barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,819
Lowassa akataja idadi ya kula alizopata Znz na zile za JPM.Katika idadi yeye aliongoza,kwa hiyo akawauliza kama yeye alimshinda JPM huko Znz akiwa wa UKAWA,kwanini waseme Shein alimshinda Maalim Seif na huko ndio "ngome" ya CUF?Ukisikiliza "vigongo" vya hotuba hizi basi unaona kwanini Mzee kaamua hii mikutano isiwepo mpaka 2020.Kuna mengi sana yangetibuka.
Maalim Seif akazibua siri,kuwa kumbe hata yale mabadiliko ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya chama yalifanyika bila hata Kinana kuelewa lolote;yaani hata yeye kaja kuyasikia tu mkutanoni kama vile mjumbe kutoka Wilaya ya Kalambo alivyoyasikia mlemle ukumbini Ikulu.MaalimSeif anasema
"Kinana weee... hujui yanayoendelea ndani ya chama chako, utayajua ya nchi wewe? Ikiwa kumefanywa mabadiliko makubwa ya muundo wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya chama chako na pamoja na kuwa Katibu Mkuu hukuwa ukiyajua, umeyasikia vikaoni kama wajumbe wengine, utayajua ya nchi wewe?"
Hii inastua!!Kwamba kumbe hata Kamaradi Kinana yanayoendelea ndani ya chama hayajui??Hii inaweza kuhitaji aya mpya na bandiko jipya.
CCM waitazame Zanzibar kwa jicho la mashauriano na si kwa ubabe.Hata baba wa mgombea wa CCM jana alitoka hadharani na kusema yeye atamuunga mkono mgombea wa CUF,si kwa sababu hampendi mwanae,bali hapendi dhulma ya Chama ambacho mwanae anagombea.
Wakati wa Ukoloni kulikuwa na msemo unasema Hence the saying: 'If the Sultan's drums sounded in Zanzibar, residents of the Great Lakes would dance to their rhythm"
Yanapofukuta Zanzibar,bara na Maziwa makuu hutikisika...Tuyapoze ya Znz,ili tusicheze ngoma yao.