Kampuni ya Fastjet yainunua Easyjet

Kampuni ya Fastjet yainunua Easyjet

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
KAMPUNI ya Ndege ya Fastjet imenunua hakimiliki zote kutoka kwa kampuni mwenza ya Easyjet kuanzia Juni mwaka huu kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 2.5 (Sh bilioni 5.25).

Akitangaza kuhusu uamuzi huo, mwanzilishi na mwanahisa wa Easy- Group, Sir Stelios Haji-Ioannou alisema kampuni yake imechukua uamuzi huo kwa lengo la kujiimarisha zaidi, hasa ikizingatiwa kuwa kwa sasa imetanuka zaidi kibiashara.
Alisema,”Fastjet ni kampuni kubwa kwa sasa inayotoa huduma sehemu nyingi Afrika, kwa hiyo tumeona ni vema tuwauzie haki zote ili wajiendeleze zaidi kibiashara.

Aliongeza, kampuni yake ilijadiliana na bodi ya Wakurugenzi ya Fastjet na kukubaliana kuiuzia hisa zake na Fastjet na bila ya kupoteza muda imezinunua.
Pia aliweka wazi kuwa kwa sasa yeye binafsi amebakiza hisa za thamani ya pauni milioni 1.3 zinazomwezesha kuwa mwanahisa na ataendelea kuishauri Fastjet. Ofi sa Mtendaji Mkuu wa Fastjet, Nico Bezuidenhout alisema kampuni yake imenunua hisa hizo kutokea kwa wakati mwafaka kutokea Easyjet.
 
Kwenda South na Uganda vinahusiana nini na bei, hebu nifafanulie kidogo
Siongelei bei ya naule or otherwise naongelea tozo ya kodi waliyokuwa wanatozwa pindi wanaanza operation na sasa hivi inautofauti mkubwa na pia inaonekana kama shirika linajiendesha kihasara kwa hizo destination kutokana na namba ya abiria kupungua day by day.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dola millioni 2.5?!? Yaani thamani za shares za kampuni yenye mapato ya dola billioni 4.7 (Wikipedia) ndiyo iuzwe kwa pesa hiyo?
 
brother unacheka wakati mda si mrefu BOT na HAZINA mambo yatakuwa oyaoya na watanzania kuna uwezekano tusilipe kodi kwa miaka zaidi ya 10..
Ujinga wako, kwani inchi ikiwa tajiri ndo hairipi kodi da hakuna mwenye akili ndogo kama wewe maana hata kanuni ya uchumi huijui

2 Timotheo:4.2
lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
 
Inawezekana wewe unayejua kanuni za uchumi ndio ukawa na akili saaana wakati kwenye maisha yako hakuna mahali hizo kanuni zako ziliwahi kusaidia jamii au kujisaidia hata wewe...
 
Siongelei bei ya naule or otherwise naongelea tozo ya kodi waliyokuwa wanatozwa pindi wanaanza operation na sasa hivi inautofauti mkubwa na pia inaonekana kama shirika linajiendesha kihasara kwa hizo destination kutokana na namba ya abiria kupungua day by day.

Sent using Jamii Forums mobile app
Saa zingine ni bora kukaa kimya kama huelewi kitu.
Unataka kuniambia ni Fastjet tu ndio inatozwa kodi kubwa?
All in All mimi nadhani Marketing Team yao ndio mbovu, walikuwa na advantage kubwa sana kupata wateja wengi kwenye nchi hizo nilizo zitaja.
 
Mkuu sijakurupuka kutoka usingizini nikaanza kuandika nilichokiandika nafahamu na ninakielewa fika nilichokiandika, siwezi kubishana na wewe siyo hulka yangu wewe baki na unachokiamini nami nibaki na ninachokifahamu, tuko pamoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom