Kampeni ya "Magufuli Baki" yaanzishwa. Yeyote atakayepinga atachukuliwa hatua

John-Pombe-Magufuli-750x375.jpg

Rais John Pombe Magufuli ameendelea kupongezwa na wananchi pamoja na Taasisi za kiraia mbalimbali kutokana na misimamo yake na kazi kubwa anayoifanya ya kupigania rasilimali za nchi, kwa masilahi ya wanyonge na masikini.

Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti leo, Julai 17, 2017 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Masjid Ridhwaa, Alhaj Suleiman Seif Nassor na aliyekuwa mgombea wa CCM wa Ubunge Jimbo la Sengerema kupitia kura ya maoni, Laurence Mabawa.

Wakati akizungumza na wanahabari, Alhaj Nassor amesema bodi hiyo imemamua kumpongea Dkt. Magufuli kutokana na kazi nzuri anayofanya tangu alipoingia madarakani.

Kwa upande wake Mabawa, amesema licha ya kumpongeza Rais Magufuli, ameandaa kampeni kabambe inayojulikana kama ‘Magufuli Baki’ inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwenye mikoa yote nchini, ambapo kupitia mikutano wananchi wenye nia njema watamuomba rais abaki katika msimamo wake wa kuwatetea wanyonge na masikini.

“Kampeni ya Magufuli Baki itahusisha mikoa yote ya Tanzania kwa kuwafikia wananchi wakiwemo wanafunzi wa sekondari kwa kufanya mikutano yenye nia njma ya kumwomba Rais abaki kwenye msimamo wake, kampeni hii itawapa fursa wananchi kutoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wake iwe kwa kupongeza au kukosoa,” amesema.

Katika hatua nyingine, Mabawa amelaani baadhi ya wanasiasa na wananchi wanaotoa lugha za maudhi na kejeli kwa watu wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.

“Niombe TCRA kuwachukulia hatua kali wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatolea maneno ya kejeli na kuudhi watu wanaojitokeza kumpongeza Rais,” amesema.
Hivi huoni soni kilicho katika title na contents si sawa. Huu ndiyo unaitwa uchonganishi. Mmezidi
 
Wapi wamesema atakayepinga atachukuliwa hatua? By the way, wamfuate ikulu wakamwombe abaki, hakuna sababu ya kuingia gharama zote hizo
 
Hili neno "back" huwa linatumika kwa Watu waliopotea au kukamatwa/kutekwa sasa sijajua yeye atafit wap?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Hata Polepole nae ni prospective presidential candidate jamani? Uuuwiiii. I hope you are kidding. Hata muonekano tu unakataa.

Naona dalili ya Rais huyu kutumikia mihula zaidi ya miwili. Haya bila shaka ni habari mbaya kwa wenye nia na urais chamani kama Mwigulu, January, Majaliwa na Polepole ambao nina uhakika kwa nafasi walizonazo hivi sasa wanayakodolea macho Ikulu ya Chamwino.
 
John-Pombe-Magufuli-750x375.jpg

Rais John Pombe Magufuli ameendelea kupongezwa na wananchi pamoja na Taasisi za kiraia mbalimbali kutokana na misimamo yake na kazi kubwa anayoifanya ya kupigania rasilimali za nchi, kwa masilahi ya wanyonge na masikini.

Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti leo, Julai 17, 2017 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Masjid Ridhwaa, Alhaj Suleiman Seif Nassor na aliyekuwa mgombea wa CCM wa Ubunge Jimbo la Sengerema kupitia kura ya maoni, Laurence Mabawa.

Wakati akizungumza na wanahabari, Alhaj Nassor amesema bodi hiyo imemamua kumpongea Dkt. Magufuli kutokana na kazi nzuri anayofanya tangu alipoingia madarakani.

Kwa upande wake Mabawa, amesema licha ya kumpongeza Rais Magufuli, ameandaa kampeni kabambe inayojulikana kama ‘Magufuli Baki’ inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwenye mikoa yote nchini, ambapo kupitia mikutano wananchi wenye nia njema watamuomba rais abaki katika msimamo wake wa kuwatetea wanyonge na masikini.

“Kampeni ya Magufuli Baki itahusisha mikoa yote ya Tanzania kwa kuwafikia wananchi wakiwemo wanafunzi wa sekondari kwa kufanya mikutano yenye nia njma ya kumwomba Rais abaki kwenye msimamo wake, kampeni hii itawapa fursa wananchi kutoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wake iwe kwa kupongeza au kukosoa,” amesema.

Katika hatua nyingine, Mabawa amelaani baadhi ya wanasiasa na wananchi wanaotoa lugha za maudhi na kejeli kwa watu wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.

“Niombe TCRA kuwachukulia hatua kali wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatolea maneno ya kejeli na kuudhi watu wanaojitokeza kumpongeza Rais,” amesema.
Usiseme wananchi wanampongeza, sema wana CCM wasiojitambua ambao kila kitu ni ndiyo. Eti wananchi!! Thubutu! Wananchi walivyopigika wampongeze! Kwa lipi? Kuna mama mmoja na watoto wake alikuwa mstari wa mbele kuikampenia ccm. Anaacha shughuli zake zanutafutaji anaenda kwenye kampeni, nadhani dila la kijani lilimchanganya. Kwa akili zake alidhani pesa ikikosekana itakuwa ni kwa wapinzani tu, vitu vikipanda bei ni kwa wapinzani tu. Sasa juzi kati nimekutana naye analalamikaaa ananiomba buku 2 akanunue mboga, nikamkumbusha alipokuwa akiniimbia kipindi cha kampeni, mtaisoma namba huku akinionesha kichinjio chake. Nikamwambia na bado pumbavu.!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom