Elections 2010 Kampeni za CCM Zimeanza Rasmi? Mabango ya Chagua CCM yafunika Dodoma!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,
Nijuavyo mimi, kampeni rasmi za Urais na Ubunge, zitaanza rasmi Tarehe 20 mwezi ujao. Katika pita pita yangu huku na kule, nimetua mjini Dodoma na kushuhudia mji mzima wa Dodoma, umeshehenezwa na mabango rasmi ya CCM yenye picha kubwa za JK na ujumbe mbalimbali ukihimiza Chagua CCM, Chagua Kikwete.

Mabango haya ni mabango rasmi, yaani sio kazi ya bahati mbaya na yamebandikwa mji mzima hali inayopelekea kufuatwa kwa sheria taratibu zote na kanuni zinazotawala uchaguzi.

Swali langu ni jee hii sio CCM inacheza rafu?. Kama ni rafu hivi kweli CCM inaweza kucheza rafu namna hii wazi wazi huku tume ya uchaguzi imewanyamazia?.

Japo nina interest kubwa na harakati za kisiasa humu nchini, natamani sana siasa za fair playing ground, hivyo hiki kinachofanywa na CCM, na kunyamaziwa na Tume ya Uchaguzi, nadhani sio fair play.

Nauliza nini kifanyike au kinaweza kufanyika ili CCM licha ya kushika mpini, lakini pia isicheze rafu?.
 
Wanasheria watuletee tafsiri halisi. kwa mfano mtu akitengeneza wheelcover ya Chagua CCM atakuwa kashaanza rasmi kampeni! wabunge walipokuiwa wanatangaza nia ndani na nje ya bunge walivunja sheria? mrema alipotangaza nia ndani ya vikao vya CCM alivunja sheria?
tusaidiane then tujadili!
 
Mtafuteni Tendwa na Jaji Makame watoe ufafanuzi. Nijuavyo mimi CCM huwa hawaachi kampeni. Wanaunganisha moja baada ya nyingine. Na 2015 kazi ni kubwa zaidi.
 
Nchi ni yao na serikali ni yao hata Tendwa ni wao.....atawafanya nini???
 
Nilimsikia Tendwa akisema, atafanya uchunguzi kama kweli kuna vyama vimeanza kampeni mapema, vitachukuliwa hatua. Siku nilipo yaona mabango ya CCM mji mzima wa Dodoma, kwenye kila mlingoti wa taa za barabarani kuelekea Bungeni, ni mabango ya JK mwanzo mwisho. Kufika Bungeni, nikamuona Tendwa nae alikuwepo, na ni miongoni mwa wageni waalikwa wa ule Mkutano Mkuu wa CCM, hivyo hayo mambo aliyaona kwa macho yake mwenyewe, hahitaji kusubiri ripoti ya uchunguzi, ni ama kutoa karipio kali, ama hiyo adhabu aliyoisema na mabango yabanduliwe kusubiri kipenga kipigwe.
 
Back
Top Bottom