Tujikumbushe nukuu muhimu ya Maalim Seif Sharif Hamad kwenye kampeni za 2020 kuhusu Mpango wa kubadili katiba ili kuongeza muda wa Kutawala!

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Akihutubia Maelfu ya wananchi kwenye kampeni za uchaguzi wa Rais wa Zanzibar mwaka 2020, Maalimu Seif aliwaambia wananchi kuwa upo mpango unasukwa wa kubadili katiba ili Rais aliyeko madarakani sasa aendelee kubaki madarakani baada ya 2025.

Maalimu akaendekea kusema kuwa kikwazo kikubwa cha jitihada hizo ni kura za Zanzibar (Zile theluthi mbili za wabunge kutoka Zanzibar), Kwa hiyo Maalim akasema zinafanyika jitihada za udi na uvumba kuhakikisha wanapatikana wabunge wa chama tawala ili waweze kupitisha hiyo hoja kiulaini.

Kwa kadri mjadala huu wa kubadili katiba unaoendelea nchini, Sijui Maalim angelipokeaje suala hilo na angekuwa na ushawishi gani kwa Wazanzibar na wabunge wake iwapo hoja hiyo ya kubadili katiba ya Muungano ili kumuongezea raisi aliyeko madarakani muda ingekuja kama aivyodokeza maalimu kipindi cha kampeni kuwa kuna mpango huo.

Tunajua msimamo wa Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi kuwa yeye amewahi kupendekeza Rais Magufuli aongezewe muda, Hatujui kana msimamo huo huo unaungwa mkono na mwanae ambaye ni Rais wa Zanzibar sasa, Yaani Hussein Mwinyi, Ila tunachojua ni kwamba Maalim alionya kwenye kampeni juu ya mpango huo. Kwa hiyo ni dhahiri kama hiyo hoja ingeletwa na kuitaka serikali ya Zanzibar iunge mkono sidhani kama Maalim angeiunga mkono, Na kutokana na ushawishi wake mkubwa ndani ya Zanzibar huenda wazanzibar wengi wasingeiunga mkono, na huenda angeweza hata kuishauri serikali ya SMZ isiiunge mkono

Tangulia Maalim

Msikilize Maalim akiwaeleza Wazanzibar juu ya mpango huo wa kubadili katiba

 
Tangulia Maalim japo umemaliza vibaya ila hatutoacha kuienzi misimamo yako kipindi ulipokuwa mpinzani asilia.
 
Maalim seif alikuwa ni zaidi ya taasisi ya wapinzani Zanzibar na Tanzania bara
 
Back
Top Bottom