuchangamka.
 
Cobb watakuwa wanazalisha grandparent stock tu sio broiler hawa wa kula mitaani, na mdau wao mkubwa ni IRVINES sasa sijajua kama sisi wafugaji wadogo tutaruhusiwa kununua parent stock kwao kwa kiwango kidogo.
 
Cobb watakuwa wanazalisha parent stock tu sio broiler hawa wa kula mitaani, na mdau wao mkubwa ni IRVINES sasa sijajua kama sisi wafugaji wadogo tutaruhusiwa kununua parent stock kwao kwa kiwango kidogo.
Soko ndio litaamua waende vipi Mkuu so wewe usiwaze
 
Cobb watakuwa wanazalisha grandparent stock tu sio broiler hawa wa kula mitaani, na mdau wao mkubwa ni IRVINES sasa sijajua kama sisi wafugaji wadogo tutaruhusiwa kununua parent stock kwao kwa kiwango kidogo.
Wapo zaidi miaka 2 sasa....kerege wapo
 
Back
Top Bottom