Kampeni za uchaguzi: Maajabu mengine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni za uchaguzi: Maajabu mengine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Sep 10, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hii nimeiona Michuzi blog:

  Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, ambaye pia ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jakaya Kikwete, ameendelea kuvua wafuasi toka vyama shindani katika mikutano ya kampeni zake baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Muheza, Joseph Mnyema, kukitosa chama hicho na kujiunga na CCM.

  Mbele ya mamia ya wakazi wa Muheza katika mkutano wa kampeni wa CCM, Mnyema alisema amehama CHADEMA kwa kuwa kimekosa sera zenye mwelekeo.

  “Kukaa upinzani ni kupoteza muda, Chama chenye mwelekeo sahihi kwa maslahi ya Watanzania ni CCM,” alisema Mnyema aliyekabidhi kadi ya CHADEMA kwa Rais Kikwete.

  Akasema zaidi kuwa viongozi wa CHADEMA hawajali utu na kwamba wengi wako kwa maslahi binafsi na si kwa faida ya wananchi.

  Naye Raisi Kikwete alimfahamisha mwanachama huyo mpya kuwa mateso aliyoyapata akiwa CHADEMA hatayaona CCM kwani inajali na kuthamini kero za Watanzania. Akawaasa wananchi kuungana na Mnyema kutafuta kura za CCM kwani amejiunga kipindi muafaka, wakati CCM ikiwa kazini kutafuta ushindi kwa Urais, Ubunge na Udiwani.


  • Hivi ni kweli maneno na sera za Chadema zinazotolewa zinaonyesha kutojali watu? Wamepewa nafasi lini ya kutojali watu, au yeye mwenyewe alijiona kuwa hajaliwi kwa sababu zake anazozijua mwenyewe? Inaonyesha wazi kuwa huyu ana tabia ambazo hazikubaliki kijamii.
  • Ni mateso gani aliyoyapata akiwa Chadema na katika hali ipi? Chadema imekuwa katika wadhifa upi ili hata kuweza kufanikisha mateso ya mtu yeyote?
  Kwa maoni mambo, tuhuma hizo zilizotolewa hapo juu ni kinyume cha mambo. Ni ccm ambayo haijali kero za watu kwa kukumbatia na kufanya ufisadi, huku wakiwadanganya watu, kwa vitendo hafifu kuwa wanafanya yanayotakiwa. Mateso wanayoyapata Watanzania ni makubwa, na ni pale watakapoitosa ccm ndipo wataelewa ni kiasi gani wlaivyokuwa wanataabika, pindi rasilimali zote zitakapolengwa katika kuboresha maisha yao, badala ya watu wachache wakiwemo viongozi wa ccm na familia zao pamoja na mafisadi ndani na nje ya nchi, walio raia na wasio raia.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi kwa nini hao wanaohama ni kutoka CHADEMA tu???????????????????? Is it the worst party of all? Kweli CCM iko desperate!!!!!
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wahenga walisema "Nyani halioni........"
   
 4. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Umasikni wa Watz, njaa, na tamaa vimegeuzwa mtaji na CCM. Kuhama huku si kwa hiari, hii ni humiliation kubwa sana mbele ya kadamnasi na mbele ya watoto wako maskini unaanza kuzikana values zako! Kama wewe huyo huyo umewahubiria watoto wako kwamba CCM ni mafisadi, wanafuja mali ya umma na wametoa ahadi hewa for nearly 50 yrs. Kesho unasimama jukwaani kwao kuwaita chama bora, Lazima uwe lunatic kupata guts za kufanya hivyo.

  Hivi mtoto wako wa miaka 7 akikuuliza imekuwaje baba CCM wamekuwa wazuri siku hizi? utamwambiaje?
   
 5. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  umenena vyema, hawana hiari hao wanaohama, na kama alitaka kuhama angehama wakati ule wa kutafuta kura za maoni, lakini CCM na kumbukeni Makamba amekuwa Tanga kwa kitambo sasa, wamemhonga ahame. Niliwahi kuona posting moja hapa ambayo ilikuwa inawataka TAKUKURU wawe wanawafuatia hawa wanaohama vyama.

  Kusema kweli ni nadra sana kusikia katika demokrasia nyingine duniani watu wanahama chama siku chache kabla ya uchaguzi. Tanzania bado tumebujika RUSHWA, na wenye kufanya hivyo ni Chama Tawala.

  Kama isingekuwa rushwa na hebu fikiria hii Ilani ya Vyama vya upinzani kama CUF na CHADEMA inavyoleta matumaini kwa mwananchi (elimu na afya bure, pia ujenzi nafuu wa nyumba), kwa nini hatuwasikii wanaCCM wanahamia huku! Ungelitegemea baada ya kutangaza hizi Ilani wengine wangekunwa wakahamia. Hili haliwezekani kwani wamezoeshwa kuhamishwa kwa hela, rushwa.
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Inachekesha. Wapinzani wanavua wabunge na mawaziri wakati ccm inavua wenyeviti wa vitongoji wa upinzani
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Alipata ajari ya pikipiki halafu hakupata mshiko kutoka chadema alipo waomba wakamwabia wang'emlipa kama ang'e anguka akiwa kazini...wakati Dr slaa alianguka bafuni ametibiwa kwa pesa ya chama akahoji bafuni kulikuwa na kazi gani.....ndicho kilicho mwondoa CHADEMA
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Milioni 60 Tshs Hiyo ishafanya kazi yake!!!
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi haujasikia viongozi wa CHADEMA wanafuatwa na kuahidiwa mihera wakiache chama na kutangaza hadharani kuwa CHADEMA nimekihama
  CCM wana hela za mchezo!
   
 10. Wun

  Wun JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2010
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 353
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hahaaaaa weekend njema
   
 11. Elinasi

  Elinasi Member

  #11
  Sep 10, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  hivi ndio vitu hata huwa siwazi,ni upuuzi mtupu vyombo vya habari kuonyesha habari nzuri za chama kimoja na mbaya tu za vyama vingine,wanatunyima haki ya habari sahihi na hivyo wananchi kuchagua kiongozi sahihi!
   
 12. p

  politiki JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160

  kamuulize husein Bashe atakwambia mateso yaliyomfika akiwa ndani ya CCM.
   
 13. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mkuu natafuta maana ya 60m na kampeni za CCM. Hii namba inaniumiza kichwa sana kujua huwa inapatikana vipi. Nahisi kimoja labda ni fidia ya miaka 5 yaani mpaka uchaguzi mwingine.
   
 14. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #14
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,447
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  aliowavuna ni matango pori, hizo ni propaganda kama za kule mbeya. nguvu yao ya fedha haiwezi kututisha.tutashida tu.
   
 15. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #15
  Sep 10, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  CHADEMA si chama makini, mtasema sana na bado watahama sana, mna double standard katika kuwashughulikia watu wenu.

  wabaguzi na mko vizuri kwa fitna na majungu.

  hata leo mnyika akitoka mtachafua kuwa si shujaa na mengine.

  maana huyu alikuwa jemedari wenu tena kwa muda mrefu tu.

  nyinyi mmekufa kibudu

  wahoi taabani tafrani jasho linawamwaika
   
 16. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  halafu leo eti mwananchi imeandika ni raia halali wa Tanzania. kazi kweli kweli
   
 17. Y

  Yasebhase Member

  #17
  Sep 10, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani kuhama nyie Hameni tu,.... Ila KURA kwa SLAA! sawa?
   
 18. B

  BRIA Senior Member

  #18
  Sep 10, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Pole sana ndugu yangu usiyejua maana kwani hufahamu Dr Slaa alianguka akiwa anatafuta wadhamini Mwanza...Pole sana mwache aende CCM akafanywe Toilet paper
   
 19. B

  BRIA Senior Member

  #19
  Sep 10, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Pole sana Ubaguzi upi kama aliofanyiwa Bashe mh acha kuwa na Hasira...Mabadiliko yanakuja ndo mana wewe unalaumu CHADEMA TU na si vyama washirika wa CCM vilivyo upinzani Moto huo utasalia Toilet Paper
   
 20. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #20
  Sep 10, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwenye nyekundu, unamaanisha hata nyerere anahusika?
   
Loading...