Kampeni ya "Magufuli Baki" yaanzishwa. Yeyote atakayepinga atachukuliwa hatua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni ya "Magufuli Baki" yaanzishwa. Yeyote atakayepinga atachukuliwa hatua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Jul 17, 2017.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,078
  Likes Received: 6,258
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais John Pombe Magufuli ameendelea kupongezwa na wananchi pamoja na Taasisi za kiraia mbalimbali kutokana na misimamo yake na kazi kubwa anayoifanya ya kupigania rasilimali za nchi, kwa masilahi ya wanyonge na masikini.

  Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti leo, Julai 17, 2017 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Masjid Ridhwaa, Alhaj Suleiman Seif Nassor na aliyekuwa mgombea wa CCM wa Ubunge Jimbo la Sengerema kupitia kura ya maoni, Laurence Mabawa.

  Wakati akizungumza na wanahabari, Alhaj Nassor amesema bodi hiyo imemamua kumpongea Dkt. Magufuli kutokana na kazi nzuri anayofanya tangu alipoingia madarakani.

  Kwa upande wake Mabawa, amesema licha ya kumpongeza Rais Magufuli, ameandaa kampeni kabambe inayojulikana kama ‘Magufuli Baki’ inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwenye mikoa yote nchini, ambapo kupitia mikutano wananchi wenye nia njema watamuomba rais abaki katika msimamo wake wa kuwatetea wanyonge na masikini.

  “Kampeni ya Magufuli Baki itahusisha mikoa yote ya Tanzania kwa kuwafikia wananchi wakiwemo wanafunzi wa sekondari kwa kufanya mikutano yenye nia njma ya kumwomba Rais abaki kwenye msimamo wake, kampeni hii itawapa fursa wananchi kutoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wake iwe kwa kupongeza au kukosoa,” amesema.

  Katika hatua nyingine, Mabawa amelaani baadhi ya wanasiasa na wananchi wanaotoa lugha za maudhi na kejeli kwa watu wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.

  “Niombe TCRA kuwachukulia hatua kali wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatolea maneno ya kejeli na kuudhi watu wanaojitokeza kumpongeza Rais,” amesema.
   
 2. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 23,679
  Likes Received: 14,631
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo hii ni kusema wanachama wa Chama Cha Makinikia wanapata hadhi ya URAIS.?
   
 3. 2hery

  2hery JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2017
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,227
  Likes Received: 1,550
  Trophy Points: 280
  Huyo mabawa aanze kujipeleka huko..hiyo lugha yake inaudhi wengi..
   
 4. A

  Al-Watan JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 6,675
  Likes Received: 7,648
  Trophy Points: 280
  Nchi ambayo elimu ni anasa, demokrasia ni ndoto na maendeleo ni hadithi.

  Sent from my Kimulimuli
   
 5. pureView Zeiss

  pureView Zeiss JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 5, 2016
  Messages: 574
  Likes Received: 1,238
  Trophy Points: 180
  Si walisema kampeni hamna hadi 2020? Hii ziara ya kutongozea kura sie hatuhitaji kama kero zipo sana tu sio mpaka ufanye ziara

  Hizo pesa za kuzunguka nchi nzima ni bora tungepewa wananchi tu tunywee mnazi
   
 6. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 23,353
  Likes Received: 32,220
  Trophy Points: 280
  Hii nchi tuna hasara kubwa sana!
   
 7. Eternal_Life

  Eternal_Life JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 28, 2016
  Messages: 653
  Likes Received: 1,342
  Trophy Points: 180
  Iyo kampeni ifanyike kolomije na chato tu,mabawa njaa itamuua.
   
 8. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 23,353
  Likes Received: 32,220
  Trophy Points: 280
  Hiyo kampeni ya "Magu baki"" baadae itaguezwa baki mad......ni.

  Alafu sio ndio utawala huu ulisema siasa mpaka 2020?
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 37,664
  Likes Received: 16,783
  Trophy Points: 280
  Hivi wanaofanya hivi maisha yao na ndugu zao yapoje??
  Hawana ndugu waliosomea ualimu arts?
   
 10. Uta Uta

  Uta Uta JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 2, 2016
  Messages: 1,709
  Likes Received: 5,124
  Trophy Points: 280
  Magufuli baki
   
 11. w

  wa mchangani JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 23, 2017
  Messages: 664
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 80
  Wanao sema mtukufu abaki ni wale ambao umri umeenda sana na wasiwasi sana kama miaka saba ijayo itawakuta duniani,tuwe nao makini maana shida zitakazotupata hazitawakuta,ova

  Sent from my Infinix HOT 4 using JamiiForums mobile app
   
 12. Kisesa Yetu

  Kisesa Yetu JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 2, 2015
  Messages: 415
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 60
  Wazalendo wote lazima waunge mkono hii movement

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 13. a

  airbag JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 5, 2016
  Messages: 707
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 180
  Magufuli baki ndiyo nini hiyo?
   
 14. mweusi asili

  mweusi asili JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 11, 2014
  Messages: 484
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  sawa tu maana mkubwa hakosei, ila na sisi waturuhusu tufanye ya UKUTA
   
 15. a

  airbag JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 5, 2016
  Messages: 707
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 180
  Intarahamwe wamevamia nchi.
  Tupo na tutayaona
   
 16. mbalizi1

  mbalizi1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 16, 2015
  Messages: 3,815
  Likes Received: 2,482
  Trophy Points: 280
  Aiseee
   
 17. B

  Boss Mdogo Member

  #17
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 14, 2017
  Messages: 44
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 25
  Mambo mengi hayajakaa vzr hasa Afya namaisha ya Watanzania maskn hafu watu wachache wanaanza kuleta SIASA za kingese hapa! Tunataka wananchi wapate Huduma stahik na sio kumpongeza mtu hapa!

  Sent from my VF695 using JamiiForums mobile app
   
 18. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,099
  Likes Received: 3,329
  Trophy Points: 280
  abaki wapi....?
   
 19. s

  singojr JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 28, 2014
  Messages: 1,724
  Likes Received: 1,582
  Trophy Points: 280
  Hapa ndo tatizo linapoanzia
   
 20. kopites

  kopites JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 28, 2015
  Messages: 4,681
  Likes Received: 3,919
  Trophy Points: 280
  Hizi kampeni zimekua nyingi sasa
   
Loading...